Pogba si mali ya mkufunzi wa Manchester United Solskjaer kulingana na Raiola

Ole Gunnar Solskjaer na Paul Pogba

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Paul Pogba amefanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu mara mbili msimu huu

Paul Pogba sio mali ya mkufunzi wa Manchester Ole Gunnar Solskjaer, asema wakala wa kiungo huyo wa kati Mino Raiola.

Kiungo huyo wa Ufaransa anaendelea kuuguza jeraha la kifundo cha mguu lakini Raiola anasema anaweza kurudi mwisho wa msimu huu. Solskjaer alijibu kwa kusema kwamba hajazungumza na Raiola na kwamba Paul ni mchezaji wa Man United na sio wa Mino.

Katika chapisho katika mtandao wa kijamii, Raiola baadaye alisema kwamba anatumai kwamba raia huyo wa Norway hasema kwamba Paul ni mfungwa wake.

Raiola aliongezea: Paul sio wangu na pia sio mali ya Solskjaer, Paul ni Paul Pogba. Kabla ya Solksjaer hajatoa tamko kuhusu suala lolote anasema anapaswa kujihabarisha vizuri zaidi kuhusu yale yaliosemwa.

''Hadi kufikia sasa pengine nilikuwa mzuri sana kwake . Solskjaer anafaa kukumbuka kuhusu mambao aliomwambia Paul mwisho wa msimu uliopita. Nadhani Solskjaer huenda amekasirishwa na vitu fulani na sasa anachanganya mambo . Nadhani kwamba Solskjaer ana maswala mengine ambayo yanamfanya kuwa na wasiwasi''.

Pogba ameichezea mara nane pekee United msimu huu na mara mbili tangu mwezi Septemba , lakini Solskjaer amesema kwamba anakaribia kurudi katika mazoezi siku ya Jumanne.

Mara ya mwisho kuichezea Man United ni wakati alipochezeshwa kama mchezaji wa ziada wakatii ambapo United iliilaza Newcastle 4-1 siku ya Boxing Day.

Kufuatia ushindi wa United wa 2-0 dhidi ya Chelsea siku ya Jumatatu, Solkjaer alisema kwamba haoni haja ya kuzungumzia kuhusu Raiola kupitia vyombo vya habari , ''naweza kujizungumzia''.

Alipoulizwa iwapo atazungumza na ajenti huyo alisema ''pengine hapana''.

Maelezo ya picha,

Ajenti wa Paul Pogba Mino Raiola

Mshambuliaji wa zamani wa Ligi ya Uingereza Chris Sutton anasema kwamba Pogba anafaa kusawazisha swala lote hilo na kutoa msimamo wake.

''Kwa nini Ole Gunnar Solskjaer ajitokeze na kuanza kujibu maswali kuhusu matamshi ya ajenti''? Sutton aliambia BBC radio 5 Live.

''Paul Pogba ni mchezaji wa Man United. amekuwa na fursa msimu huu kusema kwamba nitasalia Man United. Anachapisha mambo mengine katika Instagram na baadaye anakuja kutuambia kwamba atasalia katika klabu na hutaki ajenti kuzungumzia , hivyo ndio jinsi watu wengi wataiona hali hii- Mino Raiola anazungumza na kumwakilisha Paul Pogba.