Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 06.09.2021: Salah, Rodriguez, Elneny, Mbappe, Onana

Leroy Sane

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Leroy Sane

Mkufunzi wa Chelsea Thomas Tuchel anafikiria kumsajili aliyekuwa winga wa Manchester City raia wa Ujerumani Leroy Sane, 25, kutoka klabu ya Bayern Munich. (Express)

Kiungo wa kati wa Everton na Colombia James Rodriguez amehusishwa na uhamisho wa kwenda Istanbul Basaksehir, klabu hiyo ya Uturuki inapania kumsajili mchezaji huyo wa miaka 30- kabla ya dirisha lao la uhamisho kufungwa Jumatano wiki hii. (Footmercato - in French)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Liverpool hawajamuachilia Mohamed Salah kushiriki mechi ya ufungizi ya Misri katika kundi F dhidi ya Angola

Liverpool wanaendelea kuzungumza na wawakilishi wa Mohamed Salah kuhusu mkataba mpya wa mshambuliaji nyota huyo wa Misri aliye na miaka 29. (Liverpool Echo)

Mkufunzi wa Sevilla Julen Lopetegui anasema klabu hiyo ya La Liga huenda ikamzuia beki Mfaransa Jules Kounde, 22, kuhamia Chelsea msimu huu wa joto. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Arsenal kutoka Misri Mohamed Elneny anaendelea kuhusishwa na tetesi za uhamisho wa kwenda Besiktas, lakini mashariti ya marupurupu ya mchezaji huyo wa miaka 29- yanasemekana kuchangia kusambaratika kwa mpango huo. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kiungo wa kati wa Everton na Colombia James Rodriguez

Mkurugenzi wa soka wa Ajax Marc Overmars amesema kipa wa Cameroon Andre Onana, ambaye anasakwa na Arsenal, huenda akaondoka msimu ujao kwa mkataba wa bila malipo. (Team Talk)

Mabingwa wa Italia Inter Milan huenda pia wakamnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25-wanapomtafuta atakayemrithi kipa wa Slovenia Samir Handanovic, 37. (Calciomercato - in Italian)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Ufaransa na PSG Kylian Mbappe

Paris St-Germain wana matmaini kwamba mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe atajitolea kikamilifu kutekeleza mkataba wake mpya licha ya azma ya kiungo huyo wa miaka ya 22-kutaka kujiunga na Real Madrid kwa uhamisho wa bure msimu ujao. (Athletic - subscription required)

Arsenal inakabiliwa na hatari ya kupata hasara kubwa baada ya kushindwa kumuuza mshambuliaji wa miaka 22 Eddie Nketiah , huku mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa England wa chini ya miaka 21 akikataa ofa ya kandarasi kutoka kwa Gunners. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Kiungo wa kati wa Huddersfield Town Muingereza Lewis O'Brien ,22, ambaye pia alitakiwa na Leeds United msimu uliopita, anajadiliana na Terriers kuhusu mkataba mpya. (Huddersfield Examiner)

Tetesi Bora Jumapili

Paris St-Germain ilizungumza na Cristiano Ronaldo kuhusu uhamisho kutoka Juventus msimu huu wa kiangazi, lakini hakuna ofa yoyote iliyotolewa, na kumfanya mshambuliaji huyo wa Ureno, 36, kurudi Manchester. (Goal)

Chanzo cha picha, BBC Sport

Romelu Lukaku, 28, amesema kilabu yake ya zamani Inter Milan ilimtoa kwenye "shimo refu" baada ya kuondoka Manchester United mnamo 2019. Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji alijiunga na Chelsea msimu huu wa joto. (Daily Mail)

Manchester City itaongeza mara nne mshahara wa mchezaji wa England Phil Foden mwenye umri wa miaka 21 wakati wanatafuta kumfunga kilabuni hapo kwa kumpa mkataba mpya. (Star)

Matumaini ya Tottenham kumsaini winga wa Uhispania, Adama Traore, 25, mnamo Januari yamepata pigo baada ya kufungua mazungumzo ya mkataba na kilabu yake ya sasa ya Wolves. (Express)

Kumsaini nyota wa Brazil Neymar, 29, kutoka Barcelona mnamo 2017 kumeigharimu PSG pauni milioni 489 katika ada na mshahara wake. (Marca)