Tetesi za soka Ulaya Jumanne 18.02.2020: Sterling, Guendouzi, Smalling, Werner, Soumare

Chris Smalling

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Smalling kwa sasa anacheza kwa mkopo na klabu ya AS Roma ya Italia.

Tottenham na Everton wanamuwania beki wa Manchester United Chris Smalling, 30, ambaye anachezea kwa mkopo na klabu Roma. (Corriere dello Sport - in Italian)

Kiungo Mfaransa Matteo Guendouzi, 20, anakabiliwa na mapambano ya kusalia katika klabu ya Arsenal baaada ya kuachwa kwenye kikosi cha klabu hiyo kwenye mchezo wa Jumapili dhidi ya Newcastle. (Mirror)

Guendouzi aliachwa baada ya kugombana na kocha wa Arsenal Mikel Arteta na makocha wasaidizi wakati wa mapumziko mafupi ya katikati ya msimu jijini Dubai. (Goal)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kiu ya Sterling kunyakua Champions League itabaki kuwa ndoto kwa miaka mitatu ijayo.

Winga Raheem Sterling, 25, ataendelea kusalia Manchester City licha ya klabu hiyo kupigwa marufuku kushiriki michuano ya Ulaya, amedai wakala wake. (Manchester Evening News)

Barcelona wanatarajiwa kufanya usajili wa dharura kwa kumnyakua mshambuliaji wa zamani wa Middlesbrough Martin Braithwaite, 28, kutoka klabu ya Leganes. (Mundo Deportivo, via Teeside Gazette)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Werner (kushoto) yupo kwenye rada za Klopp licha ya mazungumzo rasmi ya usajili kutoanza.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp yungali anavutiwa na mshambuliaji wa Kijerumani Timo Werner, 23, lakini bado klabu ya Liverpool haijaabzisha mazungumzo na RB Leipzig juu ya usajili wa nyota huyo. (Independent)

Kocha wa klabu ya Lille ya Ufaransa, Christophe Galtier anadai hakuna uhasama baina ya klabu hiyo na kiungo wake Mfaransa Boubakary Soumare, 20, ambaye anawania na vilabu vya Manchester United, Liverpool na Chelsea. (Express)

Tetesi Bora za Jumatatu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Pep Guardiola

Pep Guardiola atasalia kuwa mkufunzi wa Manchester City hata kama klabu hiyo itashindwa kukabiliana na marufuku ya kutoshiriki Champions League kwa miaka miaka miwili . (Mirror)

Mchezaji wa zamani wa Juventus Alessandro del Piero anaamnini Guardiola atakuwa 'kiungo muhimu' katika klabu hiyo. Meneja huyo wa City ahusishwa na tetesi za kuchukua nafasi ya Maurizio Sarri mjini Turin. (Sky Sports)

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer haamini kuwa wakishindwa kujikatia tiketi ya kushiriki Champions League kutaathiri mpango wa uhamisho wa klabu hiyo. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ighalo anasema kuichezea United ni kukamilika kwa ndoto zake

Solskjaer anasema uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji wa Nigeria wa miaka 30, Odion Ighalo kuja Manchester United kutoka Shanghai Shenhua huenda ukafanywa wa kudumu. (Manchester Evening News)

Barcelona italazimika kumjumuisha mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann katika mpango wowote utakaojaribu kuishawishi Inter Milan kuwauzia Lautaro Martinez. (Sun)