Tetesi za soka Ulaya Jumatano 26.08.2020: Messi, Silva, Coutinho, James, Sarr, Van De Beek

Lionel Messi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji nyota wa barcelona Lionel Messi

Paris St-Germain na Manchester United wanapigiwa upatu kumsajili Lionel Messi baada ya mshambuliaji huyo wa Argentina, 33, kuifahamisha Barcelona kwamba anataka kuondoka - wako tayari kulipa ada ya kumpata. (Sport - in Spanish)

Barua iliotumwa na klabu hiyo siku ya Jumanne inasema kwamba anataka kutumia kifungu kilichopo katika kandarasi yake ili kuweza kuondoka katika klabu hiyo akiwa mchezaji huru mara moja.

Barcelona ilifungwa magoli 8-2 na klabu ya Ujerumani ya Bayern katika robo fainali ya kombe la ligi ya mabingwa Ulaya mnamo tarehe 16 Agosti.

Barcelona hatahivyo inaamini kwamba kifungu hicho kilipitwa na wakati na kwamba kandarasi ya Messi katika klabu hiyo itakamilika 2021 huku kukiwa na kifungu cha Yuro milioni 700 kwa klabu yoyote inayotaka kumnunua.

Chanzo cha picha, Empics

Maelezo ya picha,

Mlinzi wa PSG Thiago Silva

Thiago Silva, 35, yuko tayari kufanyiwa vipimo vya matibabu na Chelsea siku ya Alhamisi, licha ya jaribio la dakika za mwisho za Paris St-Germain kutaka kumpatia mkataba mpya mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil. (Sky Sports)

Philippe Coutinho angelipendelea kurejea katika Ligi ya Premia badala ya Barcelona - huku Manchester United, Arsenal na Chelsea wakimnyatia nyota huyo wa Brazil aliye na umri wa miaka 28. (Marca)

Everton wako kwenye mazungumzo ya kumsaini kiungo wa kati wa Real Madrid James Rodriguez, 29, baada ya mkufunzi Zinedine kuonesha ishara ya kumtaka aondoke klabu hiyo. (talkSPORT)

Chelsea wanakaribia kukamilisha mchakato wa kumsajili mlinzi wa zamani wa Nice Malang Sarr, 21, kwa mkataba wa miaka mitano. (Express)

Chanzo cha picha, Getty Images

Kiungo wa kati wa Ajax Donny van de Beek yuko tayari kuhamia Ligi ya Primia msimu huu wa joto huku Manchester United wakiwa mbioni kumsaka Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 23. (Manchester Evening News)

Newcastle United wanamtaka mchezaji wa safu ya kati na nyuma wa Arsenal Rob Holding, 24, kwa mkopo na Gunners wako tayari kupokea ofa. (Mail)

AC Milan wanapania kumsajili kiungo wa kati wa Real Madrid Mhispania Brahim Diaz, 21, kwa mkopo msimu wa 2020-21. (Marca)

Crystal Palace wamekubali kulipa £14m kumnunua kiungo wa kati wa QPR Eberichi Eze, baada ya kuzidisha dau lililowasilishwa kuchelewa na West Brom kumpata mchezaji huyo aliye na umri wa miaka 22- Fulham walijiondoa. (Sun)

Maelezo ya picha,

Mchezaji wa Real Madrid Brian Diaz

Aston Villa, Leeds United na West brom pia wanamsaka Watkins. (Birmingham Live)

Everton, Leicester City, Southampton na Leeds United wamewatuma wasaka vipaji wao kufuatilia mchezo wa kiungo wa safu ya kati na nyuma wa Dundee United Lewis Neilson, 17. (Dundee Courier)