Tetesi za soka Ulaya Ijumaa tarehe 05.03.2021: Konate, Lacazette, Elmohamady, Fernandes, Koulibaly, Pereira, Jakobs

Chanzo cha picha, Getty Images
Mchezaji wa safu ya ulinzi wa timu ya RB Leipzig Mfaransa Ibrahima Konate
Arsenal ni miongoni mwa klabu kadhaa zinazoangalia uwezekano wa kumhamisha mchezaji wa safu ya ulinzi wa timu ya RB Leipzig Mfaransa Ibrahima Konate mweye umri wa miaka 21. (Standard).
Konate ni mmoja kati ya wachezaji sita ambao Gunners wanashugulika kuwapata, huku klabu hiyo pia ikiwa tayari kumuuza mshambuliaji wa Ufarnsa Alexandre Lacazette, 29, kwa bei inayofaa. (Football.London)
Kiungo wa kati wa Manchester United Mreno Bruno Fernandes
Kiungo wa kati wa Manchester United Mreno Bruno Fernandes, 26,yuko tayari kusaini mkataba mpya ambao utaongeza mshahara wake mara dufu na kuweza kupata malipo ya takriban pauni 200,000 kwa wiki. (Sun)
Mlinzi wa Misri Ahmed Elmohamady, 33, ataondoka Aston Villa kwa mkataba usio na malipo msimu huu huku klabu hiyo ikiwa haina mipango ya kumpatia mkataba mpya. (Football Insider)
Chanzo cha picha, Getty Images
Kalidou Koulibaly
Napoli wamepunguza kiwango cha pesa walizokuwa wanadai kwa ajili ya kumuuza Kalidou Koulibaly hadi kufikia kiwango cha euro milioni 45 (£38.7m), huku Bayern Munich wakiaminiwa kuwa mbele ya Liverpool na Manchester United katika mbio za kusaini mkataba na mlinzi huyo kutoka Senegal mwenye umri wa miaka 21. (Il Mattino - in Italian)
Leicester City wamefufua haja yao kwa mchezaji ambaye wamekuwa wakimtaka kwa muda mrefu Ismail Jakobs, mwenye umri wa miaka 21, lakini the Foxes wanakabiliwa na ushindani kutoka Brighton ambao pia wanamfuatilia kwa karibu mchezaji huyo wa kimataifa kutoka klabu ya Ujerumani ya Cologne. (Mail)
Kiungo wa kati Andreas Pereira
Manchester United wanatafuta klabu mbadala kwa ajili ya kiungo wa kati Andreas Pereira, 25, msimu huu kwasababu Lazio wanatarajiwa kukubali hilo na kubadilisha makataba wa Mbrazili huo kutoka mkataba wa mkopo na kusaini mkataba wa kudumu nae. (Corriere Dello Sport - in Italian)
Shinikizo la kifedha linaweza kuilazimisha klabu ya Valencia kumuuza mshambuliaji wa Ureno Goncalo Guedes, 24, ambaye analengwa na West Ham katika msimu ujao (O Jogo, via Sun)
Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa safu ya kati wa Chelsea Jorginho
Juventus wamemtaja kiungo wa safu ya kati wa Chelsea Jorginho, 29, kama chaguo lao la pili iwapo watashindwa kusaini mkataba na Muitalia Manuel Locatelli, 23, kutoka klabu ya Sassuolo. (Calciomercato - in Italian)
Wakati huo huo, Mlinzi Juventus anayeskwa na timu mbali mbali Radu Dragusin mwenye umri wa miaka 19- raia wa Romania ambaye awali alihusishwa na taarifa za kuhamia Crystal Palace, yuko tayari kusaini mkataba mpya na klabu ya Turin. (Goal)
Chanzo cha picha, Getty Images
Winga wa Real Madrid na Uhispania Lucas Vazquez
Leeds United wanakabiliwa na ushindani kutoka AC Milan katika kujaribu kusaini mkataba na winga wa Real Madrid na Uhispania Lucas Vazquez, 29, ambaye mlkataba wake katika klabu ya Bernabeu unamalizika msimu ujao.(Fichajes, via Sport Witness)
Eintracht Frankfurt wamesema kuwa hawatamzuia mkurugenzi wao wa mchezo Fredi Bobic, 49,kama atachagua kuondoka, huku Manchester United, West Ham na Hertha Berlin wakihusishwa na taaruifa za kumnunua Mjerumani huyo. (Bild, via Team Talk)
Chelsea itatia kibindoni asilimia isiyojulikana ya ada itakayopokewa na Brighton wakimuuza Lamptey baada klabu hizo mbili kukubaliana katika mpango ambao ulimwezesha mlinzi huyo kuondoka Stamford Bridge na kutua Seagulls Januari 2020. (Express)
Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Manchester City na Argentina Sergio Aguero
Mgombea uraisi wa Barcelona Joan Laporta anataka mshambuliaji wa Manchester City na Argentina Sergio Aguero, 32, kujiunga na klabu hiyo msimu huu. (Mail)
Mkufunzi wa Gunners Mikel Arteta amesema "umakini kabisa" kuongoza Arsenal licha ya madai yanayomhusisha Barcelona - lakini mazungumzo ya mkataba mpya utakaomwezesha kusalia Emirates hayajaanza. (ESPN)
Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette
Arteta anasema mazungumzo kuhusu kandarasi ya mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette,29, ambaye mkataba wake wa sasa na Arsenal unaendelea hadi 2023, yataanza hivi "karibuni". (Mail)
Winga wa zamani wa England Ashley Young, 35, anamatumaini ya kunyakua taji la Serie, Inter Milan kabla ya kurejea klabu katika yake ya kwanza ya Watford kwa mkataba wa bila malipo msimu huu. (Mirror)
Meneja wa Liverpool Meneja Jurgen Klopp
Meneja Jurgen Klopp amekiri kuwa Liverpool itakuwa na wakati mgumu kuwavutia wachezaji endapo haitafuzu kujiunga na Ligi ya Mabingwa. (Goal)
Mkurugenzi wa AC Milan Frederic Massara amefichua kuwa klabu hiyo bado haijaamua ikiwa itaanzisha mazungumzo ya kumnunua Fikayo Tomori,23, - lakini AC Milan inasisitiza bei ya £26m iliyotolewa na Chelsea iko juu sana. (Express)
Mkufunzi wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer
Mkufunzi wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ameonya juu ya kiwango cha pesa ambacho kitatumiwa na klabu hiyo msimu huu wa joto wakati Old inapojiandaa kutangaza matokeo yao ya kifedha ya hivi karibuni . (Times - subscription required)