Shambulio dhidi ya Togo: Miaka 10 imetimu toka timu ya taifa ya Togo iliposhambuliwa na waasi

Togolese gendarmes carry the coffin of one of the victims of the attack, wrapped in the national flag Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Msafara wa wachezaji walionusurika pamoja na wale waliouawa uliwasili Togo Januari 11, 2010

Siku kama ya leo miaka 10 iliyopita yaani Januari 8, 2010, michuano ya Kombe la Afrika ilikuwa katika maandalizi ya mwisho.

Wenyeji wa mashindano walikuwa ni Angola na katika Jimbo la Cabinda ilipangwa kuchezwa kwa mechi za Kundi B.

Timu ya Togo wakati huo ilikuwa chini ya nahodha na mchezaji wao maarufu zaidi Emmanuel Adebayor, ambaye alikuwa mshambuliaji nyota wa klabu ya Machester City wakati huo.

Lakini, kabla ya mashindano kuanza, timu ya taifa ya Togo ilikumbwa na shambulizi la waasi ambalo mpaka sasa bado hawawezi kulisahau.

Haki miliki ya picha Other
Image caption Adebayor aliongea na BBC muda mchache baada ya shambulio

Mpaka inaingia Januari timu ya Togo ilikuwa yenye ari na maandalizi yalikuwa yamepamba moto,. Walikua wamerejea kwenye mashindano baada ya kushindwa kufuzu mwaka 2008.

Lakini pia walikuwa wamepangwa kwenye kundi ambalo lilikuwa na timu vigogo kama Ghana iliyokuwa na kiungo mahiri Michael Essien- na Ivory Caoast chini ya nahodha Didier Drogba.

Kambi yao ya maandalizi ilikuwa katika mji wa Pointe Noir nchini Congo, ambapo ni umbali wa kilomita 100 tu mpaka kwenye mji wa Cabinda uliopo Angola.

Jimbo la Cabinda halipo ndani ya Angola na halina mpaka wa moja kwa moja na sehemu yoyote na badala yake limepakana na Congo Brazzaville na DRC.

Badala ya kusafiri na ndege mpaka mji mkuu wa Angola, Luanda na kisha kupanda ndege tena kuelekea kaskazini, Togo waliamua kutumia usafiri wa barabara. Uamuzi ambao ulizaa madhara makubwa.

Walipofika mpaka wa jimbo la Cabinda walikutana na wanajeshi wa Angola ambao walitakiwa kuwasindikiza mpaka kwenye jiji ambalo walikuwa wacheze mechi zao.

Jimbo la Kabinda lina msitu mnene ambao kuna makundi ya waasi wanaodai uhuru kutoka Angola.

Wachezaji wala hawakujali kuhusu uwepo wa wanajeshi, lakini muda mfupi baadae wakawa wanapigania maisha yao.

"Tulikuwa tuna furaha baada ya kuvuka mpaka. Baadhi yetu tulikuwa tunasikiliza muziki, nakumbuka baada ya dakika 15 toka kuvuka mpaka milio ya risasi ilianza kurindima porini - wote tukacheka na kufanya mzaha. Baada ya hapo mashambulizi makali yakafuata," anaeleza kiungo Junior Senaya.

Risasi zilianza kupenya kwenye gari la wachezaji huku wenyewe wakiwa hawajui nini kinachoendelea.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Afisa wa polisi wa Angola akipiga doria wakati basi lililowabeba wachezaji wa Togo likiwasili Uwanja wa ndege wa Cabinda Januari 10, 2010 ili kuondoka Angola

Afisa habari wa Togo, Stanislas Ocloo, alikuwa amesimama akichukua video ya kuwasili kwao Angola wakati shambulizi likitokea. Alipigwa risasi na kufariki dunia.

Maisha ya kipa Kodjovi Obilale yalibadilishwa kwa sekunde chache, na toka siku hiyo hayupo tena kama ilivyokuwa kabla ya tukio.

"Nilisikia milio ya risasi, kwa haraka nikataka nisogee na kujificha, lakini ikawa kama nimepigiliwa misumari kwenye kiti.

"Hapo ndipo nilipogundua kuwa tumbo langu na miguu yangu ilikuwa inavuja damu. Hapo ndipo nilipoanza kuhamaki. Nikasema: 'Nimepigwa risasi, nisaidieni, nisaidieni, nataka kuwaona watoto wangu. Sitaki kufa hapa.'"

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Raia wa Togo wakisoma magazeti yalivyoripoti shambulio hilo

Kocha msaidizi Amelete Abalo, 54, alikuwa ni moja ya wale ambao walipigwa risasi na kufariki.

Timu hiyo ilishindwa kujinasua kwa kuwa dereva wao - Mario Adjoua - aliumizwa vibaya punde tu shambulio lilipoanza.

Inasadikiwa kuwa tukio hilo lilisalia kwa muda wa dakika 30, na Adebayor amezungumzia juu ya nusu saa hiyo ngumu na ndefu zaidi katika maisha yake.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bango la picha za maombolezo ya kocha msaidizi Amalete Abalo na afisa habari Stanislas Ocloo

"Haikuwa kama mtu mmoja au wawili wanarushia risasi gari letu mara moja au mbili... tulikuwa katikati ya shambulizi kali la risasi kwa nusu saa ma zaidi. Gari limesimamishwa na linamiminiwa risasi, unaweza kufikiri hali ilivyokuwa. Kiukweli, ile ndiyo kumbukumbu mbaya zaidi ya maisha yangu.

"Bila vikosi vya ulinzi nisingekuwa hapa. Labda leo ugekuwa unaongea na maiti yangu."

Namna gani shambulio hilo lilinyamazishwa kuna hadithi zinazotofautiana. Adebayor nasema magari ya wanajeshi yaliwasili na kuwakomboa kutoka eneo hilo huku mashambulizi kutoka msituni yakiendelea. Lakini Seyana anakumbuka kuwa kulikuwa na ukimya.

Hatimaye walifika kwenye jiji la Cabinda, na wale ambao walikuwa hawajapata majeraha wakasaidia kuwabeba wenzao wenye majeruhi na waliopoteza maisha.

"Nilimpeleka mchezaji mmoja hospitali, nilipotoka nikakuta wachezaji wote wanalia, kila mmoja anaongelea familia yake, wanapigia simu mama zao, wanalia kwenye simu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Maafisa wa usalama wakiwa katika doria kwenye hoteli walofikia timu zilizokuwa Cabinda.

Shambulio likawa habari kubwa duniani kote na si kwenye medani ya michezo tu.

Maafisa, mawaziri na wawakilishi wa Shirikisho la Mpira Afrika (CAF) walijazana Luanda, wakiwa na maswali lukuki juu ya kilichotokea. Nani ametekeleza shambulio, na iweje Togo wavunje kanuni ya mashindano kwa kusafiri na basi badala ya ndege.

Mara baada ya shambulizi kundi la Front for the Liberation of the Enclave of Cabinda, ambalo linapigania uhuru wa eneo hilo lilijitokeza na kukiri uhusika. Kundi hilo linapinga uamozi wa Ureno ambayo ilikuwa ni Mkoloni wa Angola kulikabidhi jimbo hilo kwa nchi hiyo katika miaka ya 1950.

Baada ya shambulio kukawa na maswali iwapo Togo ataendelea na mashindano ama la, kambi pia iligawanyika na kuna amaboawalitaka kurudi nyumbani.

Uamuzi mwishowe ukotoka kwa malaka za nchi hiyo jijini Lome, timu ikarejeshwa ili kushiriki mazishi ya wenzao na maombolezo ya kitaifa - uamuzi ambao ukapelekea nchi hiyo kufungiwa na CAF kwa muda mfupi kwa tuhuma za "serikali kuingilia" mambo ya mpira.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Adebayor na wachezaji wenzake wakiwa kwenye maombolezo

Watu wawili waliuawa na baadhi kuumizwa vibaya ikiwemo kipa Obilale.

Mwanzoni iliripotiwa kuwa naye ameuawa, lakini huo ulikuwa uzushi, japo aliumizwa vibaya uti wa mgongo, utumbo, ini na kibofu cha mkojo. Alisafirishwa mpaka Afrika Kusini kuanza matimabu marefu na machungu.

Toka hapo amefanyiwa operesheni kadhaa na ameyajenga maisha yake upya kimwili na kiakili.

"Nimefanya mengi, na nina fahari kuyafanya. Nimerejea shule, nikafanya mitihani na kuandika kitabu," anasema.

Kipa huyo anasema anaendelea kupokea msaada kutoka kwa Adebayor, nyota wa Kameruni Samuel Eto'o nyoita wa Andre na Rahim Ayew.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kipa Kodjovi Obilale aliumizwa vibaya kwenye shambulio hilo - pichani akiwa amelazwa hospitalini nchini Ufaransa mwezi Machi 2010

Hata wale ambao hawakuumizwa kimwili kwenye shambulio hilo wamekutana na changamoto lukuki maishani mwao baada ya shambulio.

Junior Senaya, alikuwa na miaka 25 tu na aliisaidia timu yake kucheza Kombe la Dunia nchini Ujerumani mwaka 2006, lakini maisha yake ya mpira yalikatizwa toka siku hiyo.

"Ilikuwa ni janga kubwa la kisaikolojia, ikafanya mambo yaende juu chini. Sikuweza kurejea kwenye hali ya kawaida... sikuona tena sababu ya kuendelea kucheza mpira kwenye klabu yangu kwa kuwa nilipatwa na mshtuko wa kisaikolojia."

Kwa sasa anasomea ukocha.

Shambulio lilikuwa la nusu saa ama zaidi kidogo. Kwa nini na kwa namna gani lilitokea ni maswali ambayo majibu yake bado yana utata.

Lakini kwa ujumla wake, hakuna mtu ambaye anaweza kubisha juu ya athari endelevu la shambulio lile la basi Cabinda, miaka 10 iliyopita.