Mpambano kati ya Deontay Wilder na Tyson Fury II: Mike Tyson ana muunga mkono Fury

Deontay Wilder v Tyson Fury

Chanzo cha picha, Getty Images

Wiki hii mpambano ambao umekuwa ukizungumziwa katika ndondi ni kuhusu ,Je Tyson Fury atampiga Deontay Wildena kuwa bingwa wa mara mbili wa kombe la dunia?

Wilder dhidi ya Fury II - ni nani atashinda?

Kunanafasi moja tu ya kuanzia -mwanamasumbwi dhidi ya mfalme wa knock-out . Ni Deontay Wilder dhidi ya Tyson Fury II. Na zitapigwa wikendi hii.

Baada ya mpambano wao wa kwanza katika droo iliyozua utata, wale waliokua katika mchezo wamekua wakifanya ubashiri wao.

Gwiji wa ndondi Mike Tyson anamshabikia wajina wake dhidi ya mmarekani mwenzake.

"Kila mara ninamshabikia kwasababu alipewa jina langu ," aliiambia BT Spot.

Lakini bingwa wa dunia David Haye hamuungi mkono muingereza mwenzake, ambapo aliliambia jarida la Express kwamba anatarajia Wilder atamaliza akiwa wa kwanza.

Na promota Eddie Hearn aliiambia IFL TV kwamba anaenendelea kubadili mawazo yake mara kwa mara ingawa (wakati anaandika ) anadhani Wilder atashikilia mkanda wake WBC.

THakuna mtu wa wazi ninayemshabikia zaidi na ndio maana huu ni mpambano mkali unaosubiriwa kwa hamu zaidi wa uzani mzito katika miaka ya hivi karibuni.

Fury binafsi alibashiri nock-out katika mzunguko wa pili. Hakuna mengi unayoweza kupata kutoka katika rekoti yake , au kutoka kwenye mpambano wake wa awali T, hilo linaashiria kuwa itatokea. Wengi wa mashabiki wanadhani kuwa ni suala la Fury kupitia kwa point na Wilder kupitia nock-out...

Chanzo cha picha, Twitter

Kwa hiyo je mshindi wa Jumamosi usiku atakua ndiye msindi wa uzani wa juu katika dunia?

Ni vigumu kupinga hilo - ingawa Muingereza Anthony Joshua, anayeshikilia mikanda mingine anaweza kuwa na la kusema juu ya hilo.

Lakini kama jamaa huyu alivyoelezea vizuri kwa ufupi, kuna ushindani mkubwa sana juu ya kitengo cha uzani wa juu zaidi kwa sasa na mchezo wa ndondi ndio unapendwa zaid …

Chanzo cha picha, Twitter

Kumekua na mbwembwe nyingi kuhusiana na mpambano huu, ili kukupa uhondo huo hili ni mojawapo ya matangazo maarufu ya kunadi mpambano huo- Hii itakukupa kumbukumbu za nyuma hadi miaka ya 1990...

Lakini ni nani ambaye mashabiki wangetaka kumuona akipigana baada ya mpambano huu?

Chanzo cha picha, Twitter

Dubois ajitolea kupambana na Warren

Warren huenda alipoteza ushindi Warrington kutoka kwa kundi lake la wapiganaji lakini kuna habari njema kutoka kwa promot wake wiki iliyopita huku bondia ambaye hajashindwa wa Uingereza wa uzani wa juu na mmoja wa wanamasumbwi wanaotumainiwa katika ndodi Daniel Dubois alirefusha mkataba wake kwa kusaini mkataba wa miaka mitano.

Dubois anapiga mazoezi kwa ajili ya mpambano wa mpambano wa Waingereza wote ukipenda all-British fight dhidi ya Joe Joyce tarehe 11 Aprili katika uwanja wa London O2 Arena.

Na baada ya kusikia kuhusu taarifa ya kurefushwa kwa mkataba , meneja wa Joyce Sam Jones alikua na ujumbe huu kwa Warren na Dubois…

Chanzo cha picha, Twitter

Joyce alibadili mkufunzi tena

Kabla ya mpambano na Dubois, Joyce alikua amejiunga upya na kocha wa Cuba Ismael Salas.

Mwanamasumbwi huyo wa uzani wa juu anaonekana kuwa na kitu kizuri kinachoendelea na mkufunzi wake Adam Booth, ambaye alikua maarufu kwa kumuongoza David Haye hadi kuchukua taji la dunia, lakini kwa sasa alianza kambiyake na Salas nje katika Las Vegas.

Pia kwasababu aliwahi kufanykazi chini ya kocha wa Mexico Abel Sanchez, mashabiki wanauliza iwapo joyce anastahili kubadilisha makocha wakati ambapo amekuwa na mapigano ya kulipwa mara 10 pekee.

viatu vilivyotengenezwa kwa ajili ya... pigano?

Hata hivyo, ni jambo linalotufurahisha kumuona Joyce akishirikiana tena na Salas.

Sababu kuu ikiwa ni kurejea kwa viatu maalum vilivyopendekezwa na kocha huyo.

Viatu hivyo huhivaa kukabiliana na wanamasumbwi wenzake ambao huwa na kimo kirefu kumliko yeye.

Angalia picha inayofuata alipokuwa na David Haye in 2018…

Chanzo cha picha, Getty Images

Nbado ni gumzo mitandaoni miaka miwili baadae...