Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 26.02.2020: Lingard, Pereira, Grealish, Aubameyang, Guardiola

Lingard

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jesse Lingard huenda akauzwa mwishoni mwa msimu

Manchester United inaweza kuwauza mshambuliaji wa England Jesse Lingard, 27, na kiungo wa Brazil Andreas Pereira, 24, mwishoni mwa msimu. (Express)

United wameongeza kasi katika mpango wao wa kutaka kumsajili kiungo na nahodha wa Aston Villa Jack Grealish, 24. (Manchester Evening News)

Arsenal inaweza kupokea ofa za usajili wa mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang 30. Mkataba wake na Arsenal unamalizika mwakani. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mkataba wa Aubameyang na Arsenal kuisha mwakani.

Hata hivyo, mshambuliaji huyo wa Gabon bado hajasema kuwa hatasaini mkataba mpya na Arsenal japo mazungumzo na klabu yamedumaa. (Metro)

Rais wa klabu ya Juventus Andrea Agnelli amesema klabu inataka kumchukua kocha wa Manchester City Pep Guardiola. (Manchester Evening News)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Juventus wapanga kumsajili Pep Guardiola.

Barcelona watatakiwa kuilipa Liverpool pauni milioni 225 ili kumsajili winga Msenegali Sadio Mane, 27.(Mirror)

Manchester City ipo hatarini kuwapoteza baadhi ya wachezaji wake nyota, akiwemo mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 25, endapo watatwaa ubingwa wa if they win Champions League msimu huu. (ESPN)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Sergio Ramos

Beki wa Real Madrid Sergio Ramos, 33, hana haraka ya kuingia katika mazungumzo ya mkataba mpya huku akisema mahusiano yake na Madrid ni mazuri.(Goal)

Kocha wa timu ya taifa ya UhispaniaLuis Enrique ameingia mashaka juu ya kiwango cha kipa wa Chelsea Kepa Arrizabalaga, 25, kuelekea kwenye Kombe la Mataifa ya Ulaya kwa kutopata muda mwingi wa kucheza. (AS - in Spanish)

Tetesi Bora za Jumanne 25.02.2020

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Je, Jadon Sancho kuelekea England ama kusalia Ujerumani?

Winga wa England Jadon Sancho, 19, anaweza kusalia na Dortmund baada ya msimu huu ingawa alikuwa akihusishwa na taarifa za kuhamia Chelsea, Liverpool au Manchester United. (Ruhr Nachrichten - in German)

Leicester City inafikiri kumpatia mkataba mpya Christian Fuchs, 33, wakati mchezaji huyo wa nafasi ya ulinzi akikaribia kumaliza mkataba wake. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Christian Fuchs

Kiungo wa kati wa Manchester United Nemanja Matic, 31, anatarajiwa kuondoka wakati mkataba wake utakapokwisha mwishoni mwa msimu huu, huku mawakala wakiendelea kutathimini timu, lakini AC Milan hawana mpango wa kumsajili kutokana na matakwa yake ya mshahara. (Calciomercato)

Kiungo wa kati wa Arsenal Granit Xhaka, 27, amesema anahofia hataichezea klabu hiyo tena baada ya kupoteza unahodha wake.(Evening Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Granit Xhaka

Roma na Manchester United wamebaki kwenye mazungumzo kuhusu mchezaji wa nafasi ya ulinzi Chris Smalling, 30, na mpango wa kuhamia Italia kwa mkataba wa kudumu. (Star)