Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 09.06.2020: Fati, Van de Beek, Gerson, Ngakia, Mkhitaryan

Ansu Fati

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Juhudi za Manchester United kumsajili mchezaji nyota wa Barcelona Ansu Fati zagonga mwamba

Manchester United ilifeli katika jaribio la kumnunua mchezaji wa Barcelona Ansu fati, 17 kwa dau la £89m baada ya kupoteza hamu ya kumsajili mshambuliaji wa England Jadon Sancho, 20. (Sport)

Ajax imethibitisha kwamba Man United ina hamu ya kumsaini kiungo wake wa kati kutoka Uholanzi mwenye umri wa miaka 23 Donny van de Beek. (Sun)

Chelsea inashindana na Tottenham pamoja na Borussia Dortmund kumsaini kiungo wa kati wa Flamengo na Brazil Gerson, 23. (Fox Sports via Express)

Kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan anataka kuhamia Roma kwa kandarasi ya kudumu baada ya raia huyo wa Armenia ,31, kujiunga na timu hiyo ya Serie A kwa mkopo wa muda mrefu mwisho wa msimu uliopita. (Goal)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan anataka kuhamia Roma

Newcastle United inaweza kununuliwa na mfanyabishara wa Marekani iwapo kampuni mmoja ya Saudia haitakamilisha ununuzi wa klabu hiyo.. (Telegraph)

West Ham inasubiri kuona iwapo beki wa kulia wa England ambaye hana kandarasi Jeremy Ngakia, 19, atakuwa mchezaji wa kwanza wa ligi ya Premia kukataa nyongeza ya kandarasi ya muda mfupi. (Talksport)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wachezaji wa West Ham Jeremy Ngakia na Mark Noble

Manchester United inatarajiwa kukubali kandarasi mpya na beki wa kushoto Brandon Williams, 19, na kipa Dean Henderson, 23, ambaye amehudumu misimu yake miwili kwa mkopo na klabu ya Sheffiled United.(ESPN)

Kiungo wa kati wa Uhispania Dani Ceballos, 23, yuko tayari kuandikisha kandarasi ya kudumu mbali na klabu ya Real Madrid baada ya kuhudumu msimu huu akiwa katika mkopo na Arsenal. (Independent)

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Kiungo wa kati wa Uhispania Dani Ceballos

Arsenal bado wanapigiwa upatu kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania Marc Roca, 23, kutoka klabu ya Espanyol. (Express)

Awamu za muondoano wa mashindano ya klabu bingwa Ulaya zinatarajiwa kukamilishwa mjini Lisbon katika kipindi cha wiki mbili mwezi Agosti. (Independent)