Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 09.10.2020: Bale, Ozil, De Bruyne, Upamecano, Sarri, Cuisance

Gareth Bale

Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 31, anataka kushinda taji la Uingereza msimu huu akiichezea Tottenham, kulingana na ajenti wake. (Sky Sports)

Arsenal inataka kuanzisha mazungumzo na Mesut Ozil kuhusu kufutilia mbali kandarasi yake kabla ya dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Mail)

Manchester City imepiga hatua katika mazungumzo ya kandarasi na kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bryune .Wanataka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kutia saini kandarasi nyengine ya miaka 4. (Times)

Manchester United itajaribu kumsaini beki wa RB Leipzig na Ufaransa Dayot Upamecano, 21, kwa dau la £36.5m msimu ujao. Liverpool na Manchester City zina hamu ya kumsajili. (Bild, via Sun)

Chanzo cha picha, BBC/Twitter

Aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester United Memphis Depay, 26 anasema kwamba baadhi ya sheria zilimzuia kujiunga na Barcelona katika dirisha la uhamisho. (AS)

Aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea na Juventus Maurizio Sarri ni mgombea wa wadhfa wa meneja wa klabu ya Fiorentina. (Tuttomercato - in Italian)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Michael Cuisance, 21, amefutilia mbali madai kwamba kufeli kwa vipimo vya matibabu ndio sababu iliosababisha kufeli kwa uhamisho wakekujiunga na leeds . Baadaye alijiunga na Marseille , kwa mkopo kutoka Bayern Munich. (Sky Sports)

Liverpool itafanya mazungumzo na winga Harry Wilson kuhusu uwezekano wa uhamisho wa mkopo katika klabu nyengine muda tu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 atarudi baada ya mechi ya kimataifa akiichezea. (Standard)

Bournemouth haitamruhusu kiungo wa kati David Brooks kuondoka kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho. Sheffield United inamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 . (Football Insider)

West Ham inafikiria usajili wa £5m wa kiungo wa kati wa QPR na Ireland Ryan Manning. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 pia anaweza kucheza kama beki wa kushoto. (Star)

The Hammers pia wanataka kumsaini mshambuliaji wa Bournemouth na Norway Josh King, 28, lakini wanaamini The Cherries inafaa kupunguza dau wanaloitisha la £17.. (Guardian)

Beki wa England Ashley Young, 35, anasema kwamba ataondoka Inter Miland na kuondoka Itali hivi sasa iwapo atarahusiwa kuichezea tena Watford.. (Golden Tales podcast)

Arsenal imeanza kuonesha moja kwa moja mechi zake kwa mashabiki wake katika ujwanja wa Emirates. Wataruhusu mashabiki 368 kuingia uwanjani ambao watalazimika kulipa £49 kila. (Telegraph)

TETESI ZA SOKA ULAYA Alhamisi

Maelezo ya picha,

Sijawahi kuwa na hamu ya kujiunga na man United

Mshambuliaji wa Barcelona Ousmane Dembele 23 hakuwa na hamu ya kujiunga na Manchester United kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho na sasa anataka kujiunga na Juventus msimu ujao.(Catalunya Radio, via Mirror)

Manchester United haitawasilisha ombi la kumsajili mchezaji wa Senegal na Watfotd Ismaila Sarr, 22, kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho la ligi ya EFL tarehe 16. (Goal)

Mkufunzi wa Tottenham Jose Mourinho anatarajiwa kumwacha nje beki wa kushoto wa England Danny Rose, 30, katika kikosi chake cha wachezaji 25 ambacho kinatarajiwa kukamilika kufikia tarehe 20 Oktoba. (Mail)

Mchezaji wa Westaham na Brazil Felipe Anderson anasema anaafikia ndoto yake ya kushiriki katika mechi za ligi ya klabu bingwa Ulaya baada ya kuhamia katika klabu ya Porto kwa mkopo katika kipindi cha msimu kilichosalia , lakini anaamini kwamba bado ataendelea kuichezea West (Talksport)

West Ham ina hamu ya kuongezea beki wa kati kutoka ligi ya daraja la kwanza nchini England huku pia wakitafuta kiungo wa kati atakayeziba pengo lililowachwa na Anderson . (London Evening Standard)

Kipa wa Manchester United na Argentina Sergio Romero, 33, anajiandaa kuhamia katika ligi ya Marekani ya MLS baada ya kukosa kujiunga na klabu ya Everton katika siku ya mwisho ya dirisha la. (Mail)

Chanzo cha picha, Reuters

Mkufunzi mpya wa Nottingham Forest Chris Hughton anafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Fulham na Ufaransa Anthony Knockaert, 28, on loan. (Sky Sports)

West Brom wana imani ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Huddersfield na Karlan Grant, 23, kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho katika ligi ya EFL Ijumaa ijayo. (Mail)

Mkufunzi wa Ujerumani Joachim Low anadai kwamba beki wa Chelsea na Ujerumani Antonio Rudiger "alijaribu kufanya kila kitu kuondoka Chelsea kabla ya siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho na anaamini kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 atawasilisha ombi la kutaka kuondoka katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari.. (Sun)

Bayern Munich, ambao walishindwa kuafikiana kuhusu mkataba wa kumsajili kwa mkopo winga wa England Callum Hudson Odoi 19 waliambiwa na Chelsea kwamba watapewa adhabu iwapo mchezaji huyo hatashirikishwa katika mechi nyingi katika ligi ya Bundesliga mbali na kifungu cha sheria cha Bayern kumnunua kwa zaidi ya £70m iwapo atacheza idadi fulani ya mechi. (Sport Bild)

Chanzo cha picha, Getty Images

Kiungo wa kati wa Aston Villa Jack Grealish, 25, amefichua kampeni yake ya wiki tatu ya kumshawishi kiungo wa kati wa England Ross Barkley kujiunga na klabu hiyo kutoka Chelsea. (London Evening Standard)

Grealish alikuwa mmoja wa wachezaji wanne waliokuwa wakilengwa na mkufunzi wa Man United Solskjaer ambaye alishindwa kuwasaini kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa. (ESPN)

Mshambuliaji mpya wa Manchester United na Uruguay Edinson Cavani, 33, amefichua kwamba anataka kuichezea klabu ya Boca Juniors baada ya kuondoka katika uwanja wa Old Trafford.. (Goal)

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United imejiondoa katika kumsaini mshambuliaji wa England Jadon Sancho 20, baada ya kubaini kwamba uhamisho huo huenda ukaigharimu timu hiyo £227m kutokana na dau la £108m linalotakiwa na Borussia Dortmund , pamoja na mahitaji ya marupurupu ya mshahara kutoka kwa ajenti wake (Guardian)

West Ham walikuwa wako tayari kumsaini beki wa England Fikayo Tomori, 22, kwa mkopo ambao walikuwa wamejitolea kuilipa Chelsea dau la £50,000 kila mara alipokosa kuwachezea The Hammers , lakini makubaliano hayo hayakuafikiwa. (Talksport)

Tottenham na West Ham wana hamu ya beki wa kati wa Wales Joe Rodon, 22, na huenda wakawasilisha ombi la dau la £18m kabla ya siku ya mwisho ya ligi ya EFL mnamo tarehe 16. (Wales Online)

Chanzo cha picha, Getty Images

West Ham huenda ikawasilisha ombi la kumsajili beki wa Watford na England Craig Dawson, 30, lakini watahitajika kulipa £4m. (Sun)

Ombi la Manchester United la kumsajili winga wa Senegal Ismaila Sarr kwa kipindi kilichosalia cha msimu huu lilikataliwa na Watford , lakini inaweza kujaribu tena mwezi huu licha ya kwamba The hornets wanataka mkataba wa kudumu. (Manchester Evening News)

Kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum amepuuzilia mbali hamu kutoka kwa klabu ya Barcelona . Kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 inakamilika msimu ujao katika uwanja wa Anfield. (Mirror)

Klabu ya Ufaransa ya Saint-Etienne imeikosoa Arsenal kwa kushindwa kumruhusu beki kinda wa Ufaransa William Saliba kurudi katika klabu hiyo. (Talksport)

Chanzo cha picha, Getty Images

Barcelona itasubiri hadi mwisho wa msimu wa 2021 ili kumsajili beki wa Uhispania Eric Garcia, 19, kutoka Manchester City. Barca ilitoa Yuro milioni 2 katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho. (Marca)

Jaribio la Barcelona kumsaini mshambuliaji wa Lyon na Uholanzi Memphis Depay, 26, lilikatizwa baada ya winga wa Ufaransa Ousmane Dembele, 23, kukataa kuondoka Manchester United. (AS)

Watford na Middlesbrough inamtaka beki wa kushoto wa Chelsea na Ghana baba Rahman , 26, kwa mkopo wa muda mrefu . (Goal)

TETESI ZA SOKA JUMANNE

Chanzo cha picha, Getty Images

Maafisa wakuu wa klabu ya Manchester United wamewasiliana na aliyekuwa kocha wa Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino iwapo watamfuta meneja Ole Gunnar Solskjaer. (Star)

Manchester City imekataa ofa ya dau la £15.4m na marupurupu kutoka kwa klabu ya Barcelona kumnunua beki wa Uhispania Eric Garcia, 19, katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho.. (Sky Sports)

Liverpool ilipokea maombi ya winga wa Switzerland Xherdan Shaqiri, 28, wakati wa dirisha la uhamisho na wanataraji atasalia katika klabu hiyo hadi mwezi Januari kwasasabu hawako tayari kumuuza kwa mkopo (Goal)

Chanzo cha picha, Getty Images

Beki wa Manchester City na England John Stones, 26, alikataa mbadala wa kuondoka kwa mkopo kuelekea Totenham kwasababu hakutaka kuiondoa familia yake. (Star)

Klabu ya Porto ina hamu ya kumnunua mchezaji wa West Ham na Brazil Felipe Anderson, 27, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. (Sky Sports)

West Ham iko katika mazungumzo ya kumsajili beki wa England mwenye umri wa miaka 30 Craig Dawson kutoka Watford. (Football Insider)

Barcelona imepoteza zaidi ya £181m kama mapato kutokana na mlipuko wa virusi vya corona. (Telegraph)

Chanzo cha picha, BBC/twitter

Mkufunzi wa Paris St-Germain Thomas Tuchel hafurahii hatua ya klabu hiyo kushindwa kununua wachezaji katika dirisha la uhamisho. (Guardian)

TETESI ZA SOKA JUMATATU

Chanzo cha picha, Getty Images

Kiungo wa kati wa Arsenal Matteo Guendouzi, 21, anatarajiwa kuelekea katika timu ya ligi ya Bundesliga Hertha Berlin, baada ya kuwachwa nje ya kikosi cha timu hiyo katika uwanja wa Emirates. (Mirror)

Tottenham inatarajiwa kufanya jaribio la mwisho kumsaini beki wa InterMilan mwenye umri wa miaka 25 Slovakia defender Milan Skriniar. (Mirror)

Juventus inaandaa dau la kumnunua beki wa kushoto wa Chelsea Emmerson Palmieri wakiwa na lengo la kumsaini mchezaji huyo wa Itali mwenye umri wa miaka 26 kwa. (Calciomercato - in Italian)

Arsenal imefutulia mbali mpango wao wa kutaka kumsaini kiungo wa kati wa Ghana na Atletico Madrid Thomas Partey ,27. The Gunners haiko tayari kuafikia kifungu cha kumnunua mchezaji huyo cha £45m. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Sheffield United inajiandaa kuipiku West Brom kumsajili mchezaji wa klabu ya Metz na Senegal mwenye umri wa miaka 25 Habib. (Le 10 Sport - in French)

Beki wa kati wa Ufaransa Jean-Clair Todibo, 20, huenda anaondoka Barcelona kwa mkopo, akitarajiwa kuelekea Fulham ambako anaelekea huku Everton pia nayo ikiwa ina hamu ya. (Le 10 Sport - in French)

Bayern Munich itamlenga winga wa Juventus na Brazil Douglas Costa, 30, iwapo watashindwa kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na England Callum Hudson-Odoi, 19. (Kicker - in German)

Celtic ina hamu ya kumsaini kiungo wa kati wa West Ham Robert Snodgrass ,33 kwa mkopo lakini pia wako tayari kwa makubaliano ya kudumu.. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Uhamisho wa beki wa Ujerumani Antonio Rudiger kuelekea AC Milan unaelekea kutimia , huku Chelsea ikifurahia kumwachilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kabla ya mjadiliano ya kumuongozea kandarsi , huku akiwa amesalia na miaka miwili katika kandarasi yake. (90min)

Anderlecht inakaribia kumsajili kiungo wa kati wa West Ham na raia wa Ireland Josh Cullen, 24. (Het Laatste Nieuws - in Dutch)

Brighton inaandaa dau la 11.5m euro (£10.4m) kumnunua kiungo wa kati wa Poland Jakub Moder, 21, kabla ya kumuuza kwa mkopo kwa Lech Poznan kwa msimu huu. (Super Express - in Polish)

Kiungo wa kati wa klabu ya Valencia na jamhuri ya Afrika ya kati Geoffrey Kondogbia, 27, ananyatiwa na klabu isiojulikana kwa dau la 22m.(Marca - in Spanish)

Maelezo ya picha,

Geoffrey Kondogbia,

Winga wa Roma na Uholanzi Justin Kluivert, 21, anaelekea RB Leipzig kwa mkopo wa muda mrefu (Fabrizio Romano via Football Italia)

Klabu ya Paris St-Germain imewasilisha ombi la kumnunua kwa mkopo beki wa Porto na Portugal Danilo Pereira, 29. (Goal)

Kiungo mshambuliaji wa Werder Bremen Davy Klaassen, 27, anatarajiwa kurudi katika klabu yake ya utotoni Ajax, baada ya dau la £10m kuafikiwa ili kumsajili mchezaji huyo wa Uholanzi. (De Telegraaf - in Dutch)

Mshambuliaji wa Cameroon Eric Maxim Choupo-Moting, 31, atasaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Bayern Munich, baada ya kuondoka Paris St-Germain. (Kicker via Goal)