Tetesi za soka Ulaya Jumapili 07.06.2020: Traore, Havertz, Van de Beek, Werner, Rabiot, Chilwell

Adama Traore

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Winga wa Uhispania Adama Traore

Liverpool wameulizia kuhusu winga wa Uhispania na Wolves Adama Traore, 24.

Real Madrid imewasilisha ombi la Yuro milioni 80 (£71m) kumnunua kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen Kai Havertz na itamruhusu mchezaji huyo kusalia katika klabu yake msimu ujao kabla ya kuelekea katika uwanja wa Bernabeu. (ESPN via Bild)

Manchester United imeimarisha hamu yake ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Ajax na Uholanzi Donny van de Beek, 23. (Sunday Times - subscription required)

Kiungo wa kati wa England na Aston Villa Jack Grealish, 24, amempiku mchezaji mwenza anayeichezea Borussia Dortmund winger Jadon Sancho, 20, kama mchezaji anayelengwa sana na Manchester United mwisho wa msimu huu. (Sunday Mirror)

Chelsea itasikiza ofa za wachezaji kadhaa kutokana na kuwasili kwa winga wa Morocco na Ajax Hakim Ziyech, 27, na mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner, 24, kutoka klabu ya RB Leipzig mwisho wa msimu huu . (Daily Star Sunday)

Afisa mkuu mtendaji wa klabu ya Red Bull Leipzig Oliver Mintzlaff amekana kwamba Chelsea imefanikiwa kulipa £53m kama kifungo cha sheria cha kandarasi ya Werner akisema kwamba hakuna klabu iliyofanikiwa kutumia kandarasi ya uhamisho wowote. (Sky Sports Germany via Metro)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amewataja Havertz na Werner kama wachezaji wazuri lakini akasisitiza kwamba ujio wa virusi vya corona ndio uliozuia klabu yake kuwasaini.. (Sky Sports)

Barcelona imefungua kandarasi mpya na nahodha na mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi ,32 na kipa wa Ujerumani Marc- Andre ter Stegen ,28 . (Mundo Deportivo - in Spanish)

Manchester United huenda ikampatia winga wa Wales Daniel James, 22, kandarasi mpya kabla ya kumuuza kwa mkopo msimu ujao. (Sun on Sunday)

Mchezaji anayelengwa na Manchester United na Chelsea Federico Chiesa ameambiwa anaweza kuondoka katika klabu ya Fiorentina. Mmiliki wa klabu hiyo anasema kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 raia wa Italia anaweza kuondoka. (Football Italia)

Everton inaongoza katika kutaka kumsaini mchezaji wa Juventus na Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 Adrien Rabiot, ambaye alichezeshwa kwa mara ya kwanza katika klabu ya PSG na mkufunzi wa Everton Carlo Ancelotti mwaka 2012. (Tuttosport via Mail on Sunday)

Chelsea inakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka klabu saba katika jaribio la kutaka kumsaini beki wa kushoto wa England Ben Chilwell kutoka Leicester, ambao hawako katika shinikizo ya kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Sunday Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ben Chilwell

West Ham wako kifua mbele kumsaini mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Michy Batshuayi, 26. (Sunday Express)

Arsenal na Wolvehampton wana hamu ya kumsaini beki wa Itali Daniele Ruani , 25, ambaye ameshindwa kujumuishwa katika kikosi cha kwanza katika klabu ya Juventus chini ya ukufunzi wa Maurizio Sarri.(Tuttosport via Mail on Sunday)

Wolves inajipanga kumsaini kiungo wa kati wa Paris St-Germain na Senegal, 30, Idrissa Gueye. (Sunday Express)

Mkufunzi wa Uholanzi Ronald Koeman alikataa fursa ya kuifunza Barcelona mnamo mwezi Januari ili kutekeleza ahadi yake aliotoa katika timu ya taifa ya Uholanzi . (AS)

Bournemouth itawasilisha ombi la £5m kumnunua kiungo wa kati wa Ureno Fabio Vieira, 20. (Sun on Sunday)