Tetesi za soka Ulaya Jumatano tarehe 03.06.2020: Chilwell, Pogba, Almada, Sancho, Lacazette

Chelsea wamemuweka Ben Chilwell, 23, katika mpango wao wa uhamisho

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Chelsea wamemuweka Ben Chilwell, 23, katika mpango wao wa uhamisho

Chelsea wamemuweka mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Leicester Ben Chilwell, 23, katika mpango wao wa uhamisho lakini inaweza kuwagharimu mpaka kiasi cha pauni milioni 85 kumnasa mchezaji huyo. (Athletic)

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amezungumza na wakala wa kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 27, akisema kuwa bado angependelea kumsajili mchezaji huyo. (Le 10 Sport-in French)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amezungumza na wakala wa kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba

Manchester United wamebainisha kuwa winga wa Velez Sarsfield Thiago Almada,19, anawezekana akawa sehemu ya mpango wao wa uhamisho mbadala wa winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 20. (Manchester Evening News)

Inter Milan watamsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette,29, endapo mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez,22, atajiunga na Barcelona. (Mundo Deportivo)

Maelezo ya picha,

Velez Sarsfield Thiago Almada

Tottenham imempa mchezaji wa nafasi ya ulinzi Danny Rose ,29, ruhusa ya kusalia kwa mkopo Newcastle kwa kipindi kilichobaki msimu huu .(Football Insider)

Kiungo wa kati wa Newcastle Matty Longstaff, 20, ambaye analipwa pauni 850 kwa wiki , amepatiwa ofa ya pauni 30,000 kwa wiki na timu ya serie A, Udinese. (Sky Sports)

Barcelona ina mpango wa kumsaini tena beki wa kati wa Kihispania Eric Garcia,19, kutoka Manchester City. (ESPN)

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha,

Galatasaray imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kumnyakua mshambuliaji wa Charlton na Montserrat

Galatasaray imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kumnyakua mshambuliaji wa Charlton na Montserrat international, Lyle Taylor,30, ambaye amesema hataichezea klabu huyo tena wakati mkataba wake ukitarajiwa kuisha msimu huu. (Mail)

Brighton inaelekea kumkosa mshambuliaji wa Rennes M'Baye Niang, 25, baada ya Marseille kuingia kwenye mazungumzo ya kumpata mchezaji huyo raia wa Ufaransa. (Star)

Uongozi wa ligi ya primia umeviambia vilabu kuwa hakutakuwa na zaidi ya michezo minne itakayochezwa katika viwanja ambavyo sio vyao kwa maana hiyo Liverpool anaweza beba ubingwa akiwa katika uwanja wake wa Anfield.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Lionel Messi, 32, ataendelea kubaki Barcelona

Chelsea wanafikiria kubadili uamuzi wao kwa kumsaini mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner,24, ikiwa Mjerumani huyo ataonesha nia utayari wa kuhama. (ESPN)

Mshindi mara sita wa tuzo ya Ballon d'Or Lionel Messi, 32, atasalia Barcelona msimu ujao baada ya kipengele cha mkataba wake kinachomruhusu mshambuliaji huyo wa Argentina kuondoka baada ya mkataba kuisha msimu huu (Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Arsenal wako tayari kumpatia mchezaji wa nafasi ya ulinzi David Luiz,

Arsenal wako tayari kumpatia mchezaji wa nafasi ya ulinzi David Luiz, 33, mkataba wa mwaka mmoja lakini watapunguza mshahara wake wa wiki (Mirror)

Kocha wa England Gareth Southgate hatahudhuria michezo ya ligi ya primia msimu utakapoanza kwa kuwa anahisi kuwa uwepo wake kwenye viwanja hauna umuhimu. (Star)