Ronaldinho na nduguye wawekwa katika kifungo cha nyumbani nchini Paraguay

Ronaldinho alitembelewa na marafiki katika hoteli ya Asuncion ambapo sasa ataishi akisubiri kesi yake

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Ronaldinho alitembelewa na marafiki katika hoteli ya Asuncion ambapo sasa ataishi akisubiri kesi yake

Aliyekuwa mshambuliaji wa Brazil Ronaldinho aameachiliwa huru kutoka jela na kuwekwa chini ya kifungo cha nyumbani nchini Paraguay

Mshindi huyo wa taji la ballon D'or alihudumia kifungo chake jela na nduguye baada ya kukamatwa tarehe 6 Machi akituhumiwa kwa kutumia pasipoti bandia.

Wawili hao awali walikuwa wamenyimwa dhamana lakini wakatoa $800,000 kila mmoja wao na kwamba sasa wataishi katika hoteli iliopo eneo la Asuncion huku wakisubiri kesi yao.

Wote Ronaldinho na nduguye Roberto Assis walikana kufanya makosa yoyote. Ili kuwaruhusu wawili hao kuondoka jela. Jaji Gustavo Amarilla alisema kwamba kiwango cha dhamana walicholipa ni muhimu na kitahakikisha kwamba hawatatoroka.

Ronaldinho awali alikuwa amezuru Paraguay ili kukuza kitabu na kampeni ya watoto kutoka familia zisizojiweza.

Mshindi huyo wa kombe la dunia 2002 alichezea klabu za PSG, Barcelona na AC Milan kabla ya kustaafu 2015 baada ya kuichezea klabu ya Brazil Fluminense.