Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 22.03.2020: Alisson, Philippe Coutinho, Virgil van Dijk, Jadon Sancho, Neymar

Philippe Coutinho Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kiungo wa kati wa Barcelona na Brazil Philippe Coutinho,anataka kurejea katika ligi ya premia

Chelsea, Manchester United, Arsenal na Tottenham zinamwania kiungo wa kati wa Barcelona na Brazil Philippe Coutinho, 27, ambaye anataka kurejea katika ligi ya premia. (Mirror)

Kipa wa Brazil Alisson, 27, na beki wa Uholanzi Virgil van Dijk, 28, wanakaribia kusaini mkataba mpya na klabu ya Liverpool. (Goal)

Winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho atakuwa ''kiungo muhimu" kwa kikosi cha Chelsea, kulingana na nahodha wa zamani wa John Terry, lakini mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer pia anamsaka kiungo huyo wa kimataifa wa England aliye na miaka 19. (Evening Standard)

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer pia anamsaka winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anapania kuzishinda klabu za Barcelona na Real Madrid kumsaini kwa kima cha £74m kiungo wa kati wa Napoli na Uhispania to Fabian Ruiz, 23, msimu huu wa joto. (Express)

Manchester City haijafanikiwa kubatilisha marufuku kushiriki Champions League licha ya Uefa kulegeza mashariti ya malipo ya wachezaji msimu huu na ule ujao kutokana na janga la coronavirus. (Mail)

Manchester United huenda ikawauza wachezaji Jesse Lingard, 27, na Andreas Pereira, 24, msimu huu baada ya wawili hao kutofautiana na Ole Gunnar Solskjaer. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Manchester United huenda ikamuuza kiungo wa kati Jesse Lingard

Mkufunzi wa Everton Carlo Ancelotti anataka kumsaini mshambuliaji wa Lazio na Italy Ciro Immobile, 30. (Goal)

Wawakilishi wa mshambuliaji wa Paris-St-Germain Neymar, 28, wameifahamisha Barcelona kuwa nyota huyo wa Brazil anataka kurejea Nou Camp kutoka Ufaransa. (Star)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Manchester United wanajiandaa kutangaza ofa ya £50m kumnunua Aubameyang

Arsenal wameshauriwa kumsajili mshambuliaji wa Burnley na New Zealand Chris Wood, 28, kujaza pengo litakaloachwa wazi na Pierre-Emerick Aubameyang, 30, endapo mchezaji huyo wa kimataifa wa Gabon atamua kuondoka klabu hiyo msimu huu. (Star)

Manchester United wanajiandaa kuweka dau la £50m kumnunua Aubameyang, huku Inter Milan na Barcelona pia zikimnyatia nahodha huyo wa klabu ya Arsenal. (Metro)

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Je Paris St-Germain inaweza kumshawishi Kylian Mbappe, 21, kutia saini mkataba mpya?

Kusitishwa kwa soka ya ulaya kutokana na janga la corona kutaipatia Paris St-Germain nafasi wa kumshawishi shambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 21, kutia saini mkataba mpya japo mkataba wa sasa unaenedelea hadi 2022. (Marca)

Manchester United wamefanya mazungumzo na kiungo wa kati wa Atletico Madrid na Ufaransa Thomas Lemar, 24, ambaye aliwahi kuhusishwa na tetesi za kujiunga na Liverpool. (Manchester Evening News)

Arsenal inapania kumsajili Odsonne Edouard, 22, wa Celtic kushirikiana na Mikel Arteta, kuimarisha kikosi chake lakini mshambuliaji huyo raia wa Ufaransa pia anasakwa na Leicester na Everton . (Mirror)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii