Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 03.04.2021: Haaland, Salah, Aguero, Mbappe, Odegaard, Kane

Mchezaji wa kimataifa wa Misri Mohamed Salah

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mchezaji wa kimataifa wa Misri Mohamed Salah

Liverpool inakabiliwa na hali ya suitafahamu kumhusu mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, huku baadhi ya wadau wa klabu hiyo wakizidi kushawishika kwamba nyota huyo aliye na umri wa miaka 28-anatazamia hatma yake ya siku zijazo mahali pengine. (ESPN)

Manchester United na Chelsea zinamsaka winga wa Real Madrid Mhispania Lucas Vazquez, 29. (ABC)

Chelsea wanataka kumnunua mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero, 32, atakapoondoka Manchester City msimu huu wa joto ikiwa itamkosa mshambuliaji wa Norway Erling Haaland, 20, kutoka Borussia Dortmund. (ESPN)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Chelsea wanataka kumnunua mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero, 32, atakapoondoka Manchester City

Real Madrid wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Martin Odegaard, 22, ili kufadhili uhamisho wa Haaland. Odegaard kwa sasa anachezea Arsenal kwa mkopo na Gunners wanataka kumpatia mkataba wa kudumu. (Times)

Lakini Haaland ameripotiwa kuiambia Real Madrid kwamba anataka kuwa kikosi kimoja na Odegaard msimu ujao. (Star)

Barcelona huenda wakamnunua mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 23, ikiwa juhudi zao za kumsaka Haaland hazitafua dafu. (Sport)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Barcelona kumnunua mshambuliaji wa Inter na Argentina Lautaro Martinez wakimkosa Haaland

Paris St-Germain huenda wakamwachilia mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, msimu huu wa joto endapo mazungumzo kuhusu mkataba wake yataendelea kukwama. (Le Parisien)

Barcelona wanapania kusitisha kampeni yao ya kumsaka kiungo wa kati wa Liverpool Mholanzi Georginio Wijnaldum, 30, na badala yake kumpatia nafasi muhimu kinda wa Uhispania Ilaix Moriba,18, msimu ujao. (Metro)

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Paris St-Germain huenda wakamwachilia Kylian Mbappe wakishindwa kuafikiana kuhusu mkataba wake

Juventus wanataka kumrudisja mshambuliaji wa Everton na Italia Moise Kean, ambaye sasa yuko kwa mkopo Paris St-Germain. Kiungo huyo aliye na umri wa miaka 21-alijiunga na Toffees kutoka Juve mwaka 2019. (Tuttosport - in Italian)

Mkufunzi wa Tottenham Jose Mourinho anaamini mshambuliaji wa England Harry Kane, 27, imeridhia hali yake katika klabu hiyo licha ya tetesi kwamba hueda akaondoka msimu huu. (Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mchezaji wa kimataifa wa Ubelgiji Romelu Lukaku

Inter wanataka kusalia na mchezaji wa kimataifa wa Ubelgiji Romelu Lukaku lakini dau la £102m huenda likawalazimu kumuuza kiungo huo aliye na miaka 27. (Corierre dello Sport)

Leicester City, Crystal Palace, AC Milan na Sevilla wanamnyatia winga wa Marseille na Ufaransa Florian Thauvin, 28. (L'Equipe)