Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 17.09.2020:Reguilon, Tomori, Sigurdsson, Gimenez, Partey, Garcia

Chanzo cha picha, Getty Images
Mlinzi wa kushoto wa Real Madrid na Uhispania Sergio Reguilon ,23, yupo katika kiwanja cha mazoezi cha Tottenham kwa vipimo vya afya kabla ya kujiunga na klabu hiyo ya ligi kuu.(Evening Standard)
Kocha wa Everton Carlo Ancelotti anataka kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Chelsea Fikayo Tomori, 22, lakini pia yuko tayari kuwaachia wachezaji kadhaa akiwemo viungo wa kati Gylfi Sigurdsson, 31, na Fabian Delph , 30 .(Times, subscription required)
Manchester City wanajiandaa kuwa uhamisho wa mchezaji wa nafasi ya ulinzi anayekipiga Atletico Madrid, Jose Gimenez, ikiwa Napoli itakataa kushusha dau kwa ajili ya mlinzi wa kati Kalidou Koulibaly,29. (Guardian)
Kiungo mkabaji wa Atletico Madrid Thomas Partey,27, ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na Arsenal lakini klabu hiyo ya Uhispania watamuuza tu iwapo dau la pauni milioni 45 litafikiwa.(Football.London)

Chanzo cha picha, EPA
Manchester United inaangalia uwezekano wa kumsajili winga wa kulia wa Ivory Coast Amad Traore,18, kutoka Atalanta. (Manchester Evening News)
Leicester City wako karibuni kumsajili winga wa Roma Cengiz Under.(Telegraph, subscription required)
Kocha wa Barcelona Ronald Koeaman amesema kuwa timu hiyo haitamrejesha mlinzi wa Manchester City, Mhispania Eric Garcia,19. (Manchester Evening News)
Arsenal inamfuatilia mlinda mlango wa Dijon Runar Alex Runarsson, 25, huku washika bunduki hao wakiwa na matumaini makubaliano ya dau la pauni milioni 1.5 litafikiwa. (Evening Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Lyon Jean-Michel Aulas amekana ripoti kuwa mchezaji wa nafasi ya kiungo wa kati,Memphis Depay, aliyekuwa akichezea Manchester United, yuko njiani kujiunga na Barcelona. (Evening Standard)
Sheffield United imemfuatilia mshambuliji wa Arsenal Folarin Balogun, 19, Kocha Chris Wilder amethibitisha.(Yorkshire Post)
RB Leipzig imetishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Leeds United kutokana na kushindwa kumsajili mshambuliaji , Mfaransa Jean-Kevin Augustin. Leipzig imedai kuwa Leeds kwa mujibu wa mkataba ilikuwa inatakiwa kumsajili Augustin, ambaye alikuwa akicheza kwa mkopo katika klabu ya Elland Road msimu uliopita, kwa kitita cha pauni milioni 17.7 baada ya kwenda ligi ya Primia. (Independent)

Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja wa timu ya Uingereza Gareth Southgate ameruhusiwa kurejea viwanjani kuendelea kuangalia wachezaji wa ligi kuu baada ya kukaa nyumbani kwa muda mrefu kushughulikia mipango ya timu hiyo.(Mail)
Klabu ya Birmingham City iko kwenye mazungumzo na Ipswich Town kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji Kayden Jackson. ofa ya Bournemouth ilikataliwa ilipomtaka mchezaji huyo, 26. (East Anglian Daily Times)
Newcastle wamemjumuisha kiungo mshambuliaji raia wa Ufaransa Florent Indalecio katika majaribio. Mchezaji huyo mwenye miaka 23 aliyekua akikipiga na Saint-Etienne kwa sasa hana klabu. (Newcastle Chronicle)