Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 12.06.2020: Werner, Coutinho, Bellerin, Bellingham, Tolisso, Havertz

Philippe Coutinho

Chanzo cha picha, Getty Images

Barcelona wanamsaka beki kutoka Tottenham na Chelsea katika mkataba wa kubadilishana wachezaji utakaomjumuishwa Philippe Coutinho,27. (Sport via Mail)

Uhamisho wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ujerumani Timo Werner kwa kima cha £52m kutoka RB Leipzig kuenda Chelsea umelemazwa na masharti ya karantini ya kuzuia Covid-19 kwani kiungo huyo wa miaka 24-hawezi kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu. (The Athletic -subscription required)

Inter Milan wanapanga kuwasilisha dau la £27m kumnunua beki wa Arsenal Hector Bellerin japo Mhispania huyo amesalia na mkataba wa miaka mitatu Gunners. (Express)

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Inter Milan wanapanga kuwasilisha dau la £27m kumnunua beki wa Arsenal Hector Bellerin

Mshambuliaji wa Bayern Munich, Thomas Muller amedokeza kuwa angelipendelea kujumuika kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, 21, ambaye anapigiwa upatu kuhama Leverkusen msimu huu wa joto. (Metro)

Kinda wa Birmingham City Jude Bellingham,17 huenda akakosa kujiunga na Manchester United na badala yake akaenda Borussia Dortmund . (Sport Bild via Talksport)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Muller alipewa kadi nyekundu kutokana na tukio hili

Ajenti wa kiungo wakati wa Bayern Munich Corentin Tolisso amepinga tetesi kuwa alifanya mazungumzo na Manchester United kuhusu uhamisho wa Mfaransa huyo aliye na umri wa miaka 25. (Standard via Sky Germany)

Mazungumzo yanaendelea kati ya Juventus na Barcelona kuhusu mpango wa kubadilishana wachezaji wa safu ya kati utakaojumuisha Miralem Pjanic, 30, na Arthur Melo,23. (Independent)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Chealsea kumuuza N'Golo Kante, 29, kwa Real Madrid

Chealsea huenda ikamuuza kiungo wake wa kati N'Golo Kante, 29, kwa Real Madrid ili ipate fedha za kununua wachezaji wapya. (Express)

Tottenham wanamatumaini kwamba watafikia makubaliano ya mkataba mpya na kiungo wa kati Eric Dier,26, msimu huu, kabla mkataba wake uingie mwaka wa mwisho. (Football Insider)

Liverpool wamehusishwa na uhamisho wa kiungo wa kati wa Roma Nicolo Zaniolo, licha ya tetesi kuwa huenda wakawauza baadhi ya wachezaji wao wanaolipwa mshahara mku, klabu hiyo ya Serie A haina mpango wakumuuza kiungo huyo wa miaka 20. (Tuttosport)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kiungo wa kati wa Barcelona Arturo Vidal hana mpango wa kuondoka Nou Camp

Kiungo wa kati wa Barcelona Arturo Vidal, 33, amesisitiza kuwa kipaumbele chake kwa sasa ni soka na kwamba hana mawazo ya kutaka kuhama Nou Camp huku mkatabda wake ukiingia mka wa mwisho. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Kiungo wa kati, raia wa Ghana Thomas Partey ambaye anayenyatiwa na Arsenal anataka kusalia Atletico Madrid akiongezewa marupurupu licha ya hali ya suitafahamu kuhusu hatima yake ya baadaye. (Mundo Deportivo - in Spanish)