Tetesi za soka Ulaya Alhamisi tarehe 21.01.22: Transfer rumours: Odegaard, Smith Rowe, Lingard, Garcia, Lampard, Rose

Martin Odegaard, amewsiliana na Arsenal

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Martin Odegaard, amewsiliana na Arsenal

Arsenal wamewasiliana na kiungo wa kati wa Real Madrid na Norway Martin Odegaard, 22. (Sky Sports)

Hatahivyo, Odegaard anasemakana kuwa anakaribia kujhamia Sevilla kwa mkataba wa deni. (Cuatro - in Spanish)

Maelezo ya picha,

Arsenal wanatarajia kutoa ofa ya maelfu ya pauni kwa Smith

Arsenal wanatarajia kutoa ofa ya mkataba wa malipo ya pauni 40,000 kwa wiki kwa kiungo wa kati Muingereza Emile Smith Rowe, 20. (Mail)

Paris St-Germain wanapanga uhamisho wa ghafla kwa ajili ya kiungo wa kati-nyuma wa Manchester City na Uhispania Eric Garcia, 20. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Timu za England zataka kumtoa Jesse Lingard (kushoto) Manchester United

Tottenham, West Ham na Sheffield United ni miongoni mwa klabu kadhaa ambazo zinataka kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Manchester United na England Jesse Lingard, mwenye umri wa miaka 28 kwa mkopo . (Talksport)

Kiungo wa safi ya nyuma-kushoto wa Tottenham na England Danny Rose anawindwa na timu ya Uturuki ya Trabzonspor. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30- hatakuwa na mkataba na timu yoyote kwa mwishoni mwa msimu huu. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Franc Lampard hatakiwi na Chelsea

Chelsea wangependelea zaidi kumbadilisha kocha wao anayekabiliwa na ukosoaji mkubwa Frank Lampard na kumuajiri meneja wa mpito katikati ya msimu . (Independent)

Lakini Lampard atafutwa kazi kama matokeo ya Chelsea hayataboreka haraka. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Divock Origi ni miongoni mwa wachezaji wanaosakwa na Klabu ya Ujerumani

Mchezaji w Leicester City Kelechi Iheanacho, 24, Divock Origi, 25 , wa Liverpool , na mshambuliaji wa Nice Kasper Dolberg, 23, wako katika orodha ya washambuliaji wanaosakwa na timu ya Ujerumani ya RB Leipzig. (Bild - via Leicester Mercury)

West Ham anajiandaa kutoa ofa mpya ya thamani ya takriban pauni milioni 32 kwa ajili ya mshambuliaji wa timu ya Morocco Sevilla Youssef En-Nesyri, 23. (Star)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Fikayo Tomori amekamilisha mazungumzo na timu ya Italia

AC Milan wanakamilisha mkataba wao wa mkopo kwa ajili ya kiungo wa kati-nyuma wa Chelsea mwenye umri wa miaka 23 Fikayo Tomori. (Gazzetta dello Sport)

Fulham watasikiliza maelezo ya kuhama ya mchezaji wa safu ya kati wa Norway Stefan Johansen, 30, mlinzi wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 31- Maxime Le Marchand na kiungo wa kati wa Ivory Coast Jean Michael Seri, 29. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wolves wanakaribia kufikia makubaliano ya mkopo na Willian

Wolves wanakaribia kufikia makubaliano ya mkopo kwa ajili ya mshambuliaji Mbrazili kutoka klabu ya Real Sociedad Willian Jose, 29, huku wakiwa na chaguo la kununua. (Telegraph)

Mchezaji anayelengwa na Arsenal Emiliano Buendia amekubali kuwa Norwich haitakubali kumuachilia aondoke kwa chini ya malipo ya pauni milioni 40 . Kiungo huyo wa kati wa Srgentina mwenye umri wa miaka 24- ana matumainiya kuweza kuhama msimu huu. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Manchester united wanamsaka Gabriel Veron

Manchester United wanamtaka mshambuliaji wa klabu ya Palmeira Mbrazili Gabriel Veron, 18. (Sport - via Star)

Wolves wanamuwinda winga wa Bolton mwenye umri wa miaka 17 Finlay Lockett. (Football Insider)