Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 23.07.2021: Jadon Sancho ,Kane, Mbappe, Pogba, Varane, Kessie, Hazard, Xhaka

sancho

Chanzo cha picha, Getty Images

Winga wa Uingereza Jadon Sancho anasema kujiunga na Manchester United ni "ndoto inayotimia" baada ya kumaliza uhamisho wake wa pauni milioni 73 kutoka Borussia Dortmund.

Sancho ndiye mchezaji wa pili mwenye gharama ya juu zaidi wa England wakati wakati wote nyuma ya mwenzake mpya wa United Harry Maguire.

Anajiunga na United kwa mkataba wa miaka mitano.

"Nitashukuru Dortmund kila mara kwa kunipa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, ingawa siku zote nilijua kwamba nitarudi England," Sancho, 21, alisema

"Nafasi ya kujiunga na Manchester United ni ndoto iliyotimia na siwezi kungojea kunawiri kwenye Ligi ya Premia.

"Hiki ni kikosi kichanga na cha kusisimua na najua, kwa pamoja, tunaweza kuendeleza kuwa kitu maalum cha kuleta mafanikio ambayo mashabiki wanastahili."

United ilikubali ada ya Sancho mnamo 1 Julai na mkataba wake wa miaka mitano na kilabu una chaguo la kuongezwa kwa miezi 12.

Kukamilika kwa makubaliano hayo kunamalizia harakati ya muda mrefu ya United ya kutafuta mchezaji wa zamani wa Manchester City Sancho waliyetarajia kumsaini msimu uliopita wa kiangazi lakini hawakuweza kukubalina kuhusugharama yake.

Sancho alifunga mabao 50 na kusaidiakufunga mabao 57 katika mechi 137 za Dortmund.

Kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer anasema Old Trafford itampa Sancho "jukwaa analohitaji kutoa talanta yake ambayo haijatumika".

"Jadon ni aina ya mchezaji ninayetaka kumleta kwenye kilabu - ni mchezaji wa mbele katika mitindo ya Manchester United," Solskjaer aliiambia tovuti ya kilabu.

"Atakuwa sehemu muhimu ya kikosi changu kwa miaka ijayo na tunatarajia kumuona akinawiri. Mabao yake yake na rekodi za kusaidia zinajisamamia na pia ataleta kasi kubwa, uzuri na ubunifu kwa timu.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kurudi kwa Sancho kwenye ligi ya England kunakuja baada ya kuisaidia timu ya taifa kufika fainali ya Mashindano ya Euro , ambapo walishindwa kwa penati na Italia.

Mchezaji huyo wa zamani wa vijana wa City, pamoja na Bukayo Saka na sasa mwenzake wa United Marcus Rashford, walilengw akatika ubaguzi wa rangi kwenye mitandao ya kijamii baada ya kushindwa kufunga bao kwenye mikwaju ya penalti

Kuhamia kwa Sancho kwenda Old Trafford kutamfanya ajiunge na mwenzake wa England Rashford, lakini pia Edinson Cavani, Anthony Martial na Mason Greenwood kwa kile kinachoweza kuwa safu hatari ya ushambulizi ya timu ya Solskjaer.

Sancho alifunga mabao 16 katika mashindano yote wakati wa msimu wa 2020-21, tano chini ya Rashford, lakini nne zaidi ya Greenwood, na tisa zaidi ya Martial. Cavani, ambaye alijiunga na United kwa uhamisho wa bure mwaka jana baada ya kuondoka Paris St-Germain, alitikisa nyavu mara 17.

Katika misimu minne huko Dortmund, Sancho alisadia katika kufunga mabao 57 na akaunda nafasi 65 kubwa, zaidi ya Rashford, Martial, Greenwood na Cavani katika kipindi hicho hicho.

Sancho pia yuko vizuri ikilinganishwa na majina makubwa huko Uropa.

Tangu kuanza kwa msimu wa 2018-19, ni wachezaji saba tu ambao wana mabaoa na kusaidia kufunga mengine mengi kumliko nyota huyo wa kimataifa wa England. Kati ya wachezaji hao, ni Lionel Messi (43) wa Barcelona tu ndiye ameunda mabao mengi kuliko Sancho (41) wakati huo(BBC Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Manchester City iko tayari kuwapoteza wachezaji kadhaa ili kuishawishi Tottenham kumuuza Harry Kane.

Manchester City wako tayari kumtoa mmoja wa wachezaji nyota akiwemo mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus, 24, nahodha wa Algeria Riyad Mahrez, 30, kiungo wa Ureno Bernardo Silva, 26, au mshambuliaji wa Uingereza Raheem Sterling, 26, kama sehemu ya mpango wa kuishawishi Tottenham kuwauzia nahodha wa Uingereza Harry Kane. (FourFourTwo)

Kane atapokea kitita cha pauni 400,000-kwa-wiki atakapojiunga na Manchester City baada ya mwenyeiti wa Tottenham Daniel Levy kuidhinisha kuondoka kwake wiki iliyopita. (Sun)

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, hatakubali mkataba mpya Paris St-Germain kwani anajiandaa kuhamia Real Madrid, licha ya klabu hiyo ya Ufaransa kutaka kumuunganisha na mchezaji mwenzake wa kimataifa Paul Pogba. (Marca - in Spanish)

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Kylian Mbappe hana mpango wa kusaini mkataba mpya PSG

Pogba anatarajiwa kuondoka Manchester United msimu huu wa joto baada ya kukataa mkataba wa pauni milioni 350 kwa wiki licha ya klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Premia kutaka akamilishe mkataba wake wa sasa na kuondoka 2022. (Mirror)

Manchester United pia wanang'ang'ana kufikia makubaliana na Real Madrid kumsajili beki wa Ufaransa Raphael Varane, 28. Klabu hiyo ya La Liga inataka kulipwa £50m kumuachilia mlinzi huyo huku United wakiwa tayari kulipa £40m. (Mirror)

Liverpool ni miongoni mwa klabu kadhaa za Ulaya zinazotafakari uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa AC Milan na timu ya taifa ya Ivory Coast Franck Kessie, 24. (Gazzetta dello Sport)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kessie

Newcastle wana imani ya kumpata kiungo wa kati wa Southampton na Gabon Mario Lemina, 27, baada ya kufanya mazungumzo na wachezaji kadhaa wa safu ya kati ambao bei yao iko nje ya viwango vya mshahara wa klabu hiyo. (Northern Echo)

Eden Hazard, 30, tayari ameonesha wazi hisia zake kwamba kurejea kwake Chelsea haina mjadala baada ya vyombo vya habari vya Uhispania kuripoti kuwa Real Madrid inatafuta njia ya kumuuza. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Eden Hazard asema kurejea kwake Chelsea haina mjadala

Arsenal imeambiwa na Sheffield United kuongeza ofa ya kumnunua Aaron Ramsdale ,32, kwa hadi pauni milioni 32 baada ya kukataa mara mbili dau la kumuuza kipa huyo. (Times - usajili unahitajika)

Chelsea pia wanamtaka kipa Muargentina Sergio Romero, 34, baada ya mkataba wake na Manchester United kukamilika,huku the Blues wakiendelea kumtafuta mchezaji wa tatu ambaye anaweza kushikilia nafasi ya Edouard Mendy na Kepa Arrizabalaga. (Telegraph - usajili unahitajika)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Xhaka amekuwa Arsenal tangu mwaka 2016

Kiungo wa kati wa Arsenal Granit Xhaka anakaribia kukamilisha uhamisho wake kwenda Roma baada ya klabu hiyo ya Serie A kuonesha ishara kwamba inamtaka ajiunge nao katika mechi ya kabla ya msimu huko Portugal wiki ijayo. (Daily Mail)

Aston Villa huenda wakawasilisha ofa ya kumnunua mshambuliaji wa River Plate na timu ya taifa ya Argentina Julian Alvarez wiki ijayo. (TNT Sports - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kristoffer Ajer mlinzi wa Celtic aliyenyakuliwa na Brentford ya Norway

Mlinzi wa Tottenham na Marekani Cameron Carter-Vickers, 23, huenda akajiunga na Newcastle, ambao wanamtafuta mchezaji wa safu ya kati na nyuma baada ya Brentford kushinda kinyang'anyiro cha kumsajili mlinzi wa Celtic na timu ya taifa ya Norway Kristoffer Ajer, 23. (90Min)