Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 22.05.2021: Kane, Sterling, Aguero, Buendia, Llorente, Bale, Edouard

Mshambuliaji wa England Tammy Abraham

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa England Tammy Abraham

Chelsea wako tayari kutoa wachezaji kadhaa, pamoja na mshambuliaji wa England Tammy Abraham, 23, na kipa wa Uhispania Kepa Arrizabalaga, 26, katika ofa ya kubadilishana wachezaji pamoja na pesa ili kupata sahihi ya mshambuliaji wa Tottenham na Uingereza Harry Kane.(ESPN)

Mlinzi wa Arsenal Sead Kolasinac, 27, anatarajiwa kuondoka klabuni humo msimu huu wa joto, na Schalke na Lazio wakiwa mstari wa mbele kumtafuta mchezaji huyo wa kimataifa wa Bosnia na Herzegovina (Football.London)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Manchester City watafungua mazungumzo ya mkataba mpya na Raheem

Manchester City watafungua mazungumzo ya mkataba mpya na Raheem Sterling msimu huu wa joto licha ya mshambuliaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 26 kupoteza nafasi yake katika kikosi katika wiki za hivi karibuni. (Telegraph - subscription required)

Arsenal na Aston Villa wameongeza tena hamu yao kumsajili mchezaji wa Norwich mwenye umri wa miaka 24, Emiliano Buendia, ambaye anathaminiwa kugharimu kati ya pauni milioni 35 hadi pauni milioni 40. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Ufaransa 22, Kylian Mbappe

Real Madrid wana mpango wa kumsajili Paris-St Germain na mshambuliaji wa Ufaransa 22, Kylian Mbappe (Marca)

Wolves wanafanya mazungumzo na meneja wa zamani wa Benfica Bruno Lage juu ya kumrithi Mreno mwenzake Nuno Espirito Santo, ambaye ataondoka kilabuni humo baada ya mchezo wa Jumapili dhidi ya Manchester United (Guardian)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero, amekubali mkataba wa miaka miwili kujiunga na Barcelona

Mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero, 32, amekubali mkataba wa miaka miwili kujiunga na Barcelona wakati mkataba wake wa Manchester City utakapomalizika mwishoni mwa msimu. (Guardian)

Wolves wanamfuatilia Mreno Paulo Fonseca, ambaye ataondoka Roma msimu huu wa joto.(Mirror)

Maelezo ya picha,

Gareth Bale anafikiria kustaafu

Mchezaji wa Tottenham aliye katika uhamisho wa mkopo Gareth Bale, 31, anafikiria kustaafu mkataba wake wa Real Madrid utakapomalizika mwishoni mwa msimu ujao(AS)

Tottenham watajaribu kumshawishi bosi wa Leicester, Brendan Rodgers, 48, kuwa meneja wao mpya ikiwa wolves watashindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mlinzi wa Uhispania Diego Llorente

Leeds wanatarajia kupokea ofa kwa mlinzi wa Uhispania mwenye umri wa miaka 27 Diego Llorente msimu huu wa joto lakini hawana nia ya kumuuza.(Football Insider)

Leicester wanaongoza harakati za kumsajili mshambuliaji wa Celtic Odsonne Edouard, ingawa Arsenal, Newcastle na Aston Villa pia wanamtaka Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 23. (Daily Record)

Maelezo ya picha,

West Ham wanataka kusalia na Lingard

West Ham wanataka kusalia na mshambuliai anayewachezea kwa mkopo wa Manchester United na England Jesse Lingard, 28. (Mail)

Leeds wameanzisha mazungumzo na Manchester City juu ya mkataba wa kudumu wa kiungo wa kati wa Uingereza anayehudumu huko kwa mkopo Jack Harrison.(Star)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kocha ajaye wa Roma, Jose Mourinho ameionya Manchester United

Kocha ajaye wa Roma, Jose Mourinho ameionya Manchester United kwamba hatalipa kiasi cha juu cha fedha kuliko thamani yake kiungo wa Serbia mwenye umri wa miaka 32 Nemanja Matic. (Corriere dello Sport via Mirror)

Kocha wa Swansea Steve Cooper na meneja wa zamani wa Huddersfield David Wagner ni miongoni mwa wanaowania kumrithi Sam Allardyce huko West Brom.(Sky Sports)

Norwich waliopandishwa ngazi maajuzi kujiunga na ligi ya premia wanajitayarisha kuwasilisha ofa ya kumsajili winga wa Uingereza na Sheffield Wednesday mwenye umri wa miaka 28 Adam Reach. (Football Insider)

Unaweza pia kutazama.

Maelezo ya video,

Kocha wa Simba atangaza kisasi dhidi ya Kaizer Chiefs