Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 31.07.2021: Grealish, Mbappe, Pogba, Locatelli, Simy, Ward-Prowse, Bowen, Dumfries

Jack Grealish

Chanzo cha picha, Getty Images

Aston Villa watampa ofa ya mkataba mpya kiungo wa kati Jack Grealish, 25, wa thamani ya pauni 200,000 kwa wiki ili aendelee kusalia na klabu hiyo na kumzuia asielekee Manchester City,ambayo imetangaza dau la pauni milioni 100 kumnasa mchezaji huyo. (Star)

Real Madrid wataanza mazungumzo na Paris St-Germain majuma kadhaa yajayo kwa ajili ya mshambuliaji Kylian Mbappe,22, ambaye mkataba wake utakwisha msimu ujao wa majira ya joto. (90min)

Chanzo cha picha, EPA

Kiungo wa kati wa Manchester Paul Pogba,28, ambaye kwa kiasi kikubwa amehusishwa na taarifa za kuhamia Paris St-Germain, anaweza akashuhudia mustakabali wa muda mrefu Old Trafford, lakini Mfaransa huyo anaweza asisaini mkataba mpya na mashetani wekundu. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images

Tottenham imetangaza ofa kwa Atlanta ya pauni milioni 43 kwa ajili ya Muajentina Cristian Romero, 23, na timu hiyo ya Italia wako tayari kupokea dili kama wanaweza kuwa na muda zaidi wa kumpata mbadala wake. (Sky Sports Italia, via Mail)

Kiungo mchezeshaji wa Colombia James Rodriguez amesema hana uhakika kama atasalia Everton lakini mchezaji huyo mwenye miaka 30 amekataa kurudi Real Madrid. (Mail)

Kiungo wa Borussia Monchengladbach na Ujerumani Florian Neuhaus, 24, amesalia kuwa lengo la kocha wa Liverpool Jurgen Klopp, lakini Reds hawatakuwa tayari kufikia gharama ya karibu pauni milioni 34.(Sport1 - in German)

Liverpool imejiunga na Juventus na Arsenal katika mbio za kumnasa kiungo wa kati Manuel Locatelli, 23, wa Sassuolo.(Gazzetta dello Sport, via Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Southampton imekataa ofa ya pauni milioni 25 kutoka kwa Aston Villa kwa ajili ya kiungo wa kati James Ward-Prowse, 26. (Athletic - subscription required)

Chelsea wanajiandaa kushusha gharama ya pauni milioni 40 kwa ajili ya mashambuliaji wa Kiingereza Tammy Abraham, ambaye anaivutia Arsenal, West Ham na Aston Villa. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Everton bado hawajaamua kuhusu mlinzi wa Uholanzi Denzel Dumfries, 25, anayekipiga PSV Eindhoven.(Liverpool Echo)

Vyanzo vya juu huko Liverpool havikatai uhusiano na mshambuliaji wa Kiingereza anayekipiga West Ham Jarrod Bowen. (Star)

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal wanajiandaa kumpa mkataba mpya kiungo wa kati Granit Xhaka, 28, baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswizi kuhusishwa na taarifa za kuhamia Roma.(Athletic - subscription required)

Leeds United wako kwenye mazungumzo ya awali kuhusu kumsajli kiungo Lewis O'Brien, 22, wa Huddersfield Town. (Football Insider)

Crystal Palace, Brentford na Watford wamehusishwa taarifa za kutaka kumnasa mchezaji kiungo Matthew Garbett, 19, anayecheza klabu ya Uswidi. Falkenbergs. (Sun)