Tetetesi za soka Ulaya Jumanne 09.02.2021: Messi, Lukaku, Ings, Konate, Shoretire, Alaba, Elliott

Manchester City bado wanataka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester City bado wanataka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, 33, msimu huu wa joto lakini wanajiandaa wakisubiri mpaka mwezi Machi au Aprili.(ESPN)

Mshambuliaji wa Inter Milan, Mbelgiji Romelu Lukaku, 27, na Muingereza anayekipiga Southampton Danny Ings,28, ni miongoni mwa wachezaji wanaotazamwa na Manchester City wakati huu ambapo klabu hiyo ikimtafuta mshambuliaji mpya. (Athletic - subscription required)

City itakabiliwa na ushindani wa Paris St-Germain katika kumnasa mshambuliaji Lukaku.(Calciomercato - in Italian)

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United imeweka wazi kuwa inamlenga Ibrahima Konate wa RB Leipzig, mwenye miaka 21 kuwa beki wao wa kati muhimu. Watapata upinzani kutoka kwa Liverpool na Chelsea.(Independent)

Winga wa Nigeria Shola Shoretire,17, amesaini mkataba wa kwanza na Manchester United, ingawa pia PSG, Barcelona, Juventus na Bayern Munich walikuwa na nia ya kumnyakua. (Mail)

Chelsea itamchukua David Alaba ambaye mkataba wake ndani ya Bayern Munich unamalizika katika msimu wa joto - ikiwa tu beki wa kushoto wa Austria, 28, atapunguza kiwango cha mshahara anachotaka, kiasi cha pauni 400,000 kwa wiki. (Telegraph - usajili unahitajika)

Chanzo cha picha, Getty Images

Inter Miami inayomilikiwa na David Beckham inafikiria kumnasa mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa West Brom Kieran Gibbs,31, kwa uhamisho wa bure msimu huu. (Athletic, via Mail)

Inter Miami wanaendelea na mazungumzo na mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Stoke City Ryan Shawcross,33. (Mail)

Liverpool itafahamu siku ya Jumanne kuwa ni kiasi gani cha fidia watakayoilipa Fulham kwa ajili ya Harvey Elliott, 17, huku kilabu cha zamani cha kiungo huyo wa Kiingereza kikitaka karibu pauni milioni 8. (Sky Sports)

Kazi nzuri aliyoionesha beki wa kati wa Denmark Adreas Christensen,24, pengine ndicho kilichomshawishi kocha wa Chelsea Thomas Tuchel kutohitaji kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi katika dirisha la usajili la msimu ujao wa joto. (Football London)

Chanzo cha picha, EPA

Kocha wa West Ham David Moyes anasema alikataa kutumia pauni milioni 15-20 kwa mshambuliaji mpya katika dirisha la uhamisho la Januari. Mshambuliaji pekee anayetambuliwa , Muingereza Michail Antonio,30, anapambana na uchovu.(Goal)

Arsenal inataka kumsajili kinda, beki wa kushoto kumsaiia Kieran Tierney,23. (Athletic)

Mchezaji wa zamani wa nafasi ya ulinzi wa Arsenal Nacho Monreal, 34, yuko kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba ndani ya klablu ya Real Sociedad, mkataba wake ukitarajiwa kumalizika mwezi Juni.Marca - in Spanish)

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amekataa kuthibitisha ikiwa ataendelea kubaki Bernabeu, baada ya mkataba wake kuisha mwaka 2022. (Mirror)