Cristiano Ronaldo: Mashabiki wa Korea Kusini wafidiwa baada ya mshambuliaji wa Juventus kukosa kushiriki mechi

Cristiano Ronaldo on the bench Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Cristiano Ronaldo qalisalia miongoni mwa wachezaji wa ziada na hakushiriki katika mechi hiyo

Mahakama moja ya Korea Kusini imeambia mwandalizi wa mechi kuwalipa fidia mashabiki wawili baada ya Christiano Ronaldo kutocheza katika mechi ya kirafiki ya Juventus kama ilivyotangazwa.

Mashabiki waliambiwa kwamba mchezaji huyo wa Portugal atacheza dakika zisizozidi 45 dhidi ya ligi ya K mwezi Julai uliopita.

Lakini hakushiriki katika mechi hiyo kama ilivyotarajiwa. Waandalizi , The Fasts wameagizwa kulipa £240 kwa mashabiki wawili.

Fedha hizo zinashirikisha £194 kwa shinikizo la kiakili lililowaathiri mashabiki hao kulingana na wakili Kim Min-ki.

Kim ambaye aliwasilisha kesi hiyo alisema: The Fasta iliwadanganya mashabiki wa Ronaldo kwa faida yao wenyewe. Kwa mashabiki wa Ronaldo , hii ni sawa na kumkosa mchezaji ambaye wangemuenzi na kumshabikia maisha yao yote.

Kim pia aliambia chombo cha habari cha Reuters alikuwa akiwakilisha walalamishi wengine 87 katika kesi nyengine zinazohusiana na mechi hiyo ambayo ilimalizika 3-3.

Tiketi 65 za mechi hiyo ziliuzwa zote chini ya dakika tatu huku Ronaldo akiwekwa katika matangazo.

Mashabiki walikasirika wakati walipogundua kwamba mchezaji huyo hatoshiriki katika mechi hiyo, kitu kilichowafanya kuimba nyimbo za kumshabikia Lionel Messi.

Shirikisho la soka nchini Korea Kusini pia lilituma barua ya pingamizi kwa Juventus kwa kukiuka kandarasi.

The Fasta haijatoa tamko lolote.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mashabiki waliovaia kama Ronaldo mjini Seoul

Mada zinazohusiana