Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 27.02.2021: Torres, Calhanoglu, Kane, Lacazette, Bellerin, Rodrygo, Alaba, Haaland

Gharama ya Jules Kounde (kulia) imeishinda Manchester United

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Gharama ya Jules Kounde (kulia) imeishinda Manchester United

Manchester United inaweza kuelekeza nia yake kwa kiungo wa kati wa klabu ya Uhispania Villarreal Paul Torres, mwenye umri wa miaka 24, kutokana na kwamba gharama yake ni nafuu kuliko mlinzi Mfaransa wa klabu ya Sevilla, Jules Kounde mwenye umri wa miaka 22. (Eurosport)

Meneja wa RB Leipzig Julian Nagelsmann atataka kuhamia Tottenham, kama klabu hiyo ya Primia Ligi itaamua kumtafuta meneja mwingbine badala ya Jose Mourinho. (Bild, via Express)

Maelezo ya picha,

Hakan Calhanoglu

Manchester United watatumia michezo yao 16 ya Ligi ya Uropa AC Milan kumfuatilia kiungo wa kati wa Uturuki Hakan Calhanoglu, 27, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu. (Express)

Mkurugenzi mkuu wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke anasema kuwa kabu hiyo ya Bundesliga italazimika 'kumuacilia mchezaji' kwasababu za kifedha zilizosababishwa na janga la Corona. (Handelsblatt, via Manchester Evening News)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa England Harry Kane, 27

Mshambuliaji wa England Harry Kane, 27, yuko tayari kubakia katika Tottenham kwa walau mwaka mwingine mmoja zaidi. (Telegraph)

Mgombea wa urasi wa klabu ya Barcelona Toni Freixa anadai kuwa anamakubaliano ya kusaini mkataba na wachezaji wawili wa ngazi ya juu wanaotaka kushinda taji la Ballon d'Or iwapo watachaguliwa. (El Larguero, via Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Alexandre Lacazette, 29, ameonekana kuwa analengwa na klabu ya Ligue 1

Mshambuliaji wa Arsenal Mfaransa Alexandre Lacazette, 29, ameonekana kuwa analengwa na klabu ya Ligue 1 upande wa Monaco katika msimu ujao. (Mirror)

Meneja wa Chelsea Thomas Tuchel amepewa ruksa na klabu kusaini mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland kutoka Borussia Dortmund, anayesakwa sana na klabu mbali mbali . Klabu hiyo ya Bundesliga, hatahivyo, inawasiwasi na kijana huyo mwenye umri wa miaka 20 iwapo atataka kujiunga na upande wa Primia Ligi. (Bild, via Sun)

Maelezo ya picha,

Hector Bellerin

Mlinzi wa timu ya Uhispania Hector Bellerin, 25, anaweza kuondoka Arsenal msimu huu kama sehemu ya makubaliano na meneja Mikel Arteta. (ESPN)

Mlinzi wa Austria David Alaba, 28, ambaye ameiambia Bayern Munich kuwa ataondoka mwishoni mwa msimu huu, ameazimia kujiunga na klabu ambayo itamuwezesha kucheza katika safu ya kati kuliko safu ya ulinzi. Amekuwa akihusishwa na klabu ya Real Madrid, huku Chelsea, Liverpool na Manchester United pia wakimtaka. (Le Parisien, via Star)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mbrazili Rodrygo anawindwa na Liverpool

Liverpool wanafuatilia hali ya mshambuliaji wa Real Madrid Mbrazili Rodrygo, 20, ambaye anaweza kuruhusiwa kuondoka upande wa La Liga kwa pauni milioni 50. (Diario Gol, via Team Talk)

Hatahivyo, Haaland huenda akaamua kuwa nchini Ujerumani kwa msimu mwingine zaidi. (TalkSport)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mbrazili Willian anasema alitaka katika klabu ya Chelsea

Winga wa Arsenal Mbrazili Willian, 32, anasema alitaka kubaki katika klabu ya Chelsea lakini the Blues walikuwa wanampatia mkataba wa miaka miwili tu, badala ya miaka mitatu. (UOL Esporte, via Mail)

Kiungo wa kati wa timu ya Toronto FC Jahkeele Marshall-Rutty mwenye umri wa miaka 16 amezivutia timu kubwa za Ulaya, huku Manchester City, Chelsea, Manchester United, Bayern Munich na Juventus zikisema zinamuhitaji Mcanada huyo. (Tuttosport - in Italian)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kiungo wa kati wa Manchester City Mjerumani Ilkay Gundogan

Kiungo wa kati wa Manchester City Mjerumani Ilkay Gundogan, 30, anasema Manchester United ilianza mazungumzo ya kusaini mkataba nae kuanzia Borussia Dortmund miaka miwili au mitatu kabla ya kuhamia katika City. (Sky Sports, via Mirror)

Bayern Munich ni klabu ya hivi karibuni iliyotangaza kujitenga na uhamisho wa mchezaji wa Norwich City, Max Aarons, huku matumaini ya Everton ya kusaini mkataba na mlinzi huyo wa England mwenye umri wa miaka 21-yakiongezeka kutokana na hilo. Bei ya pauni milioni 35 ambayo Norwich inaitaka kwa Aarons iliripotiwa awali Manchester United nje ya dau. (Bild, via Sport Witness)

Maelezo ya picha,

Mchezaji wa kimataifa wa Marekani Weston McKennie

Kiungo wa kati wa Shalke, ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Marekani Weston McKennie ni mchezaji anayepewa kipaumbele kununuliwa na Juventus licha ya kwamba kijana huyo mwenye umri wa miaka 22-bado anakipengele cha mkataba wake cha mkopo kinachoilazimu klabu ya Tulin kumnunua . (Calciomercato - in Italian)

Everton wanaangalia uwezekano wa kumchukua Aarons kwa mkataba wa kudumu kama mchezaji mbadala wa stalwart na mchezaji wa kimataifa wa Jamuhuri ya Ireland Seamus Coleman mwenye umri wa miaka 33 . (Liverpool Echo)