Tetesi za soka Ulaya Jumapili 10.05.2020: Meunier, De Gea, Martinez, Milinkovic-Savic, Magno, Saka

Thomas Meunier,
Maelezo ya picha,

Beki wa kulia wa PSG Thomas Meunier, 28.

Tottenham inaiongoza klabu ya Manchester United katika harakati za kumsaini beki wa kulia wa PSG Thomas Meunier, 28. (Sun on Sunday)

Manchester United inafikiria kutafuta kipa atakeyechukua mahali pake David De Gea japo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 na kipa wa Uhispania alitia saini kandarasi mpya ya miaka minne mnamo mwezi Septemba.. (Sunday Mirror)

Manchester United inajiandaa kutoa ofa ya kumnunua mshambuliaji wa Argentina na Inter Lautaro Martinez, lakini Barcelona na PSG pia zinamnyatia mchezaji huyo. (Sunday Express)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

mshambuliaji wa Argentina na Inter Lautaro Martinez

Man United , Chelsea na Tottenham zote zinamnyatia kiungo wa kati wa Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 25. (Caught Offside)

Real Madrid wameambia Arsenal kufanya uamuzi kufikia tarehe 15 mwezi Juni iwapo wako tayari kumuuza mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Pierre-Emerick Aubameyang, 30, ambaye amesalia na mwaka mmoja katika kandarasi yake (Sunday Mirror)

Atletico Madrid wamejiandaa kumuuza beki wa kushoto wa England Kieran Trippier kwa dau la £20m huku klabu yake ya zamani Burnley ikiwa miongoni mwa klabu zinazomnyatia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka. (Sun on Sunday)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

mshambuliaji nyota wa klabu hiyo ya Pierre-Emerick Aubameyang, 30 na kocha Mikel Arteta

Liverpool imejiandaa kuwasilisha ombi la kutaka kumsajili mshambuliaji wa Brazil mwenye umri wa miaka 17 na raia wa Brazil Talles Magno, ambaye anaichezea klabu ya Vasco da Gama kutoka Rio de.(Daily Star Sunday)

Liverpool inaweza kumnunua beki wa kushoto wa Arsenal Bukayo Saka, huku mchezaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 18 akiwa mazungumzo yake ya kutaka kumpatia kandarasi mpya yameahirishwa.(Sun on Sunday)

Kiungo wakati wa Liverpool na Uhispania Pedro Chirivella, 22, atajiunga na klabu ya Ligue 1 Nantes ya Ufaransa wakati kandarasi yake katika klabu ya Anfield itakapokamilika. (Football 365)

Maelezo ya picha,

beki wa kushoto wa Arsenal Bukayo Saka

Manchester United inatumai kumnunua beki wa Swansea Joe Rodon kwa dau la £20m baada ya mchezaji wa zamani na mkufunzi wa Wales kumpendekeza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22-year-old. (Sunday Mirror)

Kiungo wa kati wa Juventus Adrien Rabiot, 25, yuko tayari kwa uhamisho wa bila malipo kwenda Manchester United ama hata Everton baada ya raia huyo wa Ufaransa kufeli kuanzishwa mara kwa mara mjini (Corriere di Torino via Mail on Sunday)

Tottenham inaafaa kumsajili winga wa Uskochi na Bournemouth Ryan Fraser, 26, kwa uhamisho wa bila malipo msimu huu , kulingana aliyekuwa mshambuliaji wa klabu hiyo Darren Bent. (Sunday Express)

Mkufunzi wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger anasema kwamba Liverpool itatambulika kuwa mabingwa wa ligi hata iwapo msimu huu utafutiliwa mbali (TalkSport via Sunday Express)