Tetesi za soka Ulaya Jumanne tarehe 25.02.2020: Aubameyang, Werner, Sancho, Fuchs, Matic, Xhaka

Pierre-Emerick Aubameyang

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang

Arsenal huenda ikalazimika kumuuza mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang ikiwa watashindwa kufikia makubaliano kuhusu masharti ya mkataba mpya, mchezaji huyo mkataba wake utakwisha mwaka 2021. (Star)

Kocha wa zamani wa Everton Sam Allardyce amesema alijaribu kumsajili Aubameyang kutoka Borussia Dortmund kabla ya mshambuliaji huyo kujiunga na washika bunduki (Talksport)

Winga wa England Jadon Sancho, 19, anaweza kusalia na Dortmund baada ya msimu huu ingawa alikuwa akihusishwa na taarifa za kuhamia Chelsea, Liverpool au Manchester United. (Ruhr Nachrichten - in German)

Leicester City inafikiri kumpatia mkataba mpya Christian Fuchs, 33, wakati mchezaji huyo wa nafasi ya ulinzi akikaribia kumaliza mkataba wake. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Winga wa England Jadon Sancho, 19, anaweza kusalia na Dortmund

Kiungo wa kati wa Manchester United Nemanja Matic, 31, anatarajiwa kuondoka wakati mkataba wake utakapokwisha mwishoni mwa msimu huu, huku mawakala wakiendelea kutathimini timu, lakini AC Milan hawana mpango wa kumsajili kutokana na matakwa yake ya mshahara. (Calciomercato)

Kiungo wa kati wa Arsenal Granit Xhaka, 27, amesema anahofia hataichezea klabu hiyo tena baada ya kupoteza unahodha wake.(Evening Standard)

Roma na Manchester United wamebaki kwenye mazungumzo kuhusu mchezaji wa nafasi ya ulinzi Chris Smalling, 30, na mpango wa kuhamia Italia kwa mkataba wa kudumu. (Star)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Christian Fuchs

Smalling anasema ana ''uchaguzi muhimu wa kufanya'' kubaki na Manchester United au kuhamia Roma kwa mkataba wa kudumu.(Sky Sports)

Baba wa beki wa kushoto wa Chelsea Marcos Alonso, 29, amedokeza kuwa kijana wake atarejea Italia, kwa kuwa aliichezea Fiorentina kabla hajahamia Stamford Bridge. (Calciomercato - in Italian)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Granit Xhaka

Kiungo wa kati wa Morocco Hakim Ziyech, 26, amesema Kocha wa Chelsea Frank Lampard amechangia kwa kiasi kikubwa katika uamuzi wake wa kuhamia Blues akitokea Ajax. (Mail)

Manchester United itafanya majaribiokwa wachezaji wawili wa Poland wanaocheza nafasi ya ulinzi Mateusz Lipp, ambaye ni mchezaji wa shule ya soka ya Akademia 'Ruch' Chorzow ambaye alishawahi kufanya majaribio na Arsenal na Sampdoria na Radoslaw Sewerys, anayechezea Korona Kielce. (Express)