Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 18.03.2021: Shaw, Neto, Rudigerm Vazquez, Alaba, Koulibaly

Luke Shaw

Chanzo cha picha, BBC Sport

Maelezo ya picha,

Luke Shaw (kulia) katika mechi iliyopita kati ya Manchester United na Liverpool

Manchester United wanajiandaa kuanza mazungumzo ya mkataba wa Luke Shaw, wakati kiungo huyo Muingereza mwenye umri wa miaka 25-akijivunia utendakazi wake katika klabu hiyo. (Mirror)

Unite pia inamnyatia winga wa Wolves Pedro Neto, 21, na huenda ikamnunua kwa zaidi ya £50m msimu huu wa joto . (Sun)

Kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, amefikia makubaliano ya awali ya kujiunga na Barcelona kwa uhamisho wa bure wakati mkataba wake utakapokamilika Liverpool msimu huu wa joto. (Times - subscription required)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Georginio Wijnaldum amefikia makubaliano ya awali ya kujiunga na Barcelona

Kipa wa Everton na England Jordan Pickford, 27, huenda asicheza tena msimu huu baada ya kujeruhiwa, hali ambayo inatilia shaka kushiriki kwake katika michuano ya Ulaya . (Sun)

Leicester na Leeds wanataka kumsaini kiungo wa kati wa Uturuki Orkun Kokcu baada ya Feyenoord kupunguza bei ya mchezaji huyo aliye na umri wa miaka 20-hadi £10m. (La Razon via Sun)

Mlinzi wa Chelsea, Antonio Rudiger, 28, ameifahamisha kabla hiyo kwamba hana nia kuanza mazungumzo kuhusu mkataba mpya hadi baada ya ushiriki wa Ujerumani katika Euro 2020. (Athletic via Mail)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mlinzi wa Chelsea, Antonio Rudiger

Tottenham na Arsenal wameulizwa ikiwa wana mpango wa kumsaini winga wa Real Madrid Mhispania Lucas Vazquez, 29. (Mirror)

Mlinzi wa Bayern Munich, David Alaba,28, anajiandaa kujiunga na Real Madrid baada ya mabingwa hao wa Uhispania kumpatia ofa ya mshahara wa £165,000-kwa wiki na parupurupu mengine ya £17m . (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ole Gunnar Solskjaer anafanya kila juhudi kusalia na mshambuliaji wa Uruguay, Edinson Cavani

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anafanya kila juhudi kusalia na mshambuliaji wa Uruguay, Edinson Cavani, 34, katika uwanja wa Old Trafford msimu ujao licha ya tetesi kwamba nyota huyo huenda akajiunga na Boca Juniors ya Argentina. (Mirror)

Napoli huenda wakamuuza Kalidou Koulibaly, 29, kwa kima cha chini ya £69m walichokuwa wamemuekea kiungo huyo wa kimataifa wa Senegal awali, katika juhudi za kupunguza matumizi.Koulibaly amehusishwa na tetesi za kujiunga na Liverpool na Manchester United. (Gazzetta dello Sport, via Express)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mchezaji wa kimataifa wa Senegal, Kalidou Koulibaly

Borussia Dortmund wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Ujerumani Julian Brandt, 24, ambaye aliwahi kuhusishw ana uhamisho wa kwenda Arsenal, kwa £21.5m msimu huu wa joto . (Bild, via Team Talk)

Barcelona wanataka kummuuza kiungo wa kati wa Brazil, Philippe Coutinho,28, msimu huu na pia wanatafakari uwezekano wa kupokea ofa ya mkopo kumuachilia nyota huyo. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Barcelona wanataka kummuuza kiungo wa kati wa Brazil, Philippe Coutinho,28, msimu huu

AC Milan wamewasiliana na Benfica kuhusu uwezekano wa kumnunua kwa kima cha £43m mshambuliaji wa Uruguay, Darwin Nunez, 21. (Calcio Mercato - in Italian)

Mshambuliaji wa Brazil Neymar, 29, anakaribia kusaini mkataba mpya Paris St-Germain, unaotarajia kuendelea hadi mwaka 2026. (Mercato, via Mail)