Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 09.03.2020: Dybala, Kepa, De Bruyne, Henderson, Malen, Chong, Barisic

Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, 26,

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, 26,

Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, 26, alimwabia wakala wake kufutilia mbali uhamisho wake kuelekea Manchester United - wakati mwakilishi wa mchezaji huyo alipokuwa katika ofisi ya afisa mtendaji mkuu wa Man United Ed Woodward. (Calciomercato, via Mirror)

Real Madrid inafikiria kumsajili kipa wa Chelsea na Uhispania Kepa Arrizabalaga, 25, mwisho wa msimu huu, huku the Blues ikiwa na hamu ya kuwanunua makipa wawili kwa mkopo Marc-Andre Ter Stegen na mwenzake wa Manchester United na England Dean Henderson, 22. (Star)

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anapanga kumpatia kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 28, mkataba mpya wa mshahara wa £350,000 kwa wiki. (Express)

Maelezo ya picha,

Kevin De Bryune

Mlinda mlango wa England Dean Henderson, 22, amemwambia mwenzake wa Sheffield United atarudi kwa mkopo katika klabu hiyo msimu ujao iwapo hataanzishwa katika klabu ya Manchester United. (Mail)

Arsenal huenda ikamuwania mchezaji wake wa zamani wa timu ya vijana Donyell Malen aliyeondokja Arsenal na kujiunga na klabu ya PSV mwaka 2017. (Le10Sport)

Kiungo wa kati wa Chelsea na England Conor Gallagher, 20, aliye kwa ,mkopo katika klabu ya Swansea, ananyatiwa na klabu ya Uholanzi Vitesse Arnhem kwa usajili wa mkopo. (Sun)

Manchester United wana matumaini wanaweza kumshawishi winga wa Uholanzi Tahith Chong mwenye umri wa miaka 20 kusalia katika klabu hiyo , licha ya klabu ya Barcelona , Inter na Juventus kuonesha

nia naye. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Tahith Chong

Tottenham inafikiria kumsajili beki wa kushoto mwisho wa msimu huu na wamemlenga mchezaji anayedaiwa kuwa na thamani ya £22m Borna Barisic, 27 , raia wa Croatia ambaye kwa sasa anaichezea Rangers. (90 Min)

Kocha wa Manchester Ole Gunnar Solskjaer anasema kwamba Manchester United inahitaji wachezaji wawili ama watatu wapya ili kuonekana kama washindani wa taji la ligi ya Uingereza licha ya kuilaza Manchester City nyumbani na ugenini msimu huu kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha miaka 10 (ESPN)

Mshambuliaji wa Ufaransa na Chelsea Olivier Giroud, 33, amefichua kwamba alizuiliwa kujiunga na Tottenham katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (90 Min)

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud

Giroud amekiri alikuwa na hamu ya kujiunga na Inter wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari (Calciomercato)

Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, ambaye anaendelea kuhusishwa na uhamisho amesisitiza kuwa anafurahia kusalia Arsenal. (Mirror)

Chelsea inaongoza ushindani wa kutaka kumsajili mchezaji wa klabu ya Aldershot na England ,17, Reece Wylie. (Team Talk)

Winga wa Bournemouth na Wales Harry Wilson, 22, anayecheza kwa mkopo Liverpool , alipigwa picha akiwa amevalia koti jekundu katika mkutano huo wa klabu hizo mbili siku ya Jumamosi lakini akasisitiza kwamba alipatiwa na mfanyakazi wa Liverpool kwa sababu kulikuwa baridi.. (Liverpool Echo)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang

Liverpool huenda ikapewa fedha mwisho wa msimu huu kufuatia kifungo cha sheria cha asilimia 30 alichowekewa mchezaji wa Uhispania Luis Alberto, 27, kwenda Lazio na mkurugenzi wa michezo katika klabu hiyo Michael Edwards. (Star)