Eric Dier: Evra, Aguero, Cantona - wakati ambapo wachezaji walikerwa na kuamua kuwapiga mashabiki

Maelezo ya video,

Tazama Eric Dier akimvamia shabiki ambaye 'alimtusi'

Kufikia sasa , pengine umeona kanda ya video ya kiungo wa kati wa England Eric Dier akimvamia shabiki baada ya Tottenham kuondolewa katika kombe la FA nyumbani na klabu ya Norwich.

Alipanda juu ya viti ili kumkaribia shabiki huyo ambaye kocha Jose Mourinho anasema kwamba alikuwa amemtusi mchezaji huyo.

Lakini hii sio mara ya kwanza mchezaji kumvamia shabiki kama hivi...

Maelezo ya video,

Mbwana Sammatta

Granit Xhaka, Oktoba 2019

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Xhaka alijibu kwa hasira baada ya kuzomewa na mashabiki

Mwezi Oktoba 2019, nahodha wa klabu ya Arsenal wakati huo Granit Xhaka aliwashangaza wengi baada ya kuwatusi mashabiki wa klabu hiyo wakati alipokuwa akitoka uwanjani.

Hakumfuata shabiki mmoja , ama kundi la mashabiki , lakini baada ya kuzomwa wakati alipotakiwa kutoka uwanjani ili mchezaji mwengine wa klabu yake achukue nafasi yake katika mechi dhidi ya Crystal Palace iliozaa sare ya 2-2 nyumbani, alionekana akiwatukana mashabiki.

Baadaye aliomba masamaha lakini alipokonywa wadhfa wa unahodha.

Xhaka alielezea baadaye kwamba alikuwa amekasirika sana baada ya machapisho katika mitandao ya kijamii na katika mechi ya siku hizo ambayo yalimuudhi sana, matusi aliyopata anaelezea yalihusisha matamko kama vile 'tutakuvunja miguu, tutamuua mkeo na tunatamani kwamba mwanao angeshikwa na saratani'.

Neymar, Mei 2019

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Neymar alimvamia shabiki wakati alipokuwa anapoikea medali yake

Mapema mwaka ulioipita , mchezaji ghali zaidi duniani alipigwa marufuku kutocheza mechi tatu na shirikisho la soka la Ufaransa baada ya kumpiga shabiki mmoja , kufuatia timu yake kushindwa na klabu ya Rennes katika fainali ya kombe la ligi ya Ufaransa.

Wakati alipokuwa akitembea kuchukua medali yake ya nafasi ya pili , Neymar alivamiwa na shabiki.

Aliisikuma simu yake na baadaye kumwekea usoni mkono wake. ''Je nilitekeleza kitendo kibovu?'',

Neymar aliuliza katika chapisho lake katika mtandao wa Instagram. Ndio , lakini hakuna mtu anaweza kuwa tofauti na vile''

Sergio Aguero, Feb 2018

Maelezo ya video,

Aguero akikabiliana na shabiki uwanjani

Manchester City ilipata pigo iliopoteza kwa Wigan Athletic katika kombe la FA mwezi Februari 2018.

Baadhi ya mashabiki waliingia uwanjani baada ya mechi na mambo yakawa mabaya kati ya shabiki mmoja wa City na mshambuliaji Sergio Aguero.

Picha za runinga zilimuonyesha Aguero akimsukuma shabiki mmoja huku mshambuliaji huyo wa Argentina akisema baadaye kwamba alitemewa mate na kutukanwa.

Wigan walipigwa faini ya £12,500 kwa kuruhusu mashabiki kuingia uwanjani hatua iliopelekea mashabiki wengine kurarua matangazo na kuwatupia maafisa wa polisi waliokuwa uwanjani.

Aguero alikwepa adhabu kutoka kwa shirikisho la soka nchini England.

Patrice Evra, Novemba 2017

Maelezo ya video,

Tazama: Evra kicks akimpiga teke shabiki kabla ya mechi.

Kandarasi ya Patrice Evra na klabu ya Ufaransa ya Marseille ilikuwa fupi kufuatia hatua yake ya kumpiga teke kichwani shabiki mmoja.

Kabla ya mechi ya kombe la Yuropa dhidi ya Vitoria Guimares , kanda ya video ilimuonyesha Evra na wachezaji wengine wakikimbia katika tangazo moja ambapo baadhi ya mashabiki walikuwa wamekaribia uwanjani.

Evra alimpiga teke mmoja wa mashabiki katika kichwa na akaonyeshwa kadi nyekundu.

Alipigiwa marufuku na Uefa kutoka katika michezo yake kwa miezi saba na kuamua kuondoka Marseille kwa makubaliano baada ya kujiunga na klabu hiyo ,mwezi Januari 2017.

Eric Cantona, Januari 1995

Maelezo ya video,

Eric Cantona's infamous kung-fu kick

Cantona alikuwa mfano mzuri kuwahi kuonekana.

Mwezi Januari mwaka 1995, mchezaji huyo aliushangaza ulimwengu wakati aliporuka katika eneo la mashabiki na kumpiga teke shabiki mmoja wa Crystal Palace aliyekuwa amekaa katika eneo la mbele la mashabiki katika uwanja wa Selhurst Park, akimuudhi.

Cantona alikuwa amepewa kadi nyekundu muda mfupi uliokuwa umepita na alipokuwa akielekea kutoka uwanjani , alijibu matusi aliokuwa akipokea kutoka kwa shabiki wa Palace Matthew Simmons.

Alipigwa marufuku ya miezi tisa na shirikisho la soka la FA na kukiri kumpiga shabiki huyo.

Hukumu yake ya kuhudumia wiki mbili jela ilibatilishwa baada ya kukata rufaa na Cantona akajibu kwa kuviambia vyombo vya habari kwamba ''Mabata mzingi yanapofuata boti ya kuvua samaki hudhania kwamba '' dagaa watatupwa baharini''.

Maelezo ya video,

Jose Mourinho 'anaelewa kitendo cha Eric Dier' baada ya kumshambulia shabiki