Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 08.03.2020: Aguero, Henderson, Ter Stegen, Skriniar, Abraham, Matic, Stones

Sergio Aguero

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Manchester City kumruhusu Sergio Aguero, 31, kuondoka waki shindwa kubatilisha marufuku ya Uefa dhidi yao

Manchester City wameridhia kumruhusu mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero, 31, kuondoka klabu hiyo msimu wa joto ikiwa watashindwa kubatilisha marufuku ya Uefa dhidi yao. (Sun on Sunday)

Chelsea wanataka kumsajili kipa wa Sheffield United Muingereza Dean Henderson, 22, kwa mkopo kutoka Manchester United, kama suluhisho la kutatua tatizo lao la kulinda lango. (Star on Sunday)

Chelsea huenda pia ikaelekeza juhudi ya kumsaka kipa Ujerumani na anayepigiwa upatu kuchukua nafasi hiyo ni kipa Marc-Andre Ter Stegen, 27, ikiwa ataamua kuondoka Barcelona msumu huu wa joto. (Sunday Express)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Chelsea inamnyatia kipa wa Barcelona Marc-Andre Ter Stegen(kulia)

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anyuko tayari kutumia £80m kumpata beki wa Inter Milan na Slovakia Milan Skriniar, 25, ili kuimarisha safu yake ya ulinzi. (Sunday Express)

Mshambuliaji wa England Tammy Abraham, 22, amekataa ofa ya hivi punde ya Chelsea hadi pale malipo yake yatakaposawazishwa na kufikia kiwango cha wachezaji wakuu wa klabu hiyo. (Sunday Mirror)

Inter Milan wanataka kumsaini beki wa Tottenham na Ubelgiji Jan Vertonghen, 32, kwa uhamisho wa bila malipo mkaba wake utakapokamilika msimu huu wa joto. (SempreInter)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Inter Milan inataka kumsaini beki wa Tottenham na Ubelgiji Jan Vertonghen

Inter pia inamfuatilia mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30. (Calciomercato)

Kiungo wa kati wa Serbia Nemanja Matic, 31, anajiandaa kusaini mkataba mpya utakaorefusha muda wake Manchester United zaidi ya msimu huu. (Manchester Evening News)

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta anatarajiwa kuongeza juhudi za kumleta Gunners beki wa Manchester City na England, John Stones, 25, t msimu huu wa joto. (Team Talk)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Inter pia inamfuatilia mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang

Nyota wa zamani wa Juventus Zinedine Zidane anadai kuwa amepoke klabu hiyo ya Turin imemuomba arejee kama mkufunzi lakini haijamhakikishia hatma yake ya baadaye kama mkufunzi wa Real Madrid. (Goal.com)

Everton pia wanapanga kusaini winga wa Newcastle Mfaransa Allan Saint-Maximin, 22 msimu huu wa joto. (Sun on Sunday)

Everton ni moja ya klabu kadhaa zinazomng'ang'ania beki wa Manchester City Muingereza Tosin Adarabioyo, 22, ambaye msimu huu yuko Blackburn kwa mkopo. (90 Min)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Everton ni moja ya klabu kadhaa zinazomng'ang'ania beki wa Manchester City Muingereza Tosin Adarabioyo

Tetesi Bora Jumamosi

Real Madrid imeanzisha tena mpango wake wa kutaka kumnunua kipa wa Man United na Uhispania David de Gea, 29. (Sun)

Arsenal huenda ikalazimika kumuuza nahodha wake na mshambuliaji matata Pierre-Emerick Aubameyang, 30, mwisho wa msimu huu kutokana na mahitaji ya mshahara wake. Mshambuliaji huyo wa Gabon ameanzisha mazungumzo kuhusu kandarasi mpya na anataka kulipwa mshahara wa £300,000- kwa wiki . (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Real Madrid imeanzisha tena mpango wake wa kutaka kumnunua kipa wa Man United na Uhispania David de Gea

Manchester City iko tayari kuanzisha mazungumzo kuhusu kandarasi mpya na kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin De Bruyne, 28, na mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 25. (Mail)

Manchester City itaimarisha ombi lake la kutaka kumnunua beki wa Inter Milan na Slovakia Milan Skriniar, 25, mwisho wa msimu huu baada ya kufeli walipowasilisha ofa ya 60m euros (£52m). (Calciomercato - in Italian)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Manchester City uanzisha mazungumzo kuhusu kandarasi mpya na kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin De Bruyne

Mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 32, amehusishwa na uhamisho wa Inter Milan na klabu nyengine , sasa anataka kusalia katika klabu ya Stamford Bridge na anasubiri mkataba. (Evening Standard)