Tetesi za soka Ulaya Jumatatu tarehe 24.02.2020: Tetesi za uhamisho wa Zlatan, Smalling, Mkhitaryan, Phillips, Kostic

Mswisi Zlatan Ibrahimovic, mwenye umri wa miaka 38, amefanya marekebisho ya kipengele iwapo Wataliano watafuzu kuingia Championi Ligi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mswisi Zlatan Ibrahimovic, mwenye umri wa miaka 38, amefanya marekebisho ya kipengele iwapo Wataliano watafuzu kuingia Championi Ligi

Mkurugenzi wa masuala ya kiufundi wa klabu wa AC Milan Paolo Maldini anasema Zlatan Ibrahimovic, mwenye umri wa miaka 38, amefanya marekebisho ya kipengele cha mkataba wake iwapo Wataliano watafuzu kuingia Klabu Bingwa Ulaya. (Mail)

Meneja wa Roma Paulo Fonseca anataka kusaini mkataba na wachezaji Chris Smalling, wa Manchester United mwenye umri wa miaka 30- ambaye pia ni mlinzi wa England, na kiungo wa kati wa Arsenal raia wa Armenia Henrikh Mkhitaryan, mwenye umri wa miaka 31, kwa mikataba ya kudumu. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Meneja wa Roma Paulo Fonseca anataka kusaini mkataba na wachezaji Chris Smalling

Wolves na Burnley wako tayari kukabiliana na Sheffield United kwa ajili ya kumpata kiungo wa kati wa Leeds Muingereza Kalvin Phillips, mwenye umri wa miaka 24. (Daily Star)

Kocha wa Paris St-Germain Thomas Tuchel anaaminiwa kuwa katika maungumzo na Bayern Munich juu ya uhamisho wa kumrejesha katika nchi yake ya asili ya Ujerumani. (90 Min)

Barcelona wanakaribia kukamilisha mpango wa kusaini mkataba na Hugo Guillamon, maarufu kwa kwa pasi za guu lake la kushoto ambaye anacheza safu ya kati-nyuma mwenye umri wa miaka 20, katika timu ya wachezaji wa akiba ya Valencia ya Mestalla. (Sport)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wolves na Burnley kila upande unamtaka kiungo wa kati wa Leeds Muingereza Kalvin Phillips

Crystal Palace wanamsaka mchezaji wa klabu ya Eintracht Frankfurt Filip Kostic kama mchezaji mbadala wanayeweza kumlipa pauni milioni £10m alizokua akilipwa mshambuliaji wa safu ya kati Wilfried Zaha, 27. Winga huyo wa Serbia mwenye umri wa miaka 27, aliwahi wakati mmoja kulengwa na klabu ya Liverpool. (HITC, via Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jack Tucker anawindwa na Aston Villa na West Ham

Aston Villa na West Ham kwa pamoja zinamfuatilia kwa karibu mchezaji aliyethamanishwa kwa viwango vya juu wa klabu ya Gillingham Muingereza Jack Tucker mwenye umri wa miaka 20 anayecheza safu ya kati ya ulinzi. (Birmingham Mail).

Aston Villa wanamfuatilia kwa kwa karibu mshambuliaji wa miaka 13 Daniel Akinleye, ambaye kwa sasa anachezea timu ya ufaransa ya Quevilly-Rouen Metropole, lakini mvulana huyo mdogo amefichua nia yake ya kufuata nyayo za mchezaji wa kimataifa wa Nigeria mwenye umri wa miaka 30, Odion Ighalo, 30, na kuichezea Manchester United. (Birmingham Mail)

Rangers wanamtaka mchezaji wa West Brom Rayhaan Tulloch. Winga huyo Muingerea mweye umri wa miaka 19- amemaliza mkataba wake katika Hawthorns msimu huu. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Manchester City watafanya mazoezi katika uwanja wa Atletico Madrid Jumatano asubuhi kabla ya mechi yao na majirani zao Real katika Bernabeu usiku huo.

Manchester City watafanya mazoezi katika uwanja wa Atletico Madrid Jumatano asubuhi kabla ya mechi yao na majirani zao Real katika Bernabeu usiku huo.

Wanda Metropolitano ulikua ndio ilipochezwa fainali ya mwisho uliopita ya Championi Ligi uwanja wa msimu uliopita. (AS)

Kijana mdogo nyota wa Real Madrid Rodrygo atakosa mechi ya Jumapili ijayo nyumbani na Barcelona kutokana na adhabu aliyopewa ya kutocheza iliyotokana na kumuudhi mlindalango wa timu pinzani baada ya kuifungia klabu yake goli la pili . Kijana huyo mwenye umri wa miaka 19 kutoka Brazil alitarajiwa kurejea katika kikosi cha timu ya kwanza baada kujeruhiwa kwa Eden Hazard. (Goal)

Chanzo cha picha, PEREZ MECA/MB MEDIA

Maelezo ya picha,

Gareth Bale ameshinda ligi ya Champions mara nne akiwa na Real Madrid

Kiungo wa kati wa Manchester United na Serbia Nemanja Matic, 31, anakata kusalia Old Trafford baada ya mkataba wake wa sasa kukamilika msimu huu. (Sunday Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Nemanja Matic anayechezea Serbia

West Ham United wako katika nafasi nzuri ya kumsajili mshambuliaji Amiens, Serhou Guirassy kwa £23m ingawa Brighton naTottenham pia nao wameonesha nia ya kumsajili. (Sun on Sunday)

Mchezaji wa Manchester City, Under-21, Phil Foden, 19, anasema kwamba anafurahia kusalia katika klabu hiyo badala ya kuhamia kwengine kwa mkopo ili aweze kupata nafasi ya kujumuishwa katika orodha ya wachezaji wa kila mara wa timu. (Manchester Evening News)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Werner, katikati, akifunga bao baadaya kupata penalti dhidi ya Tottenham

Chelsea wameonyesha nia ya kumsajili mchezaji wa Inter Mauro Icardi, ambaye yuko Paris St-Germain kwa mkopo na huenda wakamtafuta wakati wa dirisha la usajili litakapofunguliwa. (Sport Witness)

Sheffield United itaweka £20m katika hatua ya kutaka kumsajili mlinzi wa timu ya Leeds United nchini Uingereza, 23. (Sun on Sunday)