Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 25.03.2021:Suarez, Torres, Costa, Kane, Ronaldo, Johnstone

Luis Suarez

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Luis Suarez

Liverpool wana nia ya kusaini tena mkataba na mshambuliaji wa Atletico Madrid raia wa Uruguay Luis Suarez, mwenye umri wa miaka 34. (Fichajes via Four Four Two)

Mshambuliaji wa safu ya kati wa Atletico Madrid Mhispania Diego Costa, 32, ataichezea Benfica msimu ujao baada ya kuafikia makubaliano na klabu hiyo ya Ureno (Mundo Deportivo - in Spanish)

Rais wa zamani wa Real Madrid Ramon Calderon ana wasi wasi kwamba klabu hiyo ina pesa za kusaini mkataba na mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 27, msimu huu. (Talksport)

Chanzo cha picha, Getty Images

Real wanataka kumrejesha mshambuliaji Mhispania Brahim Diaz, 21, kikosini kufuatia kukamilika kwa mkataba wake wa mkopo katika AC Milan. (Calciomercato - in Italian)

Hatahivyo, hawana nia ya kurejea kwa mshambuliaji wa Juventus Mreno Cristiano Ronaldo, 36. (COPE - in Spanish)

Mchezaji wa safu ya ulinzi wa Villarreal Mhispania Paul Torres mwenye umri wa miaka 24, atataka kuhamia katika klabu ya Manchester United msimu huu . (Manchester Evening News)

Mlinzi wa zamani wa Tottenham Alan Hutton ameitaka klabu hiyo kusaini mkataba na mlindalango wa England Sam Johnstone kutoka West Brom ili azibe pengo la Hugo Lloris. (Football Insider)

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Ian Wright anasema Arsenal inapaswa kusaini mkataba wa kudumu na kiungo wa kati raia wa Norway Martin Odegaard, 22, kutoka Real Madrid msimu huu. (Ringer FC's Wrighty's House podcast via Metro)

Sunderland wameanza mazungumzo na Wolves kwa ajili ya kusiani mkataba wana mlinzi Muingereza Dion Sanderson, 21, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkataba wa deni kwa pauni milioni 2. (Daily Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Antoine Griezmann

Mchezaji wa safu ya mashambulizi ya kati Mfaransa Antoine Griezmann, 30, anataka kubaki na kuthibitisha kiwango cha mchezo wake katika Barcelona. (Radio Catalunya via AS)

Barcelona inataka kuwauza Griezmann na kiungo wa kati Mbrazili Philippe Coutinho, 28. (El Confidencial - in Spanish)

Winga wa Chelsea Christian Pulisic, 22, anasema anataka kuiwakilisha Marekani katika michezo ya msimu huu ya Olympiki iliyopangwa upya mjini Tokyo. (NBC Sports via Evening Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Christian Pulisic

Mshambuliaji wa zamani wa Uholanzi Marco van Basten, 56, anasema sheria ya kuotea ( offside) inapaswa kuondolewa . (Sky Sports)

Uefa inajiandaa kuondoa sheria za Kifedha za Fair Play ili kuruhusu udhibiti mzuri zaidi wa fedha zao (La Gazzetta dello Sport via Mail)