Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 21.02.2020: Skriniar, Tah, Alonso, Klopp, Hodgson, Lallana

Jurgen Klopp

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Wachezaji wa Atletico wanamtaka Jurgen Klopp kutizama mapungufu ya timu yake badala ya kuwakosoa.

Wachezaji wa Atletico Madrid walishikwa na hasira na kushangazwa baada ya kukosolewa na kocha wa Liverpool Jurgen Klopp. Atletico iliwafunga Liverpool 1-0 Jumanne katika raundi ya kwanza ya hatua ya mtoano ya Kombe la Mabingwa Ulaya, wachezaji wa Atletico wanamtaka Klopp kutizama mapungufu ya timu yake badala ya kuwakosoa. (ESPN)

Manchester City na Barcelona wanaminyana kumsajili beki wa Inter Milan na Slovakia Milan Skriniar, 25, na klabu itakayofanikiwa kumnyakua itabidi itoe dau la zaidi ya pauni milioni 75. (Calciomercato)

Arsenal wanapanga kumsajili beki wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Jonathan Tah ambaye kwa mujibu wa mkataba wake anathamani ya pauni milioni 34. (Bild - in German)

Chanzo cha picha, TF-Images

Maelezo ya picha,

Jonathan Tah

Beki wa pembeni wa Chelsea Marcos Alonso, 29, bado yungali anawaniwa na Inter Milan lakini klabu yake inatarajiwa kuongeza bei ya mauzo ya mchezaji huyo. (Calicomercato - in Italian)

Mwenyekiti wa Crystal Palace Steve Parish anaamini wataendelea kusalia na kocha Roy Hodgson baada ya kumpatia mkataba mpya. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mkataba wa Chelsea na Willian kufikia kikomo mwishoi mwa msimu.

Winga wa Brazil Willian, 31, ambaye mkataba wake na Chelsea unamalizika mwishoni mwa msimu anasema hana mpango wa kuihamisha familia yake kutoka kwenye nyumba yao jijini London. (Mail)

Klabu ya Inter Milan inajipanga kutoa wachezaji kwenda klabu ya Verona kama sehemu ya mpango wa kumnasa beki wa Albania Marash Kumbulla, 20, ambaye pia anawaniwa na Liverpool. (Inside Futbol)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Marash Kumbulla anawaniwa na Inter Milan na Liverpool

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer alikuwa akitaka kumsajili kiungo Christian Eriksen, 28, kabla raia huyo wa Denmark kuhamia Inter Milan akitokea Tottenham. (Manchester Evening News)

Klabu za Juventus na Inter Milan wanavutiwa kumsajili beki wa pembeni wa Chelsea Emerson Palmieri, 25, lakini bado ofa rasmi hazijatumwa ajenti wake abainisha. (Goal.com)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

David Luiz alishinda Kombe la Europa msimu uliopita na Chelsea, anaamini msimu huu atashinda tena na Arsenal.

Beki wa Brazil David Luiz, 32, anaamini Arsenal wana kiwango cha ubora cha kuwafanya washinde Ligi ya Europa msimu huu baada ya kushindwa msimu uliopita. (Evening Standard)

Klabu ya Real Madrid wanamfuatilia kiungo wa Rennes na Ufaransa Eduardo Camavinga, 17. (Marca)

Tetetsi Bora za Alhamisi 20.02.2020

Mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi, 32, amepigiwa simu na klabu ya LA Galaxy kujadili uhamisho wa kuelekea Ligi ya Soka ya Marekani (MLS). (Express)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Lionel Messi akiri kuwa anahisi kuna "mambo ya ajabu" yanaendelea Barcelona.

Messi amekiri kuwa anahisi kuna "mambo ya ajabu" yanaendelea Barcelona huku kukiwa na ripoti kuwa klabu hiyo ilikodi kampuni ya mitandao ya kijamii kukashifu wachezaji wake. (Mundo Deportivo, via Mail)

Hata hivyo, Messi yungali anaiona Barcelona kama nyumbani kwake licha ya tetesi za kutaka kuihama klabu hiyo. (ESPN)

Klabu ya Manchester United inaimani kuwa itamnasa mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund na timu ya taifa ya England Jadon Sancho, 19, mwishoni mwa msimu, lakini kwanza itawapasa kufuzu kwa mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Man United inabidi wafuzu Champions League kumnasa Jadon Sancho

Klabu ya Juventus imewaorodhesha mshambuliaji wa Manchester City na Brazil Gabriel Jesus (22) pamoja na mshambuliaji wa Paris St-Germain na Argentina Mauro Icardi (27) kama kipaumbele katika dirisha la usajili la mwishoni mwa msimu. (Tuttosport - in Italian)

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner

Mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner, 23, amesema kuwa anajisikia fahari kuhusishwa na klabu ya Liverpoollakini anahisi kuwa huenda hayupo tayari kujiunga na klabu hiyo ambayo anasema ni "timu nzuri zaidi duniani." (Metro)

Mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 33, amesisitiza kuwa atacheza kwa moyo wote kwa Chelsea licha ya kushindwa kuihama klabu hiyo katika dirisha la usajili la mwezi uliopita. (Mirror)