Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 21.02,2020: PSG yamtaka Kane

Chanzo cha picha, Getty Images
Je kuna uwezekano wa Mauricio Pochettino kuungana tena na mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, Paris St-Germain?
Mauricio Pochettino anataka kuungana tena na mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 27, Paris St-Germain endapo Kylian Mbappe au mchezaji nyota wa Brazil Neymar, 29, wataondoka klabu hiyo ya Ufaransa. (Sunday Mirror)
Meneja wa Leicester City Brendan Rodgers anaongoza katika orodha ya wakufunzi watakaochukua nafasi ya Jose Mourinho kama meneja mpya wa Tottenham. (Football Insider)
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 20, ataitisha mkataba wa miaka mitano wa thamani ya £78m kuhamia klabu yoyote msimu huu. (Sunday Mirror)
Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland
Barcelona wamekusanya orodha itakayowasaidia kumsaka mshambuliaji mpya, akiwemo Haaland na mshambuliaji wa Manchester City Muargentina Sergio Aguero, 32. (Mundo Deportivo)
Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta ameashiria kuwa klabu hiyo itajaribu kusalia na kiungo wa kati wa Norway Martin Odegaard baada ya mkataba wake wa mkopo kutoka Real Madrid, ambao unakamilika mwisho wa msimu huu. (Times - subscription required)
Leicester wanatathmini uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa England na mfungaji mabao hodari Ivan Toney Brentford 24. (Sunday Mirror)
Chanzo cha picha, Getty Images
Sergio Aguero alijiunga na Manchester City mwaka 2011
Arsenal inamnyatia kiungo wa kati wa Bruges na raia wa Ivory Coast Odilon Kossounou, 20, na huenda ikamsajili msimu huu wa joto. (Sunday Mirror)
Wolves apia wanapania kumsajili Kossounou ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £20m-rated. (Sun)
Manchester United wanamnyatia kiungo wa kati wa Aston Villa Jack Grealish, 25, na huenda wakamsajili dirisha la uhamisho litakapofunguliwa msimu wa joto baada ya juhuzi za kumnunua nyota huyo wa kimataifa wa Englanda kugonga mwamba mwaka jana . (Todofichajes, via Daily Star on Sunday)
Chanzo cha picha, BBC Sport
Kiungo wa kati wa Aston Villa Jack Grealish
Tottenham wanatarajiwa kukabiliwa na ushindani mkali katika juhudi zao za kumsajili kiungo wa kati wa RB Leipzig na Austria Marcel Sabitzer, 26, msimu huu. (Team Talk)
Mchezaji wa Brighton wa safu ya kati na nyuma wa Muingereza Ben White, 23, ananyatiwa na Liverpool na huenda akatua klabu hiyo msimu huu. (Football Insider)
Manchester United haijawasiliana na ajenti wa mlinzi wa Real Madrid na Uhispania Sergio Ramos, 34, ambaye yuko tayari kujiungu na klabu yoyote msimu huu. (Fabrizio Romano, via Caught Offside)
Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United haijawasiliana na ajenti wa mlinzi wa Real Madrid na Uhispania Sergio Ramos
Manchester United wanamfuatilia mlinzi wa Everton Muingereza Jarrad Branthwaite, 18, ambaye kwa sasa yuko Blackburn kwa mkopo. (Mail on Sunday)

Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 20.02.2021: Mourinho, Aguero, Messi, Cavani, Pulisic, Giroud, Sancho, Konsa, Henry
Spurs itasubiri kwanza kabla ya kufanya maamuzi dhidi ya Mourinho, Aguero na Messi bado hawajaamua hatma yao, Man Utd iko tayari kufanya mazungumzo na Cavani na mengine mengi.