Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 05.04.2021: Neymar, Mbappe, Haaland, Messi, Rice, Soucek

Neymar na Mbappe

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Wachezaji wa PSG Neymar na Mbappe

Mshambuliaji wa Brazil Neymar, 29, ameingia makubaliano ya awali ya kuichezea Paris St-Germain mpaka mwaka 2026- na sasa klabu hiyo ya Ufaransa inafanya jitihada ya kufanya makubaliano kama hayo na mshambuliaji wa Kifaransa Kylian Mbappe,22. (Telefoot, via AS)

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland anaweza kuigharimu klabu kiasi cha pauni milioni 34 zaidi kwasababu wakala wake Mino Raiola na baba Alf-Inge wanahitaji pauni milioni 20 kwa kila kamisheni kama sehemu ya mkataba. (RAC1, via Marca)

Haaland ana kipengele cha uhamisho cha pauni milioni 64 kwenye mkataba wake ambacho kitaanza kufanya kazi mwakani lakini anaweza kuondoka msimu huu wa joto kama Dortmund wataendelea kufanya vibaya kwenye ligi ya Bundesliga na kuikosa ligi ya mabingwa. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland

Haaland, 20, amekuwa akihusishwa na taaarifa za kuhamia Barcelona lakini kocha Ronald Koeman amesema uamuzi wowote kuhusu uhamisho lazima ufanywe na rais Joan Laporta. (AS)

Lionel Messi anasubiri kuona ombi la Laporta kwa ajili ya mustakabali wa Barcelona kabla ya kuamua kusalia kwenye klabu hiyo au kujiunga na PSG au Manchester City. (Mundo Deportivo-in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images

Angel di Maria amesema angependa kucheza sambamba na Messi kwenye kikosi cha PSG ikiwa mshambuliaji huyo, 33 ataondoka Barcelona. (beIN Sports,via Goal)

Kocha wa Leicester Brendan Rodgers ana matumaini ya kumsajili kiungo wa kati Mskoti Callum McGregor,27, kutoka klabu ya Celtic. (Sun)

Kocha wa West Ham David Moyes amesema klabu hiyo itasikiliza ofa kwa ajili ya wachezaji Declan Rice,22, na kiungo wa kati wa Jamhuri ya Czech Tomas Soucek,26, msimu huu wa joto. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

West Ham kupokea ofa kwa ajili ya mchezaji Declan Rice na Tomas Soucek

Manchester United na Juventus ni vilabu vinavyoonesha nia zaidi ya kumnasa mshambuliaji wa Barcelona, Mfaransa Ousmane Dembele,23, lakini Liverpool na PSG nao wamekuwa wakimfuatilia mchezaji huyo. (Mundo Deportivo-in Spanish)

Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel amemrejesha beki wa kati Antonio Rudiger,23, kutoka mazoezini siku ya Jumapili baada ya kuzozana na mlinda mlango Kepa Arrizabalaga,26, baada ya kufungwa 5-2 na West Brom Jumamosi. (Telegraph-subscription required)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Wachezaji wa Barcelona, Lionel Messi na Ousmane Dembele

Winga wa Uhispania Lucas Vazquez,29, ambaye mkataba wake na Real Madrid unakwisha mwishoni mwa msimu, atapatiwa mikataba na Manchester United, Chelsea,AC Milan na Bayern Munich. (ABC-in Spanish)

Juventus hawana uwezekano wa kulipa pauni milioni 8.5 zaidi kwa Atletico Madrid kwa ajili ya kuongeza mkataba wa mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata kwa mwaka mmoja mwingine kwasababu ya changamoto za kifedha. (AS)

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata

Beki wa kati wa Everton na Colombia Yerry Mina,26, anataka kuhamia ligi ya Serie A msimu huu wa joto, huku Inter Milan na Fiorentina nao wakimtolea macho mchezaji huyo. (Sun)

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero, 32, hatajiunga nao baada ya mkataba wake na mahasimu wao Manchester City kumalizika mwishoni mwa msimu. (Goal)