Coronavirus: Odion Ighalo atengwa na wachezaji wengine wa Man United

Odion Ighalo afanya mazoezi pekee Manchester Haki miliki ya picha Getty Images

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Man United Odion Ighalo anafanya mazoezi mbali na uwanja wa klabu hiyo wiki hii kama hatua ya tahadhari baada ya kuwasili kutoka China.

United imeamua kutumia sera hiyo kutokana na hatari inayosababishwa na virusi vya corona.

Waliamua kutosafiri na mchezaji huyo wakati wa mapumziko ya kipindi cha baridi nchini Uhispania kutokana na wasiwasi kwamba hatoruhusiwa kuingia Uingereza.

Huwezi kusikiliza tena
Pele 'aibika' kutokana na hali yake ya kiafya

Ighalo mwenye umri wa miaka 30 anatarajiwa kusafiri na kikosi hicho kwa mechi ya siku ya Jumatatu dhidi ya Chelsea.

BBC inaelewa kwamba Ighalo amekuwa akifanya mazoezi kutokana na usaidizi wa klabu hiyo kwa kutumia mkufunzi binafsi ili kumuandaa kwa mechi ya ligi ya Premia dhidi ya Chelsea.

Mazoezi hayo yamekuwa yakifanyika katika kituo cha mchezo wa Taekwondo karibu na uwanja wa Etihad na mahala ambapo amekuwa akiishi tangu kuwasili kwake nchini Uingereza siku 11 zilizopita.

Ighalo alijiunga na United kwa mkopo wa kipindi kilichosalia cha msimu kutoka kwa timu ya ligi ya China Shanghai Shenua.

Idadi ya vifo nchini China vinavyotokana na virusi vya Corona imefikia 1,350 huku kukiwa na takriban maambukizi 60,000 kwa jumla.

Mashindano kadhaa ya michezo imefutiliwa mbali nchini China na maeneo ya mashariki ikiwemo mashindano ya magari ya Formula One Grand Prix.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii