Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 30.12.2019: Xhaka, Haaland, Bony, Lemar, Lamptey

Granit Xhaka Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Xhaka alijiunga na Gunners kutoka Borussia Monchengladbach mwezi Mei 2016

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta ana matumaini kuwa Granit Xhaka, 27, hataondoka klabu hiyo mwezi Januari licha ya kiungo huyo wa Uswizi kuhusushwa na tetesi za kujiunga na Hertha Berlin ya Ujerumani. (Football.London)

Manchester United ilimpatia ofa kubwa zaidi Erling Braut Haaland lakini mshambuliaji huyo wa Norway wa miaka 19, aliamua kujiunga na Borussia Dortmund ili aendelee kukuza kipaji chake(Independent)

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester City na Swansea Wilfried Bony, 31 ,amesema anataka kurejea katika klabu inayoshiriki ligi kuu. (Telegraph)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mshambuliaji wa zamani wa Manchester City na Swansea Wilfried Bony

Mkufunzi wa Chelsea, Frank Lampard amesema klabu hiyo inashauriana na Tariq Lamptey, 19, anayecheza safu ya kulia na nyuma kuhusu mkataba mpya huku mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kukamilika mwisho wa msimu huu. (Goal)

Arsenal lazima itangaze ofa ya kisawasawa kuishawishi Atletico Madrid kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Thomas Lemar, 24, mwezi Januari. (AS, via Mirror)

Real Madrid haitakubali kumpoteza kiungo wa kati na mshambulizi nyota wa Colombia James Rodriguez, 28, kuondoka mwezi Januari. (AS)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Real Madrid haipo tayari kumpoteza nyota wa Colombia James Rodriguez

Arsenal na Tottenham zinajiandaa kulipa £50m kumsajili beki wa kati na nyuma wa RB Leipzig, mfaransa Dayot Upamecano, 21, lakini huenda wakakabiliwa na ushindani kutoka kwa Manchester City. (Daily Star)

Newcastle inashughulikia mpango wa kurefusha mkataba wa kiungo wake wa kati Jonjo Shelvey, 27, ambaye mkataba wake wa sasa unaendelea hadi mwaka 2021. (Chronicle)

Fiorentina huenda ikasitisha mapema mkataba wa mkopo wa winga wa Leicester na Algeria Rachid Ghezzal,27, ambao ulikuwa uendelee kwa msimu mzima huku klabu ya Atalanta ya Italia ikitarajiwa kufaidi kutokana na hatua hiyo. (La Gazzetta dello Sport, via Leicester Mercury)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Fiorentina huenda ikasitisha mapema mkataba wa mkopo wa winga wa Leicester na Algeria Rachid Ghezzal

Manchester United inamfuatilia kiungo wa kati wa Birmingham City wa miaka 16 Muingereza Jude Bellingham. (Sun)

Mkufunzi wa Everton Carlo Ancelotti amesema amekuwa akimfuatilia mshambuliaji wa Toffees Dominic Calvert-Lewin akiwa katika vilabu vingine lakini hakuwahi kupata nafasi ya kumsajili mchezaji huyo wa miaka 22. (Liverpool Echo)

Atletico Madrid huenda ikamsajili mshambuliaji wa Beijing Guoan, Cedric Bakambu, 28, mwezi Januari ikiwa watashindwa kusaini chaguo lao la kwanza Edinson Cavani, 32, kutoka Paris St-Germain. (Mundo Deportivo - Kwa Kihispania)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Atletico Madrid inapania kusajili mshambuliaji wa Beijing Guoan, Cedric Bakambu

Kocha wa Sunderland Phil Parkinson amethibitisha kuwa wanamfuatilia mshambuliaji wa miaka 19 wa Bristol City, Antoine Semenyo. (Chronicle)

Stoke na Huddersfield zinamtaka mshambuliaji Chris Willock, 21, ambaye yuko West Brom kwa mkopo kutoka Benfica. (Mail)

Mkufunzi wa Newcastle Steve Bruce amesema hatawasajili wachezaji wapya mwezi Januari kwa lengo la kushughulikia changamoto ya majeruhi inayowakabili wachezaji wake . (Mail)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii