Tetesi za soka Ulaya Jumapili 28.03.2021:Bale, Werner, Haaland, Odegaard, Cavani, Almiron, Sarr

Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale hayuko kwenye mipango ya Real Madrid msimu ujao

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale hayuko kwenye mipango ya Real Madrid msimu ujao, ingawa mchezaji huyo, mwenye miaka 31 amesema anapanga kurejea katika klabu ya Uhispania mwishoni mwa msimu wake wa mkataba na Tottenham.(Marca)

Bale atakuwa mmoja wa wachezaji sita Real Madrid inawaruhusu kuondoka ili kupata fedha kwa ajili ya uhamisho wa mshambuliaji wa Kifaransa anayekipiga Paris St-Germain Kylian Mbappe, 22 na mshambuliaji Erling Braut Haaland wa Borussia Dortmund. (Sunday Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel amemtaka mmilikia wa Chelsea Roman Abramovich kumtumia mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner, 25, kama sehemu ya makubaliano ya kubadilishana ili kujaribu kumchukua Haaland kutoka Borussia Dortmund. (Sunday Express)

Nahodha wa England Harry Kane amesema hatafanya uamuzi wowote kuhusu mustakabali wake ndani ya Tottenham mpaka baada ya michuano ya Euro. Mshambuliaji huyo, 27 amekuwa akihusishwa na taarifa za kuhamia Real Madrid na Manchester City. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images

Mazungumzo kuhusu mkataba mpya kati ya Manchester City na winga wa England Raheem Sterling yamesimama mpaka msimu wa joto, huku ikielezwa kitendo cha kubadilishwa kwa wakala wa mchezaji huyo,26 kuwa sehemu ya sababu.(Star on Sunday)

City ilianza mazungumzo na Sterling kuhusu mkataba kwa malipo ya pauni 320,000 kwa wiki na pia wanazungumza na kiungo wa kati Mbelgiji Kevin de Bruyne, 29, na mshambuliaji wa Brazil Fernandinho,35, kuhusu mkataba mpya. (Sunday Sun)

Manchester United inaweza kumuwania winga wa Watford, Msenegali Ismaila Sarr,23, badala ya mshambuliaji Jadon Sancho wa Borussia Dortmund ikiwa watafanikiwa kumsajili Erling Braut Haaland. (Sunday Express)

Sarr ''alikaribia mno'' kujiunga na Manchester United majira ya joto mwaka jana, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa zamani wa ufundi wa Watford Filippo Giraldi. (Goal)

Inter Milan itasikiliza ofa kwa ajili ya mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku,27,kama wako tayari kumsajili mshambuliaji wa Manchester City, Muajentina Sergio Aguero, 32. (Star on Sunday)

Manchester City itawapasa kulipa pauni milioni 103 ikiwa wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Atletico Madrid Marcos Llorente,26. (Marca, via Metro)

Real Madrid itamuuza au kumtoa kwa mkopo kiungo wa kati wa Norway Martin Odegaard, anayecheza kwa mkopo katika klabu ya Arsenal, ikiwa Zinedine Zidane atasalia kuwa kocha wa Real Madrid. ( Football Insider)