Wafahamu wachezaji wa soka wanaolipwa mapato ya juu zaidi 2020

kandanda

Chanzo cha picha, AFP

Linapokuja suala la kupima wachezaji wazuri katika mchezo unaoshabikiwa sana, macho yote huangazia wachezaji wawili walio na upinzani mkali na umaarufu wakidaiwa kuweza kujipatia kipato cha $1 bilioni wakisakata soka. Inaweza kuwa wakati wa kutoa nafasi kwa mchezaji wa tatu.

Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ndio wachezaji wanaorodheshwa katika nafasi za juu mwaka huu kwa malipo na jarida la Forbes kwa mara nyengine, baada ya Messi kusuluhisha tatizo la kandarasi yake na kuwa mchezaji wa kwanza anayelipwa zaidi duniani akijipatia pato la $ 126m, akimshinda Ronaldo ambaye ni wa pili kwa pato la $ 117m.

Lakini wapenzi wa mpira wa miguu wana kitu kipya cha kujivunia kupitia mchezaji Kylian Mbappe, mshambuliaji wa Paris Saint-Germain ambaye anatua katika nafasi ya nne na dola milioni 48. Akiwa katika umri wa miaka 19 pekee ndiye mchezaji chipukizi wa timu ya PSG na Ufaransa baada ya kufunga magoli 103 katika mashindano yote tangu alipoanza kucheza soka ya kulipwa miaka mitano iliopita.

Akiwa na umri wa miaka 19 , alikuwa mchezaji mchanga zaidi kufunga goli katika kombe la dunia {tangu Pele alipofunga mwaka 1958 akiwa na umri wa miaka 17}, alipokuwa akiisaidia timu ya ufaransa kushinda taji lake la pili katika historia . Yuko mbele ya Messi na Ronaldo walipokuwa na umri wake.

Mchezaji huyo ambaye ameongoza kwa magoli misimu miwili mfululizo katika ligue 1 tayari amefunga magoli 12 zaidi ya Messi alipokuwa na umri wa miaka 21 na magoli 76 zaidi ya Ronaldo alipokuwa katika umri wake.

Mchezaji huyo anayetoka katika makaazi ya watu masikini alikuwa mchezaji ghali zaidi wakati PSG ilipotoa $215m kwa klabu yake ya zamani Monaco kugharamia haki zake 2017 na kumpatia kandarasi ambayo inamlipa $28m msimu huu.

Kampuni za Nike na ile ya simu ya Hublot zote zinamtumia sana kuuza bidhaa zao.

Hatahivyo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anaongozwa na mchezaji mwenza Neymar katika orodha hiyo mwaka huu akiwa nambari tatu kwa pato la $96m, lakini hali hiyo huenda ikabadilika kwa kuwa Mbappe anatarajiwa kuandikisha kandarasi mpya 2022 wakati kandarasi yake itakapokamilika.

Katika orodha yote ya wachezaji 10 bora duniani, wanatarajiwa kujipatia mshahara wa jumla ya $570m na marupurupu msimu huu iwapo hakutakuwa na mlipuko mwengine.

1. Lionel Messi-Barcelona

Jumla ya mapato : $126 million

Msharaha: $92 million

Ufadhili: $34 million

Ilichukua klabu ya Barcelona miaka 105 kushinda mataji 64 kabla ya Messi kujiunga na klabu hiyo 2005.

Katika kipindi cha miaka 16 aliiongoza timu hiyo kushinda mataji 35 , idadi ambayo imemfanya jina lake kuorodheshwa miongoni mwa magwiji wa mchezo huo na kumpatia mapato ya $1b kabla ya kulipa kodi.

Mwaka huu aliuweka ulimwengu wa soka katika hali ya ati ati baada ya kuzozana na klabu hiyo kuhusu mwaka wake wa mwisho wa kandarasi yake. Alisalia na anatarajiwa kujipatia $92m kwa kufanya hivyo, lakini 2021 kila mtu anatazama ni wapi Messi ataelekea.

2. Cristiano Ronaldo-Juventus

Chanzo cha picha, Reuters

Jumla ya mapato: $117 million

Mshahara: $70m

Ufadhili: $47 million

Ronaldo ndio mchezaji maarufu duniani akiwa na wafuasi milioni 457 katika mitandao ya kijamii. Mwezi Julai alichapisha kanda ya video ya yeye binafsi akizungumzia kuhusu barua aliomuandikia miaka 10 gwiji wa soka wa Brazil Julia Rosado.

Ni mchezaji wa pili katika historia baada ya mchezaji wa Iran Ali Daei kufunga zaidi ya magoli 100 katika mechi za kimataifa

3. Neymar Jr.-Paris Saint-Germain

Chanzo cha picha, Getty Images

Jumla ya Mapato: $96 million

Mshahara: $78million

Ufadhili: $18 million

Mshambuliaji huyo wa Braziil mwenye umri wa miaka 28 mmojawapo wa wachezaji hatari zaidi katika soka aliongeza mshahara wake mara tatu zaidi alipoamua kuwacha kucheza na Messi na badala yake kujiunga na PSG ili kucheza na Kylian Mbappe 2017.

Mbali na uhamisho uliovunja rekodi wa $263m na mshahara wa $70m, PSG inalazimika kugharamika $600m ili kuweza kumzuia katika mji huo mkuu wa Ufaransa

4. Kylian Mbappe-Paris Saint-Germain

Chanzo cha picha, Getty Images

Jumla ya mapato: $42 million

Mshahara: $28m

Ufadhili: $14 million

Kwa mwaka wa pili mfululizo, Mbappe alitajwa kushinda taji la ligue 1 la mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi.

Klabu yake pia ilishinda ubingwa wa ligi hiyo. Alilazimika kuhudumia kipindi cha ufunguzi wa ligi hiyo katika karantini baada ya kuambukizwa virusi vya corona.

5. Mohamed Salah-Liverpool

Chanzo cha picha, EPA

Jumla ya mapato: $37 million

Mshahara: $24m |

Ufadhili: $13 million

Salah amefikisha magoli 20 katika mashindano yote katika kila kipindi cha misimu yake mitatu aliyochezea Liverpool akiisaidia klabu hiyo kujishindia taji lake la kwanza la Premia katika kipindi cha miaka 30 mwaka 2019-20.

6. Paul Pogba-Manchester United

Chanzo cha picha, EPA

Jumla ya mapato: $34 million

Mshahara: $28m

Ufadhili: $6 million

Kandarasi ya Pogba inakamilika msimu ujao , ijapokuwa Man United ina mbadala wa kuiongeza mwaka mmoja zaidi.

Mchezaji huyo wa Ufaransa aliwatishia mashabiki mapema mwezi Agosti kwa kuchapisha katika mtandao wa kijamii kwamba alikuwa ameweka kandarasi na klabu ya Verdansk .

Lakini baadaye ilibainika kuwa habari bandia. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 pia amewahi kufanya tangazo na Messi pamoja na Salah katika kukuza kinywaji cha Pepsi

7. Antoine Griezmann-Barcelona

Chanzo cha picha, Getty Images

Jumla ya mapato: $33 million

Mshahara: $28

Ufadhili: $5 million

Tangu mchezaji huyo wa Ufaransa kutoridhisha wasajili wake Barcelona msimu uliopita , kuna uvumi kwamba klabu hiyo inataka kumuuza PSG ili kumrudisha Neymar kupitia mahitaji ya Messi.

8. Gareth Bale-Tottenham

Jumla ya mapato: $29 million

Mshahara: $23m

Ufadhili: $6 million

Bale aliondoka Real Madrid baada ya mgogoro wa muda mrefu na mkufunzi wa klabu hiyo Zinedine Zidane, mchezaji huyo sasa amerudi katika timu yake ya zamani ya Tottenham Hotspurs

9. Robert Lewandowski-Bayern Munich

Jumla ya mapato: $28m

Mshahara: $24m

Ufadhili:$4m

Kutokana na mlipuko wa virusi vya corona, waandaaji wa tuzo ya Ballon D'or waliamua kufutilia mbali tuzo ya mwaka 2020 kwa mchezaji bora zaidi duniani.

Kwa kufanya hivyo tuzo hiyo inamnyima Lewandowski ambaye alikuwa na nafasi nzuri kushinda katika mashindano yote mshambuliaji huyo wa Poland alichangia magoli 65 akiichezea Bayern Munich msimu uliopita , magoli 55 na kutoa usaidizi wa pasi 10 katika mechi 47.

Katika ligi ya mabingwa Ulaya alifunga katika kila mechi hadi fainali dhidi ya PSG.

10. David De Gea-Manchester United

Chanzo cha picha, Getty Images

Jumla ya mapato: $27m

Mshahara: $24m

Ufadhili: $3m

Mshahara wa De Gea wa $24m unamfanya kuwa kipa anayelipwa mshahara mkubwa zaidi duniani .

Mwezi Julai alicheza kwa mara ya 400 kama mlinda lango .