Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 20..03.2021: Haaland, Moriba, Mbappe, Aguero, Pogba

Erling Braut Halaand
Maelezo ya picha,

Erling Braut Halaand

Real Madrid na Barcelona zote ziko tayari kupambana na Manchester City, Manchester United na Chelsea kwa saini ya mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 20. (AS - kwa Kihispania)

Haaland anataka kuondoka Dortmund msimu huu wa joto na ana hamu ya kuhamia Real Madrid.

Manchester United inavutiwa na kiungo wa Barcelona mzaliwa wa Guinea wa kikosi cha uhispania cha timu ya wcahezaji walio chini ya umri wa miaka 17 Ilaix Moriba, 18.

Maelezo ya picha,

Ilaix Moriba

Paris St-Germain wako tayari kumpa mshambuliaji Mfaransa Kylian Mbappe, 22, kandarasi mpya ya euro 30m (Pauni 25.8m) ili kuzizuia Real Madrid na Liverpool kumsajili . (L'Equipe via Mirror)Mshambuliaji wa Manchester City na Argentina Sergio Aguero, 32, na kiungo wa kati wa Liverpool Mholanzi Georginio Wijnaldum, 30, wako kwenye orodha fupi ya Barcelona ya wachezaji wanaolengwa kusajiliwa katika uhamisho wa majira ya kiangazi. (AS kupitia Sport Witness)

Juventus wanaendelea kufuatilia hali ya kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, huku mkataba wa Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 28 ukikamilika mnamo Juni 2022. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)

Mashetani Wekundu bado hawajatoa ofa ya mkataba rasmi kwa Pogba licha ya kufanya mazungumzo juu ya hatma yake huko Old Trafford. Itaigharimu Tottenham £ 25m ikiwa watamtimua meneja Jose Mourinho.(Mirror)Mourinho atafutwa kazi na Spurs ikiwa watashindwa kufuzu kwa mashindano ya ubingwa wa Ulaya msimu huu, na bosi wa RB Leipzig, Julian Nagelsmann na kocha wa Leicester Brendan Rodgers wakitajwakama wawaniaji walio katikamstari wa mbele kuichukua nafasi yake .

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

MKufunzi wa RB Leipzig Julian Nagelsmann

Tottenham hawako tayari kulipa kifungu cha ununuzi cha Carlos Vinicius cha pauni milioni 36 lakini watatoa pauni milioni 17 ili kufanya uhamisho wake wa mkopo wa kutoka Benfica kuwa wa kudumu. (Mail)

Mlinzi wa Ivory Coast Eric Bailly, 26, atakataa kandarasi mpya huko Manchester United baada ya kuachwa nje ya kikosi kilishosajili ushindi dhidi ya AC milan katika mchuano wa kombe la Europa League siku ya alhamisi (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Mlinda lango wa Sweden Robin Olsen, 31, huenda hataongeza muda wake wa mkopo na Everton mwishoni mwa msimu huu baada ya yeye na familia yake kutishwa kwa panga katika uvamizi ulifanywa nyumbani kwao mapema mwezi huu (Mail)Barcelona itampa mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 33, kandarasi ya maisha msimu huu wa joto kwa nia ya kumuweka klabuni humo lakini imtake akubali kupunguzwa mshahara.(Mundo Deportivo - kwa Kihispania )West Ham bado hawajazungumza juu ya uhamisho wa kudumu wa kiungo wa kati wa Manchester United na England Jesse Lingard, 28, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo huko Hammers.(Football London)

Chanzo cha picha, Getty Images

Napoli inavutiwa na beki wa kushoto wa Liverpool Mgiriki Kostas Tsimikas, 24, ambaye amecheza mara sita tu tangu ajiunge nao msimu uliopita wa joto. (Corriere dello Sport via Sport Witness)Liverpool na Tottenham zote zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Marekani Matthew Hoppe, 20, kutoka Schalke. (Transfermarkt - in German)

Bosi wa Brighton Graham Potter anasema ataketi mwishoni mwa msimu na Danny Welbeck, 30, kuzungumzia juu ya mkataba wa mshambuliaji huyo wa zamani wa England. (Brighton and Hove Independent)Bosi wa zamani wa Juventus Massimiliano Allegri anazingatiwa na Napoli kama anayeweza kuiziba nafasi ya Gennaro Gattuso (Calciomercato - in Italian)