Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 09.08.2021: Messi, Trippier, Haaland, Icardi, Griezmann, Origi, Dzeko, Cunha,Willock

Lionel Messi

Chanzo cha picha, Getty Images

Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Uhispania Barcelona Lionel Messi amesema kwamba kuna uwezekano akajiunga na PSG , lakini kufikia sasa hakuna makubaliano yalioafikiwa wakati alipokuwa akithibitisha kuondoka katika timu hiyo aliojiunga nayo akiwa mtoto.

Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 34, amepangwa kufanyiwa vipimo vya matibabu hii leo Jumatatu kabla ya kukamilisha uhamisho wa bure kwenda Paris St-Germain. (L'Equipe - in French)

Messi atazinduliwa kama mchezaji wa PSG kwenye hafla maalum katika Mnara wa Eiffel katika siku chache zijazo.(ESPN)

Barcelona wanajaribu kuzuia jaribio lolote la PSG kumsaini Messi kwa kufungua malalamiko kwa Tume ya Ulaya ikisema kilabu hiyo ya Ufaransa itakiuka sheria za matumizi ya fedha ikiwa watafanikiwa kumsajili Muargentina huyo. Kampuni hiyo inadai kwamba hali ya kifedha ya fair Play katika klabu hiyo ni mbaya zaidi ya Barcelona. Malalamishi hayo yaliowasilishwa pia yanaelezea kwanini Messi hakuweza kutia saini kandarasi mpya katika klabu ya Barcelona, hata iwapo mchezaji huyo angechukua mshahara nusu ya anaolipwaa kwasasa. (Marca, in Spanish)

Tottenham ni miongoni mwa vilabu ambavyo vimejaribu kumsajili Messi baada ya Barca kusema hatosalia Nou Camp. (Express)

Chanzo cha picha, Getty Images

Newcastle wamekubaliana na Arsenal kuhusu ada ya zaidi ya pauni milioni 20 kumsajili kiungo Joe Willock.

Kocha Magpies Steve Bruce hajafnya siri hamu yake ya kumsaini mchezaji huyo wa miaka 21 kwa mkataba wa kudumu baada ya ufanisi akiwa kwenye mkopo msimu uliopita.

Willock alifunga katika michuano saba mfululizo ya Ligi ya premia ili kusaidia kuiondoa klabu kutoka hatari ya kushushwa ngazi tangu kujiunga nao mwezi januari (BBC SPORT)

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal iko tayari kufanya kufanya usajili wa beki wa Atletico Madrid Kieran Trippier kwani Manchester United imeshindwa kukubaliana ada na mabingwa wa Uhispania kwa mchezaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 30. (Sun)

Kocha wa Roma, Jose Mourinho anataka sana kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain wa Argentina mwenye umri wa miaka 28, Mauro Icardi, huku Edin Dzeko wa Bosnia, 35, akionekana kukaribia kuondoka mji mkuu wa Italia kwenda Inter Milan. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Dzeko anakaribia kuhamia San Siro kama mbadala wa mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 28, ambaye yuko mbioni kurudi Chelsea. (sun)

Arsenal inashindana na Tottenham kuwania saini ya mshambuliaji wa Fiorentina wa Serbia Dusan Vlahovic, huku Spurs ikimtaka mchezaji huyo wa miaka 21 kama mbadala wa Harry Kane, ambaye anatafutwa na Manchester City. (Sky Sport Italia's Gianluca Di Marzio - in Italian)

Chanzo cha picha, Getty Images

Southampton wanajaribu kumsajili tena kiungo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 27 wa Liverpool Alex Oxlade-Chamberlain, miaka 10 baada ya kuondoka St Mary's. .(Sun)

Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich Hasan Salihamidzic amethibitisha kuwa kilabu hiyo ya Ujerumani ina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Norway mwenye umri wa miaka 21 Erling Braut Haaland kutoka kwa wapinzani wao wa Bundesliga Borussia Dortmund. (Goal)

Manchester United wanajiandaa kutoa ombi la kupata huduma za mshambuliaji wa Ufaransa wa miaka 30 Antoine Griezmann. (Todofichajes - in Spanish)

Porto, West Ham, Leeds na Norwich wamehusishwa na kiungo wa kati wa Uingereza mwenye umri wa miaka 18 Fabio Carvalho, ambaye alikataa ofa ya kwanza ya kuongeza mkataba na Cottagers.(Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Leicester City inaweza kurudia harakati zao za kumsajili mlinzi wa Southampton Jannik Vestergaard, 29, ili kuiziba nafasi ya Wesley Fofana aliyejeruhiwa. West Ham pia imehusishwa na raia huyo wa Denmark (Talksport)

Leeds United bado wana hamu ya kumsaini kiungo wa Hertha Berlin Matheus Cunha, 22, ambaye alishinda dhahabu ya Olimpiki na Brazil huko Tokyo Jumamosi. (Star)

Atalanta pia imehusishwa na Cunha, ambaye thamani yake imeongezwa hadi pauni milioni 25 na Hertha baada ya mafanikio yake huko Japan. (Calciomercato - in Italian)

Burnley wamehusishwa na winga wa Santos mwenye umri wa miaka 23, Arthur Gomes, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Atletico Goianiense. (Burnley Express)

Barcelona wamemkabidhi kipa Neto mwenye umri wa miaka 32 kwa vilabu vya kaskazini mwa London vya Arsenal na Tottenham. (Express)

Chanzo cha picha, Getty Images

West Ham wapo kwenye mazungumzo ya mwanzo kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi mwenye umri wa miaka 26 kutoka Liverpool. (Football Insider)