Simba SC yashindwa kuguruma mbele ya Kaizeir Chiefs

Simba ndio walioanza utikisa nyavu mnamo dakika ya 43 ya mchezo

Chanzo cha picha, Simbasctanzania/Instagram

Maelezo ya picha,

Simba ndio walioanza utikisa nyavu mnamo dakika ya 43 ya mchezo

Mashabiki wa Simba na wadau wa soka Tanzania na Afrika Mashariki, bila shaka wamekata tamaa baada ya Simba kushindwa kuifunga magoli 5 kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, tiketi ambayo ingeiwezesha kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hata hivyo Simba FC ambao walikuwa wenyeji wa Kaizer Chiefs jijini Dar es Salaam wameonyesha mchezo wa kasi na kufanikiwa kufunga mabao 3, na kuweza kuwasisimua mashabiki wao waliokuwa wamejaa uwanja.

Simba iliweza kuleta matumaini wakati wa kipindi cha kwanza cha mechi hiyo kwa kufunga bao la kwanza dhidi ya Kaizer chiefs mnamo dakika ya 43, ikafunga la pili na la tatu, lakini haikutosha kuiwezesha kusonga mbele.

Chanzo cha picha, Simbasctanzania/Instagram

Maelezo ya picha,

Licha ya kufungwa, Simba SC walioesha mchezo wa kasi na wakusisimua mbele ya mashabiki wao

Mashabiki wa Simba walisubiri kwa hamu kuona kama Simba inaweza kurudia miujiza yao ya mwaka 1979.

Iwapo simba ingefunga magoli matano ndilo jambo pekee ambalo lingeweza kuiokoa na kuiwezesha kusonga mbele baada ya kupoteza mchezo wa kwanza ugenini huko Afrika Kusini kwa mabao 4-0. Hilo halikuwezekana.

Awali mashabiki wa simba walionekana wakimiminika kwa wingi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kushuhudia mechi hiyo ya kukata na shoka:

Maelezo ya picha,

Mashabiki walipimwa joto na kuvaa barakoa kabla ya kuingia uwanjani kutazama mechi