Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 24.03.2021: Kane, Rodriguez, Kounde, Torres, Lloris, Maignan, Koulibaly

Harry Kane

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Harry Kane

Real Madrid wanapania kumnunua mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 27. (SER Deportivos - in Spanish)

Arsenal wanatathmini uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati na mlinzi wa Real Betis na Argentina Guido Rodriguez. (Mundo Deportivo via Metro)

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United wanawasaka wachezaji Jules Kounde, 22, wa Sevilla na Pau Torres, 24, wa Villarreal, baada ya kuamua walinzi hao wawili wa La Liga wawe katika orodha yao ya wachezaji wa safu ya kati na nyuma msimu huu wa joto. (90 min)

Manchester City wanajadiliana na Fluminense kuhusu mkataba wa mshambuliaji Mbrazil Kayky, 17 wa thamani ya hadi euro milioni 21.5. (Sun)

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Hugo Lloris na Son Heung-min

United huenda pia wakamnunua kipa wa Tottenham Hugo Lloris, 34, kuchukua nafasi ya David de Gea, huku Spurs wakimnyatia kipa wa Lille na Ufaransa aliye na umri wa miaka 25- Mike Maignan. (L'Equipe via Mail)

Liverpool, Juventus na Roma wanafuatilia hali ya Nacho, Real Madrid, wakati mlinzi huyo wa Uhispania, 31, anapojiandaa kuingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake msimu huu wa joto. (AS - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kalidou Koulibaly anawindwa na Everton

Mkufunzi wa Everton Carlo Ancelotti anataka kumsajili mlinzi wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 29, ambaye alikuwa chini yake alipokuwa akiongoza klabu hiyo ya Italia. (Talksport)

Cristiano Ronaldo, 36, huenda akaondoka Juventus ikiwa Real Madrid itaamua kumrudisha mshambuliaji huyo wa Portugal katika klabu hiyo. (Marca)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Denis Zakaria mchezaji wa Borussia Monchengladbach

Raia wa Switzerland Denis Zakaria, 24, anaendelea kuvutia Manchester City, ambayo inamfuatilia kiungo wa kati wa Borussia Monchengladbach kwa mtazamao wa kutafuta mbadala wa Fernandinho msimu huu. (Sky Sports via Manchester Evening News)

Bayern Munich inafanya mazungumzo na aliyekuwa beki wa kulia wa Real Madrid Lucas Vazquez, 29, ambaye atakuwa hana mkataba kufikia mwisho wa Juni. (AS)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Sergio Ramos

Aliyekuwa mlinzi wa Real Madrid Fernando Hierro ana imani kuwa beki wa kati wa Uhispania Sergio Ramos, 34, atafikia makubaliano ya mkataba mpya na kustaafu akiwa katika klabu hiyo. (Marca)

AC Milan inafuatilia kwa karibu mlinzi wa England, 24, Fikayo Tomori ambaye yuko kwa mkopo kutoka Chelsea kuwa wa kudumu. (Goal)

Burnley na Newcastle inamfutilia beki wa kati wa West Bromwich Albion Kyle Bartley, 29, ambaye amesalia na mwaka mmoja katika mkataba wake na Hawthorns. (Telegraph)