Tetesi za soka Ulaya Jumapili tarehe 05.09.2021: Salah, Ronaldo, Foden, Camavinga, Neymar, Kessie

h

Manchester City itaongeza mara nne mshahara wa mchezaji wa England Phil Foden mwenye umri wa miaka 21 wakati wanatafuta kumfunga kilabuni hapo kwa kumpa mkataba mpya. (Star)

Chanzo cha picha, PA Media

Mshambuliaji wa Liverpool na Misri Mohamed Salah, 29, ameitisha pauni 500,000 kwa wiki ili kutia saini kandarasi mpya Anfield. (Mirror)

Paris St-Germain ilizungumza na Cristiano Ronaldo kuhusu uhamisho kutoka Juventus msimu huu wa kiangazi, lakini hakuna ofa yoyote iliyotolewa, na kumfanya mshambuliaji huyo wa Ureno, 36, kurudi Manchester. (Goal)

Romelu Lukaku, 28, amesema kilabu yake ya zamani Inter Milan ilimtoa kwenye "shimo refu" baada ya kuondoka Manchester United mnamo 2019. Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji alijiunga na Chelsea msimu huu wa joto. (Daily Mail)

Real Madrid ilikuwa ikimfuatilia kiungo wa Ufaransa Eduardo Camavinga, 18, kwa miaka mitatu kabla ya kumsajili kutoka Rennes msimu huu wa joto. (Marca)

Matumaini ya Tottenham kumsaini winga wa Uhispania, Adama Traore, 25, mnamo Januari yamepata pigo baada ya kufungua mazungumzo ya mkataba na kilabu yake ya sasa ya Wolves. (Express)

Chanzo cha picha, AFP

Kumsaini nyota wa Brazil Neymar, 29, kutoka Barcelona mnamo 2017 kumeigharimu PSG pauni milioni 489 katika ada na mshahara wake. (Marca)

Chanzo cha picha, Gety

Winga wa zamani wa Bayern Munich na Ufaransa Franck Ribery atasaini mkataba na kilabu ya Serie A Salernitana wiki ijayo. Nyota huyo wa miaka 38 amekuwa huru tangu aondoke Fiorentina. (Fabrizio Romano)

Tottenham na Chelsea zimepewa tahadhari baada ya kiungo wa Ivory Coast Franck Kessie, 24, kukataa kandarasi mpya na AC Milan (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Rais wa Barcelona Joan Laporta ana imani kamili na meneja Ronald Koeman na hana mpango wa kumtimua. (Sport)