Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 04.03.2020: Bellingham, Kane, Mourinho, Pochettino, Zidane, Sanchez, Rakitic

England's Harry Kane

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Tottenham watalazimika kufanya kila liwezekanalo wasimpoteze mshambuliaji wao Harry Kane

Tottenham watalazimika kufanya kila liwezekanalo wasimpoteze mshambuliaji wao Harry Kane, 26, msimu wa joto ikiwa watakosa kufuzu kwa Champions League msimu ujao. (Telegraph)

Mkufunzi wa Spurs Jose Mourinho amesema hana mpango wa kufanyia marekebisho kikosi chake. (Evening Standard)

Barcelona wameungana na Liverpool na Real Madrid katika kinyang'anyiro cha kumsaka winga wa miaka 20 wa Valencia Ferran Torres. (El Mundo Deportivo via Daily Mail)

Real Madrid wamemuomba meneja wa zamani wa Spurs Mauricio Pochettino kuwafahamisha kuhusu shughuli zake kwa sababu wanataka achukue nafasi ya Zinedine Zidane. (Independent)

Mshambuliaji wa Manchester United Alexis Sanchez, 31, atalazimika kukubali kupungua kwa mshahara wake ikiwa anataka kuhamia Inter Milan msimu huu wa joto. (Tuttosport via Daily Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Manchester United Alexis Sanchez

West Ham will firm up their interest in Brentford's 22-goal striker Ollie Watkins, 24, in the summer if the Bees are not promoted to the Premier League. (Sun)

Mkufunzi wa Everton Carlo Ancelotti ameshauri kikosi chake kipya cha kiufundi kujifunza Kiingereza wanapojianda kuzoea Liga Premia. (Guardian)

Mmiliki Cardiff City Vincent Tan ameripotiw akuuza nusu ya hisa zake katika klabu ya Los Angeles FC inayoshiriki ligi ya MLC - na kwamba ana mpango wa kuuza nusu ya hisa zilizobakia. (LA Times)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mkufunzi wa Everton Carlo Ancelotti

Aston Villa wanamtaka kiungo wa kati wa Marseille Morgan Sanson, 25, lakini nafasi yao ya kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa zamani wa Ufaransa wa chini ya miaka -21 itategemea kama wataponea kuondolewa katika Ligi kuu ya Premia. (Birmingham Mail)

Tetesi Bora Jumanne

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, atarejea katika mazoezi ya kikosi cha kwanza Manchester United wiki hii na anapania kubuni ushirikiano uwanjani na Bruno Fernandes aliyejiunga na klabu hiyo Januari. (ESPN)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Paul Pogba kurejea katika mazoezi ya kikosi cha kwanza Manchester United wiki hii

Manchester United wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Muingereza Jadon Sancho, 19, kwa bei inayotarajiwa kuvunja usajili wa katika ligi kuu ya Premia msimu wa joto. (Telegraph)