Cristiano Ronaldo: Je ni nini kilichomfanya mchezaji huyo kuondoka Italia?

ronaldo

Chanzo cha picha, Getty Images

Yeye ni mmoja wa wachezaji bora wakati wote, lakini akiwa amesalia na mwaka mmoja katika mkataba wake, Juventus wako tayari kumuuza Cristiano Ronaldo.

Manchester City ni moja ya vilabu ambavyo viliwasiliana na wakala wa Ronaldo Jorge Mendes, na ripoti zingine zinaonyesha kuwa masharti ya kibinafsi tayari yamekubaliwa.

Inaleta uwezekano wa hapo awali wa mshindi huyo mara tano wa Ballon D'or kwamba anaweza kucheza kwa wapinzani was City, Manchester United, kilabu cha Uingereza ambacho kilikuwa chini ya Sir Alex Ferguson kati ya 2003 na 2009, na kwa Pep Guardiola, alikiwa mpinzani mkubwa Lionel Messi.

Kwanini basi ghafla ameanza kuangaziwa - na je atafaa Manchester City ikiwa makubaliano hayo yatafikiwa kabla ya tarehe ya mwisho ya uhamisho wa Jumanne.

Timu ya wataalam wa Uropa ya Redio 5 Live - Raphael Honigstein, Julien Laurens na Kristof Terreur - wamekuwa wakijadili maswali haya na zaidi:

Kwa nini Juventus wanataka kumwondoa Ronaldo?

Chanzo cha picha, Getty Images

Ronaldo, 36, anajulikana kughadhabishwa na jinsi uhamisho wake kwenda Juventus ulivyobadilika.

Miamba hao wa Italia hawajafika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa tangu kuwasili kwake Turin na kilabu cha Serie A kimeshindwa katika hatua ya 16 bora katika kampeni mbili zilizopita.

Msimu uliopita, walipoteza taji lao la ligi baada ya kushinda kwa miaka tisa mfululizo na kuingia tu kwenye nafasi za Ligi ya Mabingwa katika michezo michache iliyopita.

Ronaldo aliachwa nje na mkufunzi Massimiliano Allegri wakati Juventus ikitoka sare kwenye Serie A katika mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Udinese - kitu ambacho kilabu kilisisitiza ni uamuzi wa pamoja na mchezaji huyo.

Honigstein: "Juventus wanajitahidi kumuuza Ronaldo na hata kuna mazungumzo juu yake labda aende kwa uhamisho wa bila malipo kwasababu wana hamu kubwa ya kumwondoa kwenye mshahara huku kifikra zao wakiangazia mchango wake mdogo katika timu - kwamba hautoshi.

"Aliulizwa James Horncastle ikiwa Juventus wana nguvu na Ronaldo au bila Ronaldo kwenye Ligi ya Mabingwa na hakusita kusema "bila Ronaldo".

Hivyo ndivyo Juventus inavyofikiria juu yake kwa sasa na sio kwasababu za kifedha tu.

Inafurahisha sana kwamba City na Guardiola wanafikiria kwamba kwa namna fulani atakuwa kipande kinachokosekana ambacho kinasimama kati yao na Ligi ya Mabingwa wakati haikufanikiwa kuwa hivyo huko Juventus.

Laurens: "Ikiwa wewe ni Juventus na unaijua City inamtaka na unajua kwamba City wamekaa pauni milioni 150 ambazo zilikuwa tayari kwa Harry Kane, Juventus wanahitaji pesa hizo kuingia ili wasipoteze wakati wote wa Cristiano Ronaldo kuwa klabuni. Nadhani hili litatatuliwa haraka sana."

Je! Anaendana na falsafa ya Guardiola?

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ronaldo na Guardiola

Mara kadha Guardiola amekuwa akipendelea kucheza bila mshambuliaji wa kati. Alipofika City, alisisitiza juu ya kuongezeka kwa kazi kutoka kwa Sergio Aguero kusaidia kukabiliana na wapinzani kutoka mbele. Hili sio jambo ambalo Ronaldo amekuwa akitaka kufanya katika misimu ya hivi karibuni.

Laurens: "Swali liko sawa - je, Ronaldo anaendana kweli na mpira wa Pep, na falsafa ya Pep?

Nadhani sisi sote tunakubali ni "hapana" zaidi kuliko "ndiyo". Lakini unajua atafunga mabao mengi kwasababu watamtengenezea nafasi nyingi, hata kama hatafanya kila kitu atakachoagizwa na Pep. "Tunajua Pep ataondoka mwishoni mwa mkataba wake katika muda wa miaka miwili kwa hivyo ni chaguo la muda mfupi hata hivyo.

Labda ukifuata njia hiyo basi pia utafanya ifanye kazi kwa Cristiano kwa muda mfupi na labda ni Pep ambaye pia atabadilika kidogo kuwa na Cristiano katika timu yake, mradi Cristiano ageuze mchezo wake mwenyewe kwendana na kile Pep anataka".

Honigstein: "Haikuingii akilini kama mtu ambaye ni mchezaji wa Pep". Haikuingii kama yeye ni mtu ambaye anataka kucheza katika mfumo wa ushirikiano. Ni ya kushangaza, lakini inafurahisha sana kwetu sote kuona jinsi atakavyocheza.

"Kwa timu ambayo ilikuwa na ufanisi mkubwa wakati wa Ligi ya Premia, kwa timu ambayo ilikuwa karibu kushinda Ligi ya Mabingwa, Guardiola kwa njia fulani anajishawishi mwenyewe kwamba anamhitaji Jack Grealish na Harry Kane kukamilisha fumbo. Hiyo inaonekana kuwa ya kushangaza na sasa kwenda kwa Cristiano Ronaldo inaonekana kuwa hatua ya kushangaza hata zaidi. Sikuweza kutafakari kwamba City ingemwendea, na sasa hapa tuko karibu na kufikia hatua hii inayotokea."

Terreur: "Ni ya kushangaza na inaonekana kama hatua ya kurukia. Sijaona vilabu vikimsaini chaguo la B ambaye hafai kwa kile walichokuwa wanatafuta. Sielewi hilo, lakini kwa kweli litaongeza kiwango cha biashara na yeye atafunga mabao mengi. Lakini sio mawazo ya muda mrefu na hiyo ilikuwa kitu ambacho City ilionekana kuwa mzuri nacho siku za nyuma.

Je! kumsajili Ronaldo kutaathiri mpango wowote wa Haaland kwenda Man City?

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Haaland na ameusishwa na uhamisho wa kuelekea Manchester City

Mshambuliaji wa Norway Erling Braud Haaland anaaminika kuwa na kifungu cha kuruhusiwa kuondoka timu hiyo kwa pauni milioni 64 katika mkataba wake utakaoanza kutekelezwa msimu ujao, na hapo awali Guardiola amezungumza juu ya hamu yake ya kumsaini mchezaji huyo wa miaka 21.

Honigstein: "Sidhani kumsaini Ronaldo kutasitisha City kumtafuta Haaland, lakini inaweza kumizuia Haaland akisema "City ni chaguo zuri kwangu". Kumbuka kuwa alihamia Dortmund sio kwasababu walilipa pesa nyingi zaidi au walikuwa wazuri zaidi kuliko vilabu vingine ambavyo vilivutiwa naye, lakini kwasababu walikuwa kilabu kilichosema kilikuwa na nafasi katika nambari tisa.

"Wanaweza kumhakikishia kuwa muhimu katika timu. Ikiwa Ronaldo yuko hapo itakuwa vigumu kiasi kwa Pep na City kusema hoja hiyo kwa ushawishi na kujiamini".