Tetesi za soka Ulaya Jumanne 14.09.2021: Zlatan Ibrahimovic, Pogba, Bellingham, Rice, Werner, Lingard, Bastoni, Kessie

Zlatan Ibrahimovic

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Zlatan Ibrahimovic amefunga katika misimu tofauti ya ligi 24 - kuanzia mwaka 1998-99

Mshambuliaji wa AC Milan Zlatan Ibrahimovic atakosa mechi ya ufunguzi ya Kundi la Ligi ya Mabingwa huko Liverpool kwa sababu ya shida ya misuli ya mguu.

Ibrahimovic, ambaye anatimiza miaka 40 mnamo Oktoba, alifunga bao baada ya kurejea uwanjani kwa mara ya kwanza tangu apone jeraha katika ushindi wa Serie A Jumapili dhidi ya Lazio.

"Baada ya mechi alikuwa na uvimbe," Kocha wa timu ya Italia Stefano Pioli, " amesema.

"Tulitarajia angeweza kucheza lakini bado alikuwa na maumivu kwa hivyo hatutaki kuhatarisha [kumchezesha]."

Mabingwa mara saba wa Uropa, Milan wanaonekana kwa mara ya kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa tangu mwaka 2014 na kuelekea Anfield wakiwa na rekodi ya 100% baada ya kushinda mechi zao tatu za kwanza msimu huu.

Kabla ya habari kwamba mshambuliaji huyo wa Sweden hatasafiri kwenda Merseyside, meneja wa Liverpool Jurgen Klopp alikuwa amesifu ubora wake wa kudumu.

Chanzo cha picha, Mirror/Twitter

Maelezo ya picha,

Cristiano Ronaldo na Pogba

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 28, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kujiunga na PSG na Real Madrid, anelekea kuongeza kandarasi yake katika klabu ya Man United baada ya Cristiano Ronaldo kurudi Old Trafford. (Athletic, subscription required)

Ingeligharimu dau la yuro milioni 100 ama zaidi kwa klabu ya Borussia Dortmund kumruhusu kiungo wa kati mwenye umri wa miaka 18 Jude Bellingham kuondoka , huku klabu za Manchester City na Liverpool zikidaiwa kuwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo wa England.. (Bild - in German)

West Ham, kama Dortmund, pia imemuwekea bei nyota wao . The Hammers inataka sio chini ya £100m kumuuza kiungo wa kati wa England Declan Rice, 22. (football.london)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Declan Rice

Chelsea inajiandaa kumpatia kandarasi mpya kiungo wa England Mason Mount , hatua ambayo huenda ikamfanya mshahara wake kuongezeka hadi £150,000 kwa wiki. (90min)

Mchezaji wa zamani wa Manchester United na England Axel Tuanzebe, 23, anataka kuufanya uhamisho wake wa mkopo katika klabu ya Aston Villa kuwa wa kudumu.. (Sun)

Bayern Munich inataka kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani na Chelsea Timo Werner, 25, Januari. (Football Insider)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Timor Werner

Leicester City ina hamu ya kumsajili kiungo wa Manchester United na England Jesse Lingard. (Fichajes - in Spanish)

Chelsea inaweza kuwanyatia mabeki wa Inter Milan na Itali Alessandro Bastoni 22 na raia wa Slovakia Milan Skriniar (Mediaset - in Italian)

Tottenham imewasilisha ofa ya kumsajili kungo wa kati wa AC Milan Franck Kessie, 24, ijapokuwa haijulikani iwapo Spurs itawasilisha ombi hilo mwezi Januari au kusubiri kumsaini mchezaji huyo wa Ivory Coast katika uhamisho wa bila malipo mwezi January (Calciomercato, in Italian)