Rais Magufuli aibua gumzo la ushabiki wake kati ya Simba na Yanga

Magufuli akipunga mkono

Chanzo cha picha, Ikulu

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa mara ya kwanza amehudhuria mechi ya wa miguu kati ya Simba na Yanga.

Rais Magufuli amehudhuria mapambano huo huku akiwa amevalia jezi ambayo upande ni sare ya Simba na upande ni sare ya Yanga.

Hivyo hajulikani anashabikia timu gani kati ya hizo mbili.

Chanzo cha picha, Ikulu

Baadhi ya raia wa taifa hilo wameandika katika mitandao ya kijamii kuonyesha mshangao wao.

Hata hivyo mechi hiyo pia imehudhuriwa na rais wa shirikisho la soka (caf) bwana Ahmad Ahmad kwa mara ya kwanza pamoja na baadhi ya wajumbe wa SADC.

Mechi ya ligi jijini Dar es Salaam ambayo inakutanisha miamba ya soka ya Tanzania ambao ni watani wa jadi, Simba na Yanga.

Wiki hii michuano hiyo imekuwa ikisemwa kuwa jiji linasimama kwa ajili ya hii mechi.

Chanzo cha picha, Ikulu

Uwanja wa taifa wa mpira una uwezo wa kujaza watu elfu sitini leo uaonekana umejaa.

Ingawa mechi hii inaonekana kuwa ya ufahari tu na haiamui ubingwa wa ligi kwa kuwa klabu ya Simba na Yanga zimepishana kwa alama nyingi.

Simba wana alama 68 huku Yanga wakiwa na alama 47.

Kwa miaka ya hivi karibuni viwango vya watani hao wa jadi vinaonekana kutofautiana sana tofauti na miaka ya nyuma, hivyo mechi zao zinaonekana kutotabirika.

Chanzo cha picha, IKULU

Mpaka hivi sasa, katika dakika ya 44 kipindi cha kwanza Yanga anaongoza kwa goli moja kwa mpira wa adhabu.