Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 03.03.2020: Pogba ,Sancho, Werner, Holgate, Lozano,Sturridge

Paul Pogba

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Paul Pogba kurejea katika mazoezi ya kikosi cha kwanza Manchester United wiki hii

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, atarejea katika mazoezi ya kikosi cha kwanza Manchester United wiki hii na anapania kubuni ushirikiano uwanjani na Bruno Fernandes aliyejiunga na klabu hiyo Januari. (ESPN)

Manchester United wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Muingereza Jadon Sancho, 19, kwa bei inayotarajiwa kuvunja usajili wa katika ligi kuu ya Premia msimu wa joto. (Telegraph)

United pia inajiandaa kumenyana na Liverpool kupata saini ya Sancho kwa £100m, pamoja na mshambuliaji wa RB Leipzig wa miaka 23-Mjerumani Timo Werner. (Express)

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho hana hofu kuhusiana na hatma yake ya baadae katika klabu hiyo

Real Madrid na Paris St-Germain pia wanamnyatia Sancho, ambaye anataka kurejea England. (Mirror)

Huku hayo yajijiri, Werner amejiondoa kwenye mtandao wa Twitter wa klabu yake ya sasa Leipzig baada ya wao kutumia picha yake akijibu maswali kuhusu Liverpool kushindwa kwa mara ya kwanza katika msimu huu wa ligi ya Premia. (Echo)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner (kulia) akifungia bao klabu yake

Mkufunzi wa Leipzig Julian Nagelsmann hangelipendelea kumuachilia beki wa Manchester City Angelino,23, ambaye kwa sasa anachezea klabu kwa mkopo - lakini anasema bei ya Mhispania huyo ni "ni ghali mno" na kwamba huenda akawa vigumu kumpatia mkataba . (Kicker - in German)

Beki wa Muingereza Mason Holgate, 23, anasema lengo lake ni kujiunga na Everton licha ya klabu nyingine kama Manchester City kuonesha nia ya kutaka kumnunua. (Mail)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Leipzig hangelipendelea kumuachilia beki wa Manchester City Angelino

Wasaka vipaji wa Everton' wapo Italia "kutathmini" uwezekano wa uhamisho wa winga wa Napoli na Mexico Hirving Lozano, 24. (Area Napoli, via Star)

Leicester wanamfuatilia beki wa Burnley Muingereza Charlie Taylor, 26, anayepigiwa upatu kuchukua nafasi ya kiungo wa kimataifa wa England Ben Chilwell, 23. (Times)

Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard anaamini kipa wa klabu hiyo Mhispania Kepa Arrizabalaga, 25, bado anastahili kupewa nafasi katika klabu hiyo. (Mail)

Maelezo ya picha,

Kipa wa Chelsea Kepa Arrizabalaga

Beki wa Brazil Alex Telles, 27, amabaye ananyatiwa na Chelsea, amekataa ombio la kurefusha mkataba Porto. (A Bola, via Sun)

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta anahofia klabu hiyo isipofuzu kwa Champions League msimu huu itakuwa na wakati mgumu kuwavutia wachezaji. (ESPN)