Barcelona 5-0 Eibar: Braithwaite asema hatoosha tishati yake baada ya kumkumbatia Lionel Messi

Chanzo cha picha, Getty Images
Martin Braithwaite aliifungia Middlesbrough magoli manane na sasa anashirikiana na Lionel Messi Barcelona
Mchezaji mpya wa Barcelona aliyesajiliwa kwa sababu za dharura katika klabu hiyo Martin Braithwaite alifanya mzaha kwamba hatofua fulana yake baada ya kumkumbatia Messi alipompatia pasi iliosababisha goli moja kati ya matano ya Barcelona dhidi ya klabu ya Eibar.
Barca waliruhusiwa kumsaini aliyekuwa mchezaji wa Middlesborough wiki hii, na alitoka katika benchi na kuchangia goli la mwisho la Messi hatua inyoongeza shinikizo kwa viongozi wa ligi Real Madrid.
''Messi alinipongeza, ni mtu muzri sana na alijaribu kunifanya nijisikia nyumbani uwanjani kwa kunipigia pasi mara kwa mara'', alisema Braithwaite, mwenye umri wa miaka 28.
''Nafurahia sana kumsaidi Messi kufunga goli''.
'Tumefanya usajili mzuri sana'
Messi alifunga magoli matatu katika dakika 26 za kwanza kabla ya kuongeza la nne kwa mchango wa Braithwaite huku Barcelona ikipanda juu pointi mbili.
Baada ya mechi kuanza polepole, Messi alifunga goli la kwanza baada ya kuwazunguka walinzi na kufunga goli zuri alipompiga kanzu Marko Dmitrovic baada ya dakika 14.
Huku kipindi cha mapumziko kikikaribia Messi alivamia tena ngome ya Eibar na kufunga goli la pili kabla ya mshambuliaji huyo wa Argentina kufunga goli lake la tatu baada ya kupata mpira uliowatoka wachezaji wa Eibar na kuihakikishia timu yake uongozi thabiti kabla ya mapumziko.
Chanzo cha picha, Getty Images
Messi ndiye mfungaji magoli mengi wa la Liga kufiki sasa akiwa na magoli 17
Mkufunzi Quique Setien alikiri kwamba alishanganzwa na machango wa mchezaji wake mpya .
''Braithwaite alichaza zaidi ya alivyotarajiwa'', alisema Setien